Katika yote nakubaliana na wewe ila chadema kuwa kina udini hapo nawaunga mkono hao kina ponda kwa 100% ila mengine wametia chumvi tu na wanatumia ujinga wa baadhi ya waislam wasiojitambua
Rafiki yangu hata hilo la kwamba CHADEMA kina udini ni uongo mtupu na ni propaganda tu za kisiasa! Udini umetumika na watawala kudanganya wapiga kura ili kupata kura zao kiurahisi.
Utakumbuka wakati CUF ilikuwa tishio kwa CCM mwaka 2005 wananchi waliambiwa ni chama cha kidin-kiislamu na kwamba kilikuwa na mpango wa kufanya nchi hii iwe ya kiislamu pindi watakapochukua madaraka. Hata walisingiziwa Kuingiza silaha toka uarabuni. Na kweli wakristo wengi waliachana na CUF.
Ni janja hii hii imetumika kuwaogopesha waislamu mwaka 2010 ili wasipigie kura CHADEMA na kwa bahati mbaya hii propaganda imeendelezwa hadi leo na kuwekwa vikolezo vya ukabila, udini na ukanda. Na kwa bahati mbaya zaidi kina Ponda wameweka kibwagizo na kuongezea kuwa adui wao ni wakristo-ujinga mkubwa!
Sasa jiulize CHADEMA au CUF ni vyama vya kidini kwa misingi ipi? Soma katiba zao, soma sera zao, angalia wanachama wao kama wanatoka mkoa mmoja au dini moja, hudhuria mikutano yao na hata angalia viongozi wao wakuu je ni wa dini moja? Tena utashangaa viongozi wakuu wa CHADEMA Sita, Kati yao 4 ni waislamu. Niliwahi kuweka orodha yao hapa jf wakati wa kuchangia hoja. Ila ngoja nikuwekee kwa urahisi wa kuliona hili. Ila nakushauri uwe unatafuta taarifa badala ya kusubiri kudanganywa na kina Ponda.
Viongozi wa Kitaifa wa CHADEMA
1. Mwenyekiti Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe- Kutoka Hai, Kilimanjaro
2. Makamu Mwenyekiti Bara, Mhe. Said Amour Arfi -Kutoka Mpanda, Rukwa
3. Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Mhe. Said Issa Mohammed-Kutoka Pemba
4. Katibu Mkuu, Mhe. Willibrod Peter Slaa-Kutoka Karatu, Arusha
5. Naibu Katibu Mkuu - Bara Mhe. Zitto Zuberi Kabwe-Kutoka Mwandiga, Kigoma Kaskazini
6. Naibu Katibu Mkuu - Zanzibar Mhe. Hamad Mussa Yussuf-Kutoka Kaskazini Pemba
Nadhani majina yanajieleza.
Unaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama chochote lakini usiache kujiunga na chama chochote kwa kudanganywa kwamba ni chama cha kidini. Kwanza kutokana na katiba ya nchi yetu chama chenye udini hakiwezi kusajiliwa na kikigundulika baada ya kusajiliwa kinaweza kufutwa kwa mujibu wa sheria.