Waishi pamoja kwa miaka 62 wafariki pamoja

Waishi pamoja kwa miaka 62 wafariki pamoja

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
ImageUploadedByJamiiForums1407408770.712887.jpg
Watu walioishi katika ndoa kwa miaka 62 wamekufa pamoja nchini Marekani.

Don na Maxine Simpson, kutoka Bakersfield, California walipishana kwa saa chache tu kufa, katika vitanda vilivyowekwa karibu, huku wakishikana mikono katika saa zao za mwisho duniani.

Melissa Sloan, ambaye ni mjukuu, amesema bibi yake alitangulia kufa, na mwili wake ulipoondolewa chumbani, babu yake naye akafuata.

"Kitu pekee alichokitaka Don ni kuwa na mke wake mpenzi. Alimpenda sana bibi yangu, mpaka mwisho"

Don alikuwa na umri wa miaka 90, huku Maxine akiwa na miaka 87. Walikutana mwaka 1952 na kuoana mwaka huohuo.

Wawili hao waliwahi kuishi nchini Ujerumani wakati Don akifanya kazi katika jeshi la Marekani kama mhandisi, na walipokuwa huko, wali-asili watoto mapacha wa kiume kutoka katika nyumba moja ya kulelea watoto yatima.

Waliporejea Marekani, Maxine alifanya kazi ya uuguzi huku Don akifungua kampuni yake ya uhandisi.

Wameacha mtoto mmoja wa kiume na wajukuu watano.

SOURCE: BBC
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1407408822.140922.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1407408822.140922.jpg
    31.5 KB · Views: 109
hizi ndo ndoa sasa acha hizi za kileo mkikaa wote miaka 10 mnashukuru Mungu
 
Kimya kimya you wonder..... what's their secret?
 
Hii ndo ukisikia mwanamke ameumbwa kwa ubavu wa mwanaume ndo huku. Huyo bibi na huyo babu walipendana sana.
 
Back
Top Bottom