Wahitimu wa ualimu, chukua projects hapa zikusaidie kuombea kazi

Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
3,009
7,309
Habarini wakuu.

Kama tunavyojua ualimu ni kada yenye ushindani sana katika upatikanaji wa ajira zake, leo naomba niwape projects (miradi) zenye kuvutia waajiri wakupe nafasi,

i) Remidial classes:
Hapa utaelezea kuwa utaanzisha program maalum ya kufanya kuanzia form 1 hadi form 4 wawe wanabaki jioni hadi saa 11 wewe ukiwa msimamizi mkuu, unasema utaandaa mitihani ya kusolve hiyo jioni au topic maalum kwa kila darasa wajadiliane na ijumaa unawapa mtihani wa kile walichodiscuss na kile ulichofundisha kutokea jumatatu hadi alhamisi.

ii) storm months
Huu ni mradi/project ambayo itahusu kuchagua miezi 2 Simultaneously yani kwa kila miezi 2 kutakuwa na mwezi mmoja special kwaajili ya kufanya mitihani na mwezi mmoja wa kufanya necta solving yani hakuna kusoma ni only solving, mfano mwezi march and april na mwezi june and july kunakuwa na hiyo program

iii) Student Development file
Hapa unasema kuwa utaongea na uongozi wa shule kuwe na file maalumu lenye kurecord maendeleo ya mwanafunzi toka aingiapo shuleni na kila hatua yake ya maendeleo hii itasaidia sana kujua ni waoi pakumsaidia mwanafunzi au kugundua mapema kipindi mwanafunzi anapoanza kushuka au kutoka nje ya mstari.

iv) shini parents
Unasema kuwa huu mradi utahusu kuwaalika wazazi shuleni kila baada ya miezi 4 au 6 au kila mwisho wa mwaka ambapo walimu wataongea na wazazi namna bora ya ujifunzaji, wazazi wataona jinsi watoto wanavyojifunza shuleni na kupata nafasi kuuliza maswali mbalimbali kwawalimu juu ya watoto wao.

v) Hot saturday unasema kuwa ukipewa nafasi ya kufanya kazi katika taasisi hiyo basi utaanzisha mradi wa Hot saturday kwenye masomo (3 au 4) unayoyaweza mfano (geography,biology,english) ambapo alhamisi watoto watakuwa wanatoa shilingi 200, wewe mwalimu utakuwa unachapa mitihani (kama una pc inakuwa rahisi) unafanya printing, jumamos saa 2 watoto wanafamya mitihani wakimaliza unawafanyia masahihisho, jumatatu unawagawia mitihani kwa viboko, (unaweza pia kusema hiyo hot saturday itahusu somo lako tu ila ukisema na masomo mengine at keast 3 itafanya uonekane wa mujimu zaidi.

Kuna vitu vingi sana vya kufanya ila onesha attitude ya upambanaji onesha kuwa utakuwa mwalimu mkali sana anaependwa na wanafunzi, sio kuwa mkali tu bila sababu kukiwa na muda wa utani fanya utani,toa ushauri, kiufupi waambie waajiri wako kwenye interview kuwa nataka niwajenge wanafunzi wangu katika picha ambayo mimi nilishindwa itimiza........

Mungu awaongoze katika kila hatua.
 
Saloot Boss
Saloot Boss
Shukrani mkuu hapo kwenye page ya pili ya cv juu unaandika kichwa PROJECTS alafu chini unaandika if given a chance to work with your institution i will implement the following projects the unashuka hizo.
 
Mbona kwenye hiyo miradi hakuna kipya hapo. Hivyo vyote vilivyotajwa hapo vilikuwa vikifanyika tangu miaka ya 90's huko nilivyokuwa mwanafunzi wa primary na hadi leo bado vinaendelea kwenye baadhi ya mashule.

Baadhi ya mashule wameachana na hayo mambo kutokana na wazazi kuchoshwa na michango ya mara kwa mara na usumbufu wa vikao vya mara kwa mara.
 
Mbona kwenye hiyo miradi hakuna kipya hapo.
Hivyo vyote vilivyotajwa hapo vilikuwa vikifanyika tangu miaka ya 90's huko nilivyokuwa mwanafunzi wa primary na hadi leo bado vinaendelea kwenye baadhi ya mashule.
Baadhi ya mashule wameachana na hayo mambo kutokana na wazazi kuchoshwa na michango ya mara kwa mara na usumbufu wa vikao vya mara kwa mara.
Sawa mkuu.
 
Back
Top Bottom