Waitara ampandia Rais Magufuli

Waitara ampandia Rais Magufuli

Wanajipima ubavu, wanadhani itawasaidia kuwashawishi wananchi wawaone wanaweza Waitara tunamwangalia tu huku UKONGA, 2020 bila kitu tunambwaga hainaga USHEMEJI hiyo.
Mnambwaga nyie akina nani. Kwani mlimchagua? Acha vitisho. 2020 ukonga tunasafisha ccm kuanzia s/mitaa, kata na ubunge.
 
Hakuna cha maana alichokisema, ni mwendelezo ule ule wa kutafuta umaarufu. Aliyoyasema yamesemwa sana na watafuta umaarufu kama yeye, wamemuwahi.

TataMadiba,
Unahitaji ushauri nasaha maana naona una upungufu wa kuelewa mambo.
Kwako wewe wale wote wanaomkosoa Rais Magufuli kwa Kukiuka na Kuvunja Katiba ni watu wanaotafuta umaarufu! Haya ni mawazo ya Kichizi,Kinafiki na Kipumbxxxxx!!
 
Wanajipima ubavu, wanadhani itawasaidia kuwashawishi wananchi wawaone wanaweza Waitara tunamwangalia tu huku UKONGA, 2020 bila kitu tunambwaga hainaga USHEMEJI hiyo.
Wewe siyo mpiga kura wake acha kubwabwaja. Hii ni tabia ya Lizaboni
 
Mnambwaga nyie akina nani. Kwani mlimchagua? Acha vitisho. 2020 ukonga tunasafisha ccm kuanzia s/mitaa, kata na ubunge.
Bora umemweleza huyu tatadiba, naona busara yake inapungua siku hadi siku
 
na kwa jinsi rais wako anavyowagwaya ukawa iko siku ataamrisha TV na Redio zote marufuku kuwaalika upinzani isipokuwa wanaccm tu.
Rais anawagwaya UKAWA, lakini kwa sababu ya rais huyo huyo UKAWA wameanza kuwagwaya Wananchi , 2020 Magufuli hapigi kampeni.
 
MWITA Waitara, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam amesema, marufuku ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara nchini inatokana na kukosekana kwa fikra pevu miongoni mwa viongozi, anaandika Regina Mkonde.

Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Uongozi Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dar es Salaam amesema hayo leo katika kipindi cha ‘Tuongee Asubuhi’ kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Star TV.

“Anachofanya Rais Magufuli ni kuzuia siasa za CHADEMA ili tusijiimarishe huku yeye akisuka mipango ya CCM kusikika peke yake pia anadhibiti vyombo vya habari vinavyoandika ukweli, hii ni siasa ya kitoto,” amesema na kuongeza;

“Maamuzi yaliyofanyika si ya haki, Magufuli amezuia mikutano ya CHADEMA anaruhusu ya CCM tu, mwanzo alikataza mikutano ya hadhara lakini alipoona chama chake kitahitaji kufanya mikutano akaruhusu wabunge kufanya kwenye maeneo yao, jambo hili si sawa.”

Waitara amesema kuwa inashangaza kuona hata tamko la kuwataka wabunge na madiwani peke yao kufanya siasa katika Kata na Majimbo yao likikiukwa kwa kuwaruhusu viongozi wakuu wa CCM kufanya mikutano lakini viongozi wa upinzani wakizuiliwa.

“Christopher Ole Sendeka ni msemaji wa CCM na siyo Mbunge, amefanya mkutano mkoani Arusha na polisi walimlinda wala hawakumzuia, lakini ukiacha hilo vyama visivyo na wabunge au madiwani vitajijenga vipi na kupata wabunge wapya bila mikutano?” Amehoji.

Katika hatua nyingine, Waitara amesisitiza adhima ya CHADEMA kufanya mikutano na maandamano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu ili kupinga viashiria vya udikteta ambavyo vimeanza kuonekana katika serikali ya awamu ya tano.

“Kufanya mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba na kisheria kwa vyama vyote vya siasa, na UKUTA upo pale pale kwasababu hii ni nchi ya vyama vingi, kama CHADEMA hatufanyi mikutano ya maendeleo watuache, waitishe ya kwao na watushitaki kwa wananchi,” amesema.
Aangalie isije ika 'MKOSIT'
 
Bora umemweleza huyu tatadiba, naona busara yake inapungua siku hadi siku
Hakuna ukweli wowote nilioambiwa hapo, ukweli tutaujua 2019 na 2020.Waitara akirudi mnikate kidole mimi mkurya mwenzake lakini dalili za kumng'oa zimeshaonekana.
 
Namshangaa huyu mbunge Waitara anang'ang'ania kutaka azungumze na watanzania waliopo Mbeya na kuacha watu wake wanataabika kwa kutokuwa na umeme. Mfano wakazi waliopo maeneo ya Bomba mbili hawana umeme,maji, barabara mbovu, hakuna zahanati na shule ipo moja tu haina hata madawati. Badala ya kutatua kero zilizomzunguka kwenye jimbo lake anataka kwenda mbeya na kwingineko. Namtahadharisha kuwa awe makini maana 2020 sio mbali na tumeshadhamiria kumbwaga hana maana huyu mbunge. Ameshauriwa na Raisi kuwa awe karibu na sisi wananchi tuliomchagua sasa hataki kufanya hivyo badala yake anakimbilia kwenye vyombo vya habari na kuzungumuza mambo amabyo sisi wananchi wa eneo hili tunayaona hayatufai.
 
makufuri na mfaninasha na mtu aliye ingia kwenye ulingo wa ngumi na baada kuona ameshindwa anaanza kuruka salakasi ili aendele kujitafutia mashabiki ingawaje ameshindwa.

ni sawa na makufuli inshu ya viwanda imemshinda ameaumua kuanza kuipindisha sheria ili aendelee kujitafutia washabiki.

na kama kweli yeye makufuli ni dikteta huo udikteta wake auweke kwenye viwanda tuone udikteta wake.
 
Back
Top Bottom