Wahuni siyo watu wazuri

Daah ilikuwa hatari sana
 
Mi nikiwa na mubebe aisee tutauana.

Nilikua namrudisha binti kwao, wote tunaishi mtaa huo huo ila yeye upande mwingine.

Tumefika njia fulani ambapo kwao tunapaona na ina giza la kutosha tu nasikia sauti "We malaya" mi na binti tukasimama. Ile ile sauti ikasema "Kum2m2ko sogea huku"

Sasa mi nawaza huyu mhuni gani hanijui mimi mtaa huu? Wahuni wakubwa nilikua nao kundi la Majani Unit, wahuni wa Kisiwani na maeneo yanayotuzunguka hua wananiletea simu za wizi kutoa lock, wahuni wapya wakati wanakua nawaona, wahuni wengine nipo nao gym. Hawa wahuni gani?

Mara wakajitokeza washkaj watano. Nawaona tu pale street mmoja akasema "We malaya unaringa halafu mbaya kishenzi" nikapeleka kitasa. Akasogea wa pili kitasa, nikavamiwa nikawekwa chini ebwana nilikula mabomba hapo binti kaenda kuwaita kaka zake.

Kaka zake kufika hawajauliza wakaingilia show ndiyo nikaponea hapo.
 
Kuna watu wanapiga vibaya aiseee
 
hahahahahahahaha. hii inafaa utoe movie kabisa
 
Shida yako mleta mada unataka kuishi maisha ya kitamthilia.

Punguza kutazama hizo mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…