Waislam tumefeli kwenye hili tu, tubadilike

Waislam tumefeli kwenye hili tu, tubadilike

EXPULSION

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2015
Posts
407
Reaction score
303
Napenda kuweka wazi kuwa mimi ni muislam, ninayefuata misingi yote ya dini. Nimesoma dini kwa kadri ya uwezo alionijalia manani na pia elimu dunia, namshukuru muumba kwa hili. Nawashauri waislam wenzangu tubadilike, tuitafute elimu dunia popote ilipo, mana kwenye dini tumefaulu, sasa tuitafute elimu dunia kwa udi na uvumba mana hapa ndipo tumefeli.

Napenda kutoa dukuduku langu, kwamba hatutokuwa na malalamiko tukishapata hii elimu kwa wingi mana tutakuwa tuna vyote vya kutufanya tuchambue mambo kwa uwanja mpana zaidi.

Najua tatizo la waislam wenzangu ni kwamba tunaona tunaonewa ila wakati mwingine sisi wenyewe ndio tunaosababisha. Namshukuru muumba nchi yetu ni ya amani na upendo pamoja na baadhi ya mambo kutuendea kombo, ila manani yupo pamoja nasi watanzania. Naomba na wasio waislam, wajitahidi kuwaelimisha waislam wenzangu tujenge taifa lililo bora na la kumpendeza muumba wetu.

Nawasilisha
 
Mtoa mada umevurugwa ww ndio muislam pekee unayelalamika wengine tuna ujuz wa kutosha wa kupambanua mambo tatizo lako unazungumzia mambo.ya mwaka 47 jipange....
 
Mabadiliko yawe kwa wote, wapo wakristo wanaoamini kuwa eti wao wamesoma zaidi kuliko waislam. Hiyo sio hoja, hoja ni hii wote kama watanzania tuongozwe na nia ya dhati ya kizalendo na kuitumikia nchi yetu kwa pamoja.
 
pakalolo
Mfumo Kristo ni huu:

  • Kufanya mambo kwa kumtegemea mungu,
  • Kutokuwa na mawazo mabaya dhidi ya watu wengine
  • Kutobweteka na kupiga majungu au kuwatuhumu watu wengine mambo ya kipuuzi
  • Kuhamasisha watu wengine wampende Mungu wa kweli ambaye wakimshika atawapa hekima na akili njema
  • Kuhakikisha kuwa watoto wanasoma vizuri elimu dunia ili wawe na akili njema
  • Kuheshimu dini za watu wengine
  • Kufanya kazi kwa bidii na kuondoa wazo lolote la kutegemea mtu mwingine ili kufanikiwa
  • Kuwaombea watu wasiomjua mungu ambao wamefanya dunia iwe sio sehemu salama
  • Kuwa wakimya na watulivu hata pale ambapo tungeweza kujibu na kuwaudhi wengine
  • Kukubali udhaifu wa watu wengine ambao wengi wao adui (shetani) na pepo wachafu wamejenga ngome kwenye mioyo yao
  • Kuwaombea wote wanaosema kuwa nchi hii ina mfumo wa Kikristo kwani hawajui wasemalo maana roho ya pepo wachafu ndiyo inayo wasukuma waseme hivyo
  • n.k
 
Last edited by a moderator:
pakalolo
Waislam wamesoma na wengi wanazo nafasi nzuri. Tatizo ni mfumo kristo.. Hapa mkuu sijakuelewa, sijui ulikuwa ulikuwa unataka kusema nini.
 
Last edited by a moderator:
mleta mada naweza kukubaliana nwe japo kwa point ndogo tu. Mtaa ninaoishi asilimia kubwa ni waislam na wakristo tuko baadhi tu. Cha ajabu wao kwa wao hapendani hata kidogo na ugomvi wao ni wa kipumbavu inafikia mahali nasikia wanatupiana majini.

Vile vile ninapoishi pembeni kuna madrasa yaani pale watoto wa umri wa miaka kuanzi 3 nakuendelea wanafundishwa hadi usiku mkubwa na siku zingine wanakwenda kwenye ziara halafu wakirudi wanalala madrasa bila ya hata kuwatenganisha maana kuna wasichana na wavulana kama 14 au 13 yrs, sasa huyu mtoto anapata muda gani wa kupumnzika na kufuatilia vipindi madarasani.

Watoto wanashinda madrasa na shule haendi. Mzazi wala hana habari. Inafikia mzazi mwingine anaona bora mtoto aende madrasa kuliko shuleni. Na wakienda shule, wengi wao hua wanakwenda kucheza na kusumbua walimu.

Mwalimu akimchapa, mzazi anakuja juu na kusema mwanangu ana mashetani mkimpiga yatapanda hivyo walimu wanawaacha kama walivyo na watoto mpaka wanamaliza shule hawajui chochote hivyo wanasubiri kuolewa au kubeba vimizigo umpe elfu mbili.

Ukimpeleka mtoto shule ya gharama, wanaona wewe una hela kumbe wewe unajenga maisha ya mtoto wako ya baadae. Naomba tusimseme vibaya mleta mada. Kweli wenzetu pelekeni watoto shule na muwafuatilie wawapo shuleni, sio kuwaacha tu.
 
ngusekel
Mikoa ambayo leo tunaisikia na matukio ya kishirikina, wengi wao huko ni Wakristo. Halafu unatakiwa ujue;chuki haiwezekani umchukie usiemjua. Maana wanaoishi eneo moja ndiyo wanaokosana, hii hata kwenu ipo.
 
Last edited by a moderator:
Gor
Sikatai. Waisam tumesoma sana kwa wakati huu, ila tusome kwa wingi zaidi kama wenzetu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia mia, mana hata mimi nimetokea huko, wakati nipo madrasa nilikuwa najitahidi na kufanya vizuri shuleni ila wenzangu wengi walikuwa hawahudhurii vizuri shuleni, nilikuwa sijui hapo badae ntaona impact yake, mana nilikuwa bado mdogo, sasa ndo nimeelewa tatizo limeanzia wapi.

Tujitahidi kukumbushana katika hili kwa kujenga taifa bora.
 
Back
Top Bottom