Waislamu tukatae udini wa akina Ponda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu tukatae udini wa akina Ponda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Oct 17, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nchi yetu iko katika hatari kubwa ya kuingia katika machafuko ya kidini yanayotokana na kufumbiwa macho chokochoko za kidini ambazo zimeanza muda mrefu sasa. Uvumilivu miongoni mwa waumini wa dini kuu chini yaani uislamu na ukristo ambao umekuwepo nchini toka uhuru sasa unatoweka kwa kasi ya ajabu.

  Nimesoma kinachoitwa "waraka wa waislamu" nimeweka inverted commas kwa sababu sikubaliani kabisa na title hiyo. Kilichomo ndani ya waraka huo hakina sifa ya kuitwa waraka wa waislamu kwani ni dhihaka na tusi kubwa kwa waislamu wengi ambao ni wastaarabu, wastahimilivu na wasomi. waraka umejaa ujinga mtupu ukisherehesha na matukio ya kubuni ya uongo na ya kiwango cha chini sana ndiyo maana nasema haustahili kuitwa waraka wa waislamu, ungefaa kuitwa "waraka wa ponda kwa waislamu ambao ni wajinga"

  Waraka unajaribu kutuaminisha kuwa Mhe Hadji Mponda na Mhe. Mustapha Mkullo walipoteza nafasi zao za uwaziri kwa shinikizo la wakristo bila kujali tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao ikiwamo ubadhirifu na kushindwa kumudu majukumu yao. Tunafahamu Mhe Mponda alishindwa kushughulikia ipasavyo mgogoro wa madaktari na serikali, pia ili lazimu awajibike kwakuwa MSD iliyo chini ya wizara yake ililitia hasara taifa la zaidi ya shs 5bilioni kwa kusababisha dawa zenye thamani ya pesa hiyo kuharibika kwa kufikia mwisho wa muda wake wa matumizi(expiry) bila kuzisambaza mahospitalini ambako zilikuwa zikihitajika sana na wagonjwa wakifariki kwa kuzikosa dawa hizo. Pamoja na Mhe Mponda mwingine aliyewajibika katika hili ni Mhe Dr Lucy Nkya aliyekuwa naibu waziri, lakini waraka haumtaji kwa kuwa ni mkristo hivyo hoja ya udini inayojengwa itavurugika.

  Mhe Mkulo pamoja na kushindwa kabisa majukumu yake kama waziri wa fedha alikuwa na tuhuma za kuuza kinyemela kwa kampuni ya METL kiwanja mali ya PSRC. Pia Mkulo alishinikiza kuvunjwa kwa taasisi ya CONSOLIDATED HOLDING LIMITED na kuhamishiwa shughuli zake kwa msajili wa hazina. Hapa lengo lilikuwa ni kuwalinda wadaiwa sugu ambao bado hawajamaliza kulipa madeni yatokanayo na ununuzi wa mashirika ya umma. CHL ni mrithi wa iliyokuwa ikiitwa PSRC. Mhe Zitto Kabwe ndiye aliyeibua sakata hili lakini waraka haumtaji kwakuwa ni muislamu ili kujenga dhana kuwa Mkullo aling'olewa kwa shinikizo la wakristo.

  Waraka una maelezo marefu lakini yasiyoeleweka juu ya chadema kuwa chama cha kikristo ambacho waislamu tumetakiwa kujiepusha nacho bila kutueleza na kutuelekeza chama cha kukiunga mkono ambacho bila shaka ni cha kiislamu. Jambo lingine ni mali nyingi zinazomilikiwa na makanisa kuwa eti imewezeshwa na mfumo kristo uliopo nchini. Nasema huu ni ujinga na uongo wa mchana kweupe kwani taasisi za kikristo toka kabla ya uhuru pamoja na kuandaa waumini wao kiroho hazipata kuwa nyuma katika kushughulikia huduma za kijamii kwa waumini wao pamoja na wasiokuwa wakristo. Wakristo walimiliki shule na hospitali nyingi ambazo zimehudumia watanzania wote bila ubaguzi. Baba yabgu mzazi ambaye ni mwislamu alisoma katika shule za kikristo yaani st mary na st andrews. Shukrani za pekee kwa baba wa taifa(mkristo) ambaye alitaifisha shule za kanisa ili kuwezesha waislamu kusoma katika shule hizo, pamoja na hatua hiyo ya kizalendo kuna waislamu wenzetu ambao wanamdhihaki mzee huyo kwa udini, huku ni kukosa shukrani kwa kiwango cha juu sana.

  Najiuliza bila hatua hiyo ya Nyerere wazee wetu wa kiislamu wangesoma wapi ilhali Mazengo sec schoo, Mkwawa sec. school, Tosamaganga, Musoma alliance, Pugu, Minaki, Malangali, Rugambwa, Forodhani zilikuwa mali ya madhehebu ya kikristo. Narudia kuandika tena kuwa waraka huu ni janga na ni kielelezo kuwa waislamu bado tunasafari ndefu ya kuutokomeza ujinga kama wanaojiita viongozi wetu wa uislamu wanaweza kuandika waraka muflisi kama huu.
  NAWASILISHA
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Sheikh ponda yupo Osterbay anaisaidia polisi!
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa manake uislamu unataka kutumiwa vibaya na wahuni kama hawa akina Ponda.
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Serikali imemlea sana Ponda. Nakumbuka Tuntemeke Sanga alimdhalilisha Rais Nyerere (as he then was) kuwa hapashwi kuwa Rais kwa vile hakusoma kama yeye. Nyerere hakumkawiza, alimweka kizuizi cha Nyumbani akajuta, mpaka anakufa alikuwa amenyooka.
   
 5. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NYERERE ni Rais pekee duniani aliyenyang,anya shule na mahospitali ya waumini wa dini yake (wakristo) ili wafuasi wa dini isiyo ya kwake( waislamu) wasome na kutibiwa lakini anatukanwa zaidi na waislamu kuliko wakristo unafikiri utamfanyia nini Mwisilamu ili kukidhi haja yake labda ubadili dini na Tanzania yote kuwa ya waislamu.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mapogolo salute! nakubaliana nawe 100% waislamu waadilifu wakatae uhuni huu unaoletwa na akina ponda kwa mgongo wa dini. Watz wote ni ndugu na tumeishi kwa amani miaka yote hii tusiruhusu wageni (akina ponda) watuharibie nchi yetu
   
 7. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere ni Rais pekee hapa Tanzania aliyetafuta fedha na kusimamia ujenzi wa nyumba ya ibada isiyo ya dini yake msikiti wa butiama. Kwa maneno yake alikwenda kwa Gadaff ambaye ni mwislamu na kumwambia kwamba wananchi wake wa dini ya kiisilamu kijijini kwake butiama hawana mahali pa swala Gadaff akajenga msitiki wa kisasa kwa wailsmau.

  Hii rekodi bado haijavunjwa na Rais yeyote hapa nchini baada ya Nyerere.

  Je waislamu wanahaki ya kubeza matendo yote ya Nyerere
   
 8. M

  Mboko JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu nimefanya research miaka karibu 5 sasa hawa jamaa zetu waislam wamezoea kupokea tu lakini kuudisha kwao ni mwiko kwa ujumla hawaridhiki na hawana ahsante ni kwamba hawa jamaa hawaeleweki wamenishinda
   
 9. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tatizo sio kukataa udini wa ponda. Tuangalie anasema ponda sio ya kweli? Ikiwa sio ya kweli ndio tuyakatae. Vyenginevyo sisi waislam tutayaunga mkono
   
 10. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Leo na wewe umekuwa Muislam (rejea heading yako). Acha unafki huo .... ebu pitia baadhi ya comments zako hapo chini uone unavodhihirisha imani yako;

  mapogolo
  4th June 2012 13:37
  #6 [​IMG] [​IMG] Member Array


  Join Date : 8th May 2012
  Posts : 37
  Rep Power : 169
  Likes Received14
  Likes Given8


  [​IMG] re: Serikali, shughulikieni akina 'Sheikh Ponda' haraka sana

  Kweli mkuu hata mi nimewaona, ni pumba mwanzo mwisho. Ila namsifu sana mtangazaji wa channel ten jina simjui. Alijitahidi sana kuwabana kwa maswali mazito mazito wakawawanaishia kujikanyaga. Huyo aliyekuwa na ponda ndiyo mufilisi kabisa na kujitia kuongea maneno kadhaa ya kidhungu ambayo kumbe hajui ni lugha ya haohao asiowapenda.

  Jamaa wamechoka mpaka wanatia huruma eti kipengere cha kuulizwa dini kisipowekwa kwenye sensa waislamu wote wagomee sensa. Kama unaamini dini yako ndiyo kubwa zaidi nchini onyesha hilo kivitendo (hospitali, shule na vyuo)kama anavyoshauri kisimajongoo na si wingi wa wapiga ramli Mbagala na kwingineko ambao wanafahamika ni wa dini gani. Nyambafu!!!


  Mnafki mkubwa kujiita Muislam, Unafki kama wako na Walioanziasha udini kabla na just baada ya Uhuru (Serikali + Kanisa kwa makubaliano maalum). Waislam hatutakuwa lele mama Mpaka kuhakikisha haki inakuwa sawa kwa wote.
   
 11. K

  Ka2 Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umempeleka ww?
   
 12. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kadanganye ukoo wako eti wewe muislamu wakati andika yako tu unaonekana mgalatia
   
 13. m

  mada dingyyyzz Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wee kafiriiii sisi waislamu tuanojitambua tumekwisha amka ule uislamu ubwabwa sasa hamna tena hapa mpaka kieleweke

  na tunamuunga mkono kamanda wetu ponda issa ponda 100%.
   
 14. B

  Bichau Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania, ni busara kila mmoja aheshimu dini ya mwenzie ili tulinde Amani yetu, cha msingi tuna mungu mmoja na sote tulizaliwa na tutakufa kwa wakati stahili. Chondechonde wapendwa tudumishe Amani, vita mbaya msione katika TV tuu.,

  Eh mola tuepushe na hili balaa la kututenganisha kwa udini. Na hao wanaofanya ukorofi wa makusudi ni vyema wakachukuliwa hatua za kisheria. Lazima tuheshimiane.
   
 15. m

  mada dingyyyzz Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mpaka kielewekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee nyinyi makafiri tu
   
 16. m

  mada dingyyyzz Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa muislamu wa kweli kuwa oysterbay ni jambo la kawaida kwani hata mitume wote walipata tabu,yussuf alikaa jela kwa miaka isiyopungua kumi hivyo sheikh wetu ponda endeleza mapambanooooooooooooooooooooooooooooo
   
 17. m

  mada dingyyyzz Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  uyo jamaa kanyeshwa mafuta ya nguruwe anajifanya muislamu
   
 18. L

  Luca Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nawaomba ndugu zangu waislam tufikir kwa kutosha kabla maamuz
   
 19. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,926
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Sijawahi ona thread yoyote iliyoandikwa na muislam humu jamvini kutoa malalamiko au kutusi iman hii ya upande wa pili,,kwanini mnapenda sana kutufuata fuata??wapo wanaodiriki kuitukana had qur an yetu na kuendelea kuudhalilisha uislam wetu,,kwani vipi??kama watu tumepotea leave us alone,,kwanin muonekane kuguswa na kuumia sana kwa sisi kua waislam??kwani mkoloni alipoondoka na kuwaachia hii dini aliwalazimisha??tuacheni haya mambo,bila wazee wenu hapo zamani kuja kutawaliwa na kufanywa watumwa kisha wakaachiwa hii dini na mkoloni nyie leo mngekua wakristo??whats so special about christianity to ur origination??
  Kwanini mnapenda kutufata fata sana,nyinyi mna dini yenu na sisi tuna dini yetu why mnapenda sana kutufanyia choko choko??
  Makafiri tunaomba kila mtu achukue time zake,kila mtu achukue ustaarabu wake aamin kile anachokiamin,,
   
 20. s

  schwester Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza tujiulize hao waislam wanayoibua chuki ili nchi ikose AMANI, walitusaidia nini sisi waislamu wenzao? Ndiyo wanajinufaisha wao na familia zao na kuokota vimada Makafiri na kuwapeleka Nje. Kama kweli ni wazuri na wameyaona haya kwanza wangepeleka fedha kwenye jumuiya zetu ili shule nazo zijengwe kama wakristo wanavyofanya na hospital baada ya hapo tuone wanayosema. Wanatudanganya wazidi kutuvuruga kwa hili TUKIIUNGANA WAISLAM TUKAMUOMBA ALLAH UNAFIKI WAO UTAWAANGAMIZA WENYEWE.
   
Loading...