KERO Wahitimu wa Kozi ya Agricultural Investment and Banking wanashindwa kuomba kazi kupitia Ajira Portal

KERO Wahitimu wa Kozi ya Agricultural Investment and Banking wanashindwa kuomba kazi kupitia Ajira Portal

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nilihitimu degree kwenye Chuo cha SUA, Kozi ya Agricultural Investment and Banking, kozi mpya ilianzishwa Mwaka 2020, Mwaka 2023 ilitoa Wahitimu kwa mara ya kwanza.

Mimi nilihitimu Mwaka 2024, nashukuru Mungu Alhamdullilah nina kazi, nimeajiriwa DRC lakini sasa Vijana waliohitimu wanashindwa kuomba kazi za Ajira Portal sababu wamewekwa kwenye catégories moja ambayo haiwaruhusu kuomba kazi za benki kama hizi za BoT licha ya kukidhi vigezo vyote.

Sijui hawa watu wanasaidiwaje?

Wamewekwa kwenye category ya Farming and Livestock baadala ya banking, economics and financial services.

Hizo kwenye picha ni course structure tulizosoma Chuo Kikuu.

Unaweza ona namna gani tupo competent kwenye banking kuliko kilimo kiasi kwamba zinazotumwa ajira za kilimo tunashindwa kwenye interview, maana maswali yana-base kwenye kilimo moja kwa moja wakati sisi tumesoma kilimo uchumi zaidi, kwa hiyo wale waliosoma Agriculture General wanakuwa na advantage.

1773852321189.jpeg

1773852348963.jpeg


1773852405716.jpeg
 
Back
Top Bottom