Mwita Waitara: Kumekuwa na mzaha mzaha, hata Rais ametoa maagizo watu wanaibuka wanazungumza mambo yao

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara: Kumekuwa na mzaha mzaha, unatoa maelekezo hata mheshimiwa Rais juzi ametoa maagizo watu wanaibuka wanazungumza mambo yao ambayo kwakweli ni makosa makubwa sana.

Sisi tunatakiwa kupata muongozo kwa kiongozi mkuu wa Nchi, Rais ni Taasisi, sasa kama amejiridhisha kwenye vyombo kwa jambo hili la chanjo ni jambo salama tena amesema itakuwa chanjo ya hiari.

Sasa kama hutaki, usitoe kupotosha watu wengine, tunaanza kudeal na contradictions, mwingine akisikia kutokana na nafasi yako ataamini wewe ndio uko sawa, sasa sisi kama serikali na sisi watanzania nchi hii inaongozwa na sheria, msemaji mkuu wa nchi ni Rais.
 
Tunapokosea ni pale ambapo hatusemi ukweli,sioni sababu ya kumuogopa yule anayepotosha wananchi.

Kama Waziri Naibu sema kwa herufi kubwa kwamba Askofu Gwajima ni mpotoshaji ktk swala la Corona.

CCM ....Gwajima ni mbunge wenu na amekwenda kinyume kabisa kabisa na Mh Rais ktk swala la Corona mpaka kutamka maneno yaliyotuudhi...kwa nini hamumfukuzi chamani na ubunge pia.

Kuna mengi ya upotoshaji na uwongo amekuwa akiyasema since akiwa ktk Campaign za ubunge.Huyu apigwe chini fasta tumrudishie Halima wetu kiti chake.
 
Tunapokosea ni pale ambapo hatusemi ukweli,sioni sababu ya kumuogopa yule anayepotosha wananchi. Kama Waziri Naibu sema kwa herufi kubwa kwamba Askofu Gwajima ni mpotoshaji ktk swala la Corona...
Yessss, Halima anarudi CCM Gwajiboy anapigwa chini, Halima anapitishwa na CCM, Halima anarudi bungeni.
 
Wewe uishukuru Sana CHADEMA kwa kukufikisha hapo, kila mtu ana uhuru wa kujieleza
Waitara alikuwa CCM kabla ya Chadema na alikuwa na cheo tena alikuwa mwamba kweli kweli akiwa UVCCM enzi za Dk. Nchimbi. Chadema waliramba dume alipoahamia kwao na ndio maana walimpa vyeo vya juu juu! Hivyo, Chadema ndio walipoteza waliooshindwa kumtumia na kuamua kurudi nyumbani.
 
Gwajima unafiki na usaliti utamponza! Muda ndiye hakimu wa Yote!!

Alikua na hiyo nafasi huko nyuma na watu walimfuata Leo kapewa cheo kwa dhulma anafikiri anaweza kuwa Na jeuri na uhuru Kama ‘enzi zile’

Hicho kikundi chake cha legacy kutoka lake zone kitakwenda nae na maji.

Poor him!!
 
Wananchi Wana hoja ya msingi, nadhani wajibiwe kwa hoja wasibezwe. Waelezwe suala la Chanjo ulikuwa msimamo wa Serikali au mtu?
Then sasa hvi bado Ni msimamo wa mtu au Serikali?. Then waambiwe kwanini waamini msimamo wa sahvi na siyo ule wa awali. Waelezwe wasifokewe na kubezwa.

Membe on twitter
 
Stupid Waitara! Kwanza wewe ni msaliti mkubwa. Huna maana ni huo uharamia w Jiwe ana Samia kukuweka ofisi ya umma.

Rais ni mtu kama wewe, hana la zaidi ya kutumwa na wananchi kuwatumikia. Anachokiagiza lazima kiwe questioned kama kuna sababu ya ku question hayo maagizo.
 
Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara: Kumekuwa na mzaha mzaha, unatoa maelekezo hata mheshimiwa Rais juzi ametoa maagizo watu wanaibuka wanazungumza mambo yao ambayo kwakweli ni makosa makubwa sana....
Nchi hii ya kijinga Sana, nilitegemea saizi Gwajima atakuwa yupo somewhere anapewa torturing , haiwezekani Hakashifu maamuzi na msimamo wa Rais
 
Waitara alikuwa CCM kabla ya Chadema na alikuwa na cheo tena alikuwa mwamba kweli kweli akiwa UVCCM enzi za Dk. Nchimbi. Chadema waliramba dume alipoahamia kwao na ndio maana walimpa vyeo vya juu juu! Hivyo, Chadema ndio walipoteza waliooshindwa kumtumia na kuamua kurudi nyumbani.
Ni nani kizazi kilichopita hajawahi kuwa mwana ccm?
 
Sina kumbukumbu na uCCM wa Lissu. Ebu tudadafulie tuujue.
Zamani ulikuwa ukifikisha miaka 18 lazima uwe mwanachama Wa ccm,youth league.
Kwa hiyo kuna vitu lazima uitishwe kama kujiunga chuo uwe na Cheti cha ubatizo au kadi ya mwanacccm, kwa hiyo lazima lisu alishakuwa mwanacccm hapo kabla ya vyama Vingii kuwepo.

Wwngi tulivipotezea kwenye kuvi renew maaana haikuwa bure kupata kadi Mpya.
 
Back
Top Bottom