Wahuni sio watu wazuri

Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
2,049
2,249
Ooozaah niaje wajomba humu fyade!? Najua aikatox ainaga wengeree bablai sidai hopeful mko yechu.

Nisilete lomoni au perepete shazi acha niende moko moko kwenye topic..Jana night kunae mamiloo angu alihudhuria fas duas ya maskani,baada ya kumhondomola mishale kaa ya saa4 ivi za PM,ikabidi nim'escort coz uku Wang'ata lami wapo kila chochoro wasije wakampukutisha manzi angu asee.!!

ile tumedana wanchi wanchi chochoro fas ya road,mala nywele zangu zikaanza kusisimka dingii,,ohooo nikang'amua pande izi kunae waenduru wanaopolaga visivyo vya kwao.

Kweli chaliangu ile tumepiga hatua chache tu mala ghafla tunapigwa torch usoni alaf ikafata sauti ya kibabe"Oraaa apo apo mlipo stop nyie ndezi"..Daah manzi aliijua ile sauti ya yule mjuba akanambia"Mungu wangu hao ni kina Lil Wayne wa Matejoo!!tumeisha yesu wangu",,nikamwambia "tulia usihanye mamaa uko na Mimi"

Nikageuka nyuma yule chalii akasema"Oya Dullah wawahi chap wanataka kukimbia hao"wakati Huo wajuba wanakuja tuliposimama..ile wamefika wakatuweka kati kwanza alaf wana mapanga,nondo,beto,mikasi hadi vipande vya mbao.

Muda Huo manzi analia kinyama anawaambia "Lil Wayne kama hela nawapa ila mtuache nawaomba" ikabidi niongee kiume sasa"Wee Amina skiliza..uwape moneygram wanakudai hawa machalii?"

Chalii mmoja eti akasema"We msomali naona hutumanyi yechu sisi,,Tutakupururua hutoamini"Nikamjibu yule mduanzi"Aah wapi!?we si una panga?usiongee sana Fanya unachoweza na hilo panga lako nikuoneshe man,unanitishia mapanga Mimi chaliangu??me nilipokulia Mogadishu nimekua naona mitutu sio izi silaha zenu za kimamiloox,mnajiona wahuni sio?Sisi uhuni tunaujua ila hatuufanyi,mnajiona wajafanja sio..Mimi ni kwere ile kinyama kihuni kifaranyaki yaani usipime usibonyeze ariff,hii dishi yangu ni chenga et!"baada ya kuongea ivo wale wahuni uchwara wako kimya kaa hawapo yaani..

Baada ya kuwaona wameshadevela nikaendelea kushindilia msumari mbele ya manzi"Sisi kuchaniza hii road unafikiri hatumanyi kuwa kuna wahuni?nyie hata hamjiulizi kwanini tumepita??au tofauti nasisi kuna maraia wengine wamepita pande hizi??"wako kimya laana.

Nikamshika mkono manzi nikamwambia"Amina ebu twenzao",,Daaah sikuamini tumetoka salama asee,ikabidi nimchukulie Bodaboda manzi akachimba alaf Mimi nkatoka kibati road ingine Babaako.

@NgarenaroBoy.
 
Huyooo
tapatalk_1493627895302.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom