Waislam nijibuni hili

aisee.
 
Kipindi hicho unachozungunzia kilikuwa ni baada ya mtume kufariki. Kipindi cha uhai wa mtume kulikuwa na mikataba ya ujirani mwema kati ya waislam, mayahudi na makuraish. Baada ya kufa mtume, kulitokea uasi. Waasisi wakitaka kuiteka madina. Na ikatokea vita. Baada ya waasi kushinfwa vita wakapewa masharti hayo, musilimu au muishi chini ya dola ya kiislam kwa kulipia zakka ili mupate ulinzi dhidi ya maadui wengine.

Pitia hapa

 
Mkuu, shukrani sana kwa huu uzi, umeandika ukweli ulio wazi..

Matatizo mkubwa ya Waislam hasa hawa wa Tanzania ni ukosefu wa kujua DINI yao..

Waislam wanaamini kuwa kujenga Misikiti ni sadaka kubwa sana ambayo itakulinda siku ya Mwisho uko akhera..

Wasichokijua au wanalijua lakini kutokana a upeo mdogo wa elimu ya dini yao kuwa hata ukijenga SHULE , HOSPITALI , VIWANJA VYA KUCHEZEA WATOTO, NYUMBA ZA YATIMA, VYUO VIKUU nk, vita kulinda vile vile siku ya mwisho uko Akhera..

Uislam unaamini Ibada ni kufanya mambo mzuri kwako wewe au kwa Jamii...

mfano umeona kipande cha KIGAE kipo njiani, ukakiondoa KIGAE kile na kikiweka pembeni au kukitupa kwenye debe la taka ili watu wasidhurike iyo nayo Ibada, na unapata dhawabu kwa hilo..

Ukenda nchi za waislam wanaojua dini yao mambo hayako kama hapa kwetu, Misikiti ni sehemu ya kuabudu lakini kuna kuwa na Vyuo Vikuu, na harakati nyengine katika sehemu husika..
 
Jordan,UAE,Oman zinatosha..umeonyesha ujinga wako kwa kuitolea somalia mfano na yenyewe iko mashariki ya kati?Ila hizo nchi nilizozitaja mwanzo zimekuumiza roho pole sana bwana mdogo!!!
Kati ya nchi zote za mashariki ya kati zenye Amani ni nchi tatu?hapo ndipo utasemakuna Amani??Somalia nilisema kati ya nchi zenye vurugu!!Lakini kwa sababu akili yako imeshikwa utaendelea kubisha!!
 
Nafikiri umemsoma vibaya huyu jamaa, kaka kama wewe ni Muislam unatakiwa ujue kuwa Uislam sio kujenga Misikiti tu..

Uislam ni mfumo wa maisha, kama maisha yako na ya mtoto wako pamoja na familia yako hayako katika mazingira mzuri basi ujue hata huo Uislamu utauona shubiri

Waislam tubadilike Dunia inatiacha, badala ya kujenga sehemu za IBADA, tujitahidi pia na kujenga VYUO VIKUU vyetu, HOSPITALI zetu nk..

Sadaka sio kujenga Misikiti tu..
 
Wamiliki wa 'dini' wana akili sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya nchi zote za mashariki ya kati zenye Amani ni nchi tatu?hapo ndipo utasemakuna Amani??Somalia nilisema kati ya nchi zenye vurugu!!Lakini kwa sababu akili yako imeshikwa utaendelea kubisha!!
Unachekesha kweli!! maana hata ulichouliza hukijui ulitoa hoja uthibitishiwe kama kuna nchi mashariki ya kati zina amani zimepatikana unaruka usemi wako!!!huna hoja•
 
Mgalatia hawezi kuelewa!!!
 
Akhy, naomba unifafanulie kuhusu hiyo asili ya neno "Sheikh" kama ulivyosema. Hiyo kauli uliyosema umeitoa wapi??

Halafu hapo kwenye hadith, hiyo hadith unaweza kuonesha sanad yake na kuniambia kaipokea nani? Je ni hadith sahih, hasan, dhaif au mawdhuu'?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amri ya kwanza katika uislamu baada ya kuamini ni kusoma......hakuna anayepinga lakini huyu mtoa mada anaukashifu uislamu kwa maamuzi ya muislamu mmoja kuamua kujenga msikiti inakuwa ni tuhuma kwa waislamu wote hapo ndio inakuwa shida humu,huyu huyu aliyejenga msikiti akijenga shule au hospitali akaitoa kwa waislamu wAtakuja kulaumu tena mambo ya udini...hawa wagalatia sio wakuwaunga mkono hata siku moja.
 
Lakini wenzao wa Dubai, Saudia na Oman watu binafsi wanajenga mashule na mahospitali ya kisasa kila siku.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Akhy ukisoma historia ya Uislam (taarikh) wa Marne tatu bora za hatuoni neno Sheikh likitumika. Makhalifa wote waongofu hakuna aliyeitwa Sheikh.

Neno sheikh lilianza kutumia karne za hivi karibuni. Na ndio maana haya znz kiongozi wa serikali za mitaa wanaitwa Sheha, asili yake shekhe.

Unaweza kupitia hapa kwa ufafanuzi zaidi


Kuhusu sanadi ya hadhithi ya mtume; hadithi hiyo haina hadhi ya Sahihi, lkn bado inatazamwa kuwa Ni hadithi. Hata hivyo upon ushahidi mwengine juu ya kutafuta elimu; taarikh inasema moja ktk vita vilivyopiganwa wakati wa mtume na waislam wakashinda, mateka wa vita vile mtume (saw) aliamrisha wasiuwawe kama baadhi ya maswahaba walivyotaka. Bali mtume (SWA) aliamrisha wale mateka wa vita kuwa wangeweza kuachiwa huru kama wana elimu au ujuzi Fulani wangewafundisha Waislamu ujuzi waliona au kuwafundisha kujua kusoma na kuandika ndipo watawaachia. Na wasio na ujuzi walipe kikomboleo (fidia).
 
Kaka inabidi tumshukuru mtoa mada, bila shaka yeye sio Muislam, kwahiyo hivyo ndivyo anavyowaona Waislam, sioni kama kawakashifu au kuwa sema vibaya Waislam..

Mkuu, hapa kwetu Tanzania kuna tafauti kubwa ya yale yanayofanywa na Wakristo na wnayofanywa na Waislam katika jamaii..

Angalii hapo unapoishi Hospitali kubwa ni ya nani, Vyuo Vikuu ni vya akina nani, Waislam hatujui dini yetu ukweli ndio huo, inatakiwa tujitizame tumekosa wapi..

Ukisoma historia ya Uislam na mambo waliyofanya katika Dunia na vipi wamebadilisha Jamii tafauti duniani,..utaona UMUHIMU wa dini ya kiislam

Humu humu katika JF, kuna mada inayoeleza Kuwa IKULU ya Daresalam pamoja na hospital ya Ocean Road ilikuwa Madrasa kwa Waislam wa wakati huo, nyumba hiyo ilikuwa inaitwa "Daru Salam" yenye maana "nyumba ya salama"..

Daru Salam ilikuwa kama unavyoiona sasa ilikuwa imezungukwa na nyuma za wageni, sehemu ya kusali(misikiti), sehemu ya kusoma madrasa nk
.
Waliojenga hiyo sehemu walikuwa wanajua nini maana ya SADAKA, walikuwa wanajua Sadaka ya kukusaidia siku ya mwisho sio kujenga misikiti tu, bahati mbaya au nzuri Waliojenga walikuwa sio WAAFRIKA walikuwa WARABU, hapo ndio utajiuliza sisi Waafrika tunakosea wapi?? Au Uislam wetu tafauti na watu wengine??

Lazima tujirekebishe au Dunia itatuacha, Akhera tutajibu maswali mengi kwa Mungu wetu.. Tafakari
 
Shukran sana Akhy. Ila hili la matumizi ya neno "Shaikh" nitalifuatilia zaidi nijue kwa hoja na dalili za kielimu. Hayo maelezo ya kwenye hiyo website bado hayajaniridhisha vizuri naona tu kwa kiasi kikubwa yametarjumiwa kutoka Wikipedia.

Vile vile mara nyingi watu wanapoinukuu hiyo "hadith" ya kutafuta elimu mpaka China wanainukuu wengi wao bila ya kujua ni mawdhuu. Na cha kusikitisha imekuwa maarufu mpaka watu wengine wengi huitumia sana kama hoja na hata kuichukulia kama hadith sahih.

Pia tunapotaka kuonesha umuhimu wa elimu katika Uislam ni bora zaidi tutumie hadith sahih na hasan kuliko kuzitanguliza hadith dhaif wakati sahih na hasan zipo na zinatosha kuonesha umuhimu wa elimu katika Uislam.

Ila shukran sana Akhy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Shukran Akhy. Inshallah jikinaishe kwa kufatilia taarikh ya neno Sheikh. Na ikiwezekana utuletee mrejesho inshallah.
 
6. Hizo Zahanati ziwe nyingi kiasi hicho zipate kuwatibu maradhi ya zinaa na blood.poisoning related to alcoholism?
Hapa napo weye umeharibu points zako. Mbona humo humo misikitini wanaingia waliotoka kufanya uchafu nao wanajifariji kuwa wesha koga na sasa wana tawadha tu waingie kuswali?? Hatuwaziki kwa vifo vya magonjwa hayo hayo ya zinaa??
Point ya mleta hoja ni kuwa; Je, ni lazima tujenge msikiti?? Kwa nini nisinunue vitabu vya dini nikavimwaga penye ule msikiti?? Weka Kuruani za kumwaga hapo watu waji sevie wenyewe ili kila nyumba ipate kitabu hicho kitakatifu. Mwaga Juzuu za kutosha na vitabu vingi vya dini ambavyo watu wengi hawana uwezo wa kuvinunua. Vigawe bure ili watu waisome dini yetu waielewe. Fadhili mihadhara ielezee dini yetu, Misikiti mingi mitaani sio kuwafanya watu kusilimu.
 
Mtoa mada siyo muislamu,kwa hiyo hakuna jema hata moja anautakia uislamu,Labda ungesema wewe tungekuunga mkono na so kinyume chake.....kwenu katika maisha yako yote hakuna waislamu waafrika waliojenga shule au vyuo vya dini si dhani kama huko sahihi kwa hili.
 
Nyie mnashida kumuunga mkono mtoa mada,hakuna msikiti unaokosa madrasa kwa ajili ya kupata elimu lakini cha ajabu wewe unayetetea huoni umuhimu Wa elimu ya dini pia vitabu vipi vinavyotolewa Bure kabisa na waislam mbalimbali na hata wako watu wanaojitoleya kusafiri kwenda kufundisha dini na wala hawaonekani kwenye TV lakini kazi ya dini wanaifanya.
 
Waonyeshe Hospital moja tu ya Rufaa.
 
Kuna tafauti kubwa sana kati ya Waislam na Wakristo katika hili, hata kama kuna waislam wamejenga Shule lakini kidogo sana..

Kwa vile mtoa mada sio Mwislam ndio inakuwa vizuri kumsikiliza mawazo yake kuhusu Uislam na usaidizi wa Jamii kitu ambacho dini yetu imesisitza

Kusaidia WAJANE , MAYATIMA na MASKINI ni jambo lililosisitizwa sana katika dini ya Kiislam

Quran zimejaa aya zinazosisitiza kusaidia Jamii hasa ya makundi hayo,..

Swali langu utawasaidiaje hao Maskini, Mayatima na Wajane kwa kujenga Misikiti, Misikiti ni sehemu ya Ibada sio chengine..

Tuamkeni Waislam, tujaribu kuisoma dini yetu na kuifahamu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…