Wajamani, "it feels good 2 know ur limits."

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,653
Points
2,000

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,653 2,000
Waswahili hulonga..."penye chokochoko.."
Usiache kupapulizia papoe, pakitulia...
Basi ujue mambo yamejipa na ni shwari..
Pakiendelea kufurukuta basi elewa kazi ipo
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

Wengi huamini ukikaza musuli utafanikiwa,
Wengi hujidanganya, "the sky is the limit"
Wengi hujipooza, lolote lawezekana.............
Lakini ukweli wabakia tunayo mipaka ya nguvu..
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

Kauli na makeke huwa hayatupiti........
Tunapopigwa chini huanza kutafuta visingizio......
Lawama kibao kwa wengine, huku kwetu ni ukimya..
Hivi tatizo ni wao au ndoto zetu zisizotekelezeka?
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

Tambua mipaka yako utaishi kwa miraha..
Karaha kwako kando kwani utapanga mipango fanikika
Watakaokucheka zao ni arobaini kwani wataumbuka
Usitawaliwe na kauli za wengine ila misimamo yako
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

"Kisukari kubwa" na kiharusi kwako itakuwa mwiko
Kwa sababu unakula kulingana na mkono wako
Kujilinganisha ni mtego wewe sasa umeukwepa
Kwani kila mmoja alizaliwa kivyake-vyake..
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

I am beginning to feel like it is X-MAS..............
 

Ndallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
7,572
Points
2,000

Ndallo

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
7,572 2,000
"Kisukari kubwa" na kiharusi kwako itakuwa mwiko
Kwa sababu unakula kulingana na mkono wako
Kujilinganisha ni mtego wewe sasa umeukwepa
Kwani kila mmoja alizaliwa kivyake-vyake..
Wajamani,
Ruta nani amekuudhi wajameni?
 

Forum statistics

Threads 1,390,169
Members 528,095
Posts 34,044,557
Top