Waislamu Waazimia Kumuunga Mkono Lowassa!

Waislamu Waazimia Kumuunga Mkono Lowassa!

Wivu ni mbaya sana. sijawahi kuona mtu anayetesa watu kama Lowassa. Taifa hili sasa limekaa kimya na kuangalia mafuriko ya Rais 2015 itakavyokuwa. La pili, Tuhuma za Lowassa si Tuhuma bali ni chuki na Hila dhidi ya uwaziri mkuu na nafasi ya sasa anayoihitaji. Ni juzi Ikulu imewasafisha watu (mawaziri ) waliohusika na sakata la escrow. kwa nini ikulu haijawahi kumsafisha Lowassa au kumpeleka mahakamani au kuitwa katika kamati ya maadili ya umma na matokeo yake ni baadhi ya watu wasiokuwa na mvuto kwa watu kuendelea kwa hila kwa lowassa hafai kwa sababu mbalimbali zikiwepo oooh baba wa taifa alisema lowassa hawezi kuwa rais, oooh anatuhuma za ufisadi, oooh ni mgonjwa(utafikiri wao wazima) na mengine mengi. kama ni suala la Baba wa taifa, mbona Azimio la Arusha limevunjika na aliianzisha yeye kwa nia nzuri na kwa maslahi mapana ya nchi yetu? hao walioondoa azimio la Arusha hawakuwa mafisadi? Na mengine mengi. kiukweli ccm mwaka huu kazi mnayo mwaka huu na wote timu M, P, J, S, M, M, Nya, na wengine wengi kwisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

engijape tuachane na hayo mambo ya wivu (tena wa kike). Mimi naomba mnisaidie iwapo hii SAFARI YA MATUMAINI kwa kila Mtanzania ina tofauti na MAISHA BORA kwa kila Mtanzania. (Wakati mkinisaidia kupata ufafanuzi kumbuka kuzingatia kuwa architect ni huyo huyo).
 
Mwaka wa uchaguzi huu tutasikia na kuona mengi sana.
 
HIVI HAWAKUWEPO na WAKRISTO PALE KTK harambe mtoaMADA

Walikuwepo mpaka wasio na dini...kwani harambee ilikuwa maalumu kwa waislamu tu....inaelekea una elements za udini...
 
Last edited by a moderator:
Mbele ya Pesa kila goti litapigwa...... Muislamu kaisahau Memorandum Of Understanding MOU... Njaa mbaya.
Teh teh !! Umenikumbusha mbali mkuu,lkn angalia hali ya hewa isichafuke
 
Usitadhi Abdalla ana tisha zaidi ya Mesi,chezea kitu pesa Yuda uzalendo ulimshinda akamsaliti Bwana wake kwa sababu ya kitu pesaa.
 
najua limekugusa!!! tukutane nec mama!!!!!
haya ni mafuriko!!!

Hakuna mgombea ambae ana nia kweli ya kuchaguliwa kwenye ngazi yoyote ile atazibeza kura za Waislam. Kumbuka hilo.

Hata ex Padri Slaa akiteuliwa kuwa mgombea Urais leo hii utamuona atavyojipendekeza kwa Waislam na utanikumbuka kwa hili, kwani ni mbali?
 
WanaJF,

Pamoja na kwamba mzee Lowassa kwa sasa amesitisha harakati zake za utangazaji wa nia ya kuelekea magogoni kufuatia amri ya chama, ila kuna nguvu ya ziada kutoka kwa wapenzi wake inayoendelea kumshawishi kutangaza nia na kuendelea na safari yake ya matumaini.

Leo kwa mara ya kwanza nakiri kwenu wanaJF kuwa Lowassa hahusiki kwa namna yoyote kupanga ama kuratibu vikundi vya watu kufanya maigizo ya kumshawishi, bali ni umati wenyewe ndio wenye mapenzi kwa huyo mzee.

Baada ya makamu wa rais kumuomba Lowassa akamwakilishe katika harambee ya waislamu ya ujenzi wa msikiti, Mhe Lowassa alifika na zoezi lilianza mara moja la harambee. Zoezi lilikwenda kama ilivyopangwa isipokuwa lengo la kiwango walichokihitaji waislamu kilizidi takribani kwa mara mbili na kufikia takribani Milioni mia tatu.

Hali hiyo iliwafanya waislamu (kulikuwa na uwakilishi kutoka maeneo mbalimbali nchini), kwa msimamo wao mmoja kutoa tamko la kumuunga mkono Lowassa katika safari yake ya matumaini! Hali ambayo ilipokelewa kwa furaha na waumini wengi wa dini ya kiislamu waliohudhuria harambee hiyo.

View attachment 252017

Lowassa akiwasili kwenye eneo la tukio.

View attachment 252036

Hapa akiwa anasalimiana na mashekhe mbalimbali.

View attachment 252018

Lowassa akipatiwa shukrani baada ya kukamilisha zoezi la harambee.

View attachment 252019

Maelfu ya watu walijitokeza kwenye harambee hizo.

Note: Pesa hizo zitatumika kujengea msikiti ambao utaenda sambamba na uanzishwaji wa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu.

My take,

Kweli mafuriko hayawezi kuzuiliwa kwa kiganja.
Kwa hiyo walikuwa wanamsubiri akawachangie pesa kwanza ndiyo wamuunge mkono?.
 
Hakuna mgombea ambae ana nia kweli ya kuchaguliwa kwenye ngazi yoyote ile atazibeza kura za Waislam. Kumbuka hilo.

Hata ex Padri Slaa akiteuliwa kuwa mgombea Urais leo hii utamuona atavyojipendekeza kwa Waislam na utanikumbuka kwa hili, kwani ni mbali?

sio mbali tuwe patient tucheki picha hili!!!!!
 
Back
Top Bottom