Kidogo nife ningekaa kiree kisa demu.

Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
2,049
2,249
Ooraah ni gani man chalii zangu humu fyade?..Natumai mko OG wazeya...Sina perepete shazi so acha niende direct kwenye mada...Apa fas ya kitaa kunae mamsi mmoja ananileteaga shobo za ki'waki ni kisoro yaani..anapendaga kuwaambia maraia eti waga natokaga nae sijui mala nilimpa mimba akaichoropoa tu..!!But to be honest sijawahi mdinya uyu manzi wala sina mahusiano nae zaidi ya kumgei hi then napita ivi na 70 zangu..!!Sasa kumbe akiwa anabofonga izo mastori Braza zake waga zinawauma kinyama yaani wanajaa sumu...Asa jana night mida ya saa1:30 nko ki'road road nasololoa moko moko nikazama chochoro moko hivi waga kuna kama kimgahawa flani hivi wanauzaga uji wa ulezi..ile nakatisha pande zile niaje kuna sauti ya kike ikaskika"Wee macho msomali njoo"..!!Khaa nikageuka namdekerea ni yule mamiloo mwenye shobo elfu18,ikabidi nijongee ile natimba ananiambia"Kaa nikununulie uji bas"nikaona aina kwerekweche nikakaa,but kama sekunde20 ivi wakaja wamama wakanisanua eti kuna wajuba wananisakanya kibingwa yaani machochoro zote...Ohoo nikamanya ni wale wahuni mabraza zake na uyu manta..nikamwambia yule demu"Kaa kwa kutulia nakuja one time",dem akasema"Unaenda wapi tena Chaliloo asee?"nikamwambia nakuja kwani huoni uji wangu nimeuacha apo fas nakuja kuumalizia asee.!!nikaenda kuchukua mkasi na bisibisi alaf nikarudi sasa pale mgahawani,ghafla Waenduru hawapa doooh!!"Uyu kuzi yupo apa man"aliskika mmoja wao..Yule kiongozi wao akaja chap akanishika koti akaninyanyua pale nilipokua nime'chill akanivuta pembeni penye uwazi uku mkononi alikua na Beto,nondo na msumeno,Alaf kawaka ni kinoma yaani,wale machalii zake wengine wanayoga kinyama"Oraa Mapansu mlete uku ndichi tumchune ngozi uyo ndezi"kwanza nikamsukuma akateleza a'drop chini but akakaza ila akaachia koti langu then nikakaa yechu ili niwaamshie popo hadi wadevere kidawgie..Mkasi wangu nikauweka vizuri coz nilikua nimeushika mkononi alaf nikaufunika na koti langu lenye mikono mirefu..Yule chalii akarusha ngumi me nilichofanya ni kutoa mkasi wangu chap kidogo akakutana nao kwa fas duas nikambana alaf nikauminya mkasi ukamchana..wahuni wake wakaja kunishambulia nikanyanyua meza nikawatwishwa waka'go danta kwanza,,Dem akaanza kunisihi"Usipigane watakuumiza Macho achaa"Baadhi ya wazee walokua wanakunywa kahawa pale eneoni wakajongea karibu,wakatuachanisha..Pia Wamama wakajaa pale ikawa mtu v*zi..wale madingilii/wazee walifoka sana wakati huo wale mak*ma wamesogea pembeni namimi nko uku na wamama na yule manzi"Watoto wa Ngarenaro mna laana gani wapumbavu nyinyi??hamna wazazi eti?Yaani juzi tu katobolewa mtu na spoku apa kwa mzee Olesendeka sababu ya haya haya maugomvi yasiyo na maana"waliskika wazee wale..kina mama nao wakasikika"Njooni sasa mnajifanya mnajua sana ugomvi simbilisi nyie,Uyu kijana msomali ata hanaga shida ni mstaarabu lakini mnamletea fujo,au kwa vile mnamuona ni mwembamba?!!"..Wale machalii wakaondoka uku. wakikoroma"Tutamshika tu uyu fala labda alale hapohapo,lazima tumtoe pattern asituletee umbax sisi",,Bas walipoondoka namimi nikaamsha though nilikua naogopa kinyama isije ikawa wamechill kitengo wananisubili...nashukuru nilifika salama Mageiyo/ghetto..






@NgarenaroBoy
 
BASI NA TUOMBE....
Tunakushukuru Mungu wetu kwa upendo wako kwetu,tangu tulipoamka hata sasa u pamoja nasi,
Umetulinda tulipotoka hata kurudi kwetu.
Tunakushukuru Mungu wetu na tunakurudishia heshima na utukufu.
Tunaomba toba kwa mambo yote tuliyotenda kinyume na mapenzi yako,tunaomba ututakase kwa Damu ya Yesu Kristo.
Ni usiku mwingine tena Baba tunaomba ulinzi wako,sawa na zaburi 127:1.kwani
Ulinzi wetu si chochote pasipo Wewe Mungu wetu.
Tuepushe na mipango yote ya adui yetu na wafuasi wake wote,
Tunanyamazisha kimya kila roho ya malipizi na watesi wetu, kwa jina la Yesu krito......
AMEN....


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom