Waifu kanisamehe kikweli kweli au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waifu kanisamehe kikweli kweli au?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ndibalema, Oct 12, 2010.

 1. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Msaada wenu wa mawazo please.
  Juzi Nimerudi kutoka safari ya kikazi na kwa bahati mbaya wife ameibamba sim card yangu ya siri(ambayo yeye alikuwa haijui)
  Kwenye hiyo laini kuna sms za hatari amezikuta ambazo mtu mzima nimeshindwa kabisa kujitetea kwani mambo ni hadharani.
  Ikabidi nimwombe radhi wife na nikamwambia ni shetani tu.
  Cha ajabu wife wangu ambaye ni mtata sana akanisamehe kirahisi sana bila kuleta songombingo.
  Wakati sio kawaida yake kwani siku za nyuma kama akitilia shaka jambo hata kama si la kweli basi moto wake si wa kitoto.
  Jamani hivi wife kanisamehe kikweli kweli au anapanga 'revenge' ambayo nitakiona cha moto?
  Au na yeye yapo mabaya yake hivyo kaona ngoma ndroo haina haja ya kulianzisha?
  Mwenzenu nina hofu kweli.
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  USIJALI WALA USIOGOPE AMEKUSAMEHE kama unavyosema "Makalio ya sufuria hayaogopi moto"
   
 3. RR

  RR JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,718
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Anavizia akukate hizo nanhii.....kwa hiyo usilale hata chembe...
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu usibabike na hiyo signature.
  wanawake ni watu wa visasi sana ni lazma niwe na hofu.
   
 5. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwa vile wewe ndiye unayemjua vizuri na uko karibu naye,wewe ndio usome alama za nyakati kwa makini halafu utajua kama kasamehe au la.
  nakuomba uache hako katabia kenye kupelekea visms vya hatari.
  NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
   
 6. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  U r wrong kaka yangu,hakuna watu wepesi wa kusamehe kama wanawake.
  tunasamehe ila hatusahau kirahisi.
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  kama na yeye ana mabaya yake inakuuma? mbona wewe una yako na umemuumiza vya kutosha tu sema ana act haja mind...kuna mawili kakuweka kiporo kwanza atulie ajue afanyaje au ndio yupo kwenye mchakato wa revenge, maisha ni mafupi sana nyie waume zetu bado mnataka kuyafupisha zaidi.... ,huwaga cna huruma kwa watu kama nyie....AMESAMEHE KIRAHISI HIVYO...UNACHEZA WEWE!
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hebu anza kuchunga mnara wako wa simu asije akaamka usiku akaung'oa si unajua wanawake huwa wanaangalia wapi pa kuumiza itabidi usiku ulale umevaa PROTECTIVE GEAR
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  So kwenye red hapo unamaanisha kazi za nje niendelee kama kawaida ila niwe makini kwenye sms tu? Asante sana.
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nimekumiss kweli :hug::hug:umewekwa kinyumba na nani?
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Dearest upo wangu
   
 12. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hivi hiyo ndio tutaweza sema kinyongo? bac mie kiboko wa hiyo...jamani tuseme ukweli hakuna mwanamke wa kusahau kitu kama hiki mapema ni ngumu sana, wanaume kila cku nawambia humu nyie ndio chanzo cha matatizo ndani mwenu, halafu unafikiria kwamba na yeye labda ana mabaya yake kaona ngoma droo haina haja ya kulianzisha...mschew! sasa hapa tegemea vituko vianze.....yaani mnaharibugi sana, hapa umeshampanua akili ya ziada amabyo hakuwa nayo mwanzoni.
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kila kukicha vituko vya wanaume haviishi ..
  Sina hakika kama mkeo amekusamehe au raha ..inawezekana kampokea roho mtakatifu. au ulimkuta katoka mood nzuri
  Muulize tena kwa upole kama ni kweli amekusamehe toka moyoni ,uombe msamaha na usirudie tena hayo makosa .
  Mbona hamridhiki ?
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Lets assume umempata mwanaume mwingine bado utaendelea kukumbuka yale mabaya aliyokutendea yule mwingine uliyeachana nae na kuendelea kumuwekea kinyngo?
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Amekusamehe - Wewe endelea tu na akina "Anjelina" as usual:

  Usijaribu hata kidogo kubadilisha "life-style" : Tafuta sim card nyingine ya "siri" uedelee na mawasiliano ya "siri"

  Concept ya Mke-Mmoja Mme-Mmoja imepitwa na wakati : Watu wana-pretend tu!
   
 16. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,052
  Trophy Points: 280
  Ukiona amekuwa mpole ghafla ujue amekuonea huruma, yeye anafanya mabaya zaidi yako
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hauwezi kupingana na NATURE by the way mke mtarajiwa anaendeleaje unamkuza vizuri
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  nipo dearest....nimekacrika kama nini, yaani Ndibalema amenikacrisha sana,hapo ana cm card ya magendo akija home cm yake ipo hapo ni ya kifamilia zaidi, mwanamke unajidai ooohh mume wangu, oohh mume wangu jamani hatoki nje ...oohh mume wangu jamani cjawahi kuona vituko kwenye cm yake...nachukiaga sana wadada wanaojifanyaga mume wangu mume wangu kumbe ndio kama hawa, wameshamaliza mambo yao huko wakija nyumbani wanakuchora tu.....yaani cjuagi kwanini niliolewa.....unamuamini mtoto wa mwanamke mwenzio kuliko unavyojiamini....mschew!...WADADA WA HUMU NDANI WANAUME WOTE MAMA YAO MMOJA....HAKUNA HAKUNA MWENYE MAMA TOFAUTI...TUNAYAONA KILA KUKICHA...UPATE WA KUKUPENDA/KUKUPA HESHIMA/KUJALI
   
 19. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hio sio kinyongo,si ushashuhudia mara nyingi kina baba wanatembea/zaa na housegirls,wanacheat na vituko vingi vya usaliti lkn wanawake zao wanawasamehe na maisha yanasonga na wanaendelea kuwapenda lkn kusahau lile tukio sio rahisi .kinyongo ni pale unaposhindwa kumsamehe mtu hata upite muda gani unamchukia tu.
  anyway huo ni mtizamo wangu.
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ngoja ninukuu hii kwa niaba ya katibu halafu nitaipeleka kwenye kikao chetu cha ISC ijadiliwe kwa mapana zaidi
   
Loading...