Wahitimu ualimu wazua tafrani wizarani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahitimu ualimu wazua tafrani wizarani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 25, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Wahitimu ualimu wazua tafrani wizarani


  Na Benjamin Masese

  SAKATA la baadhi ya walimu waliohitimu mwaka 2009/2010 la kuvamia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi kudai ajira limeingia sura mpya baada ya
  jana kuzua tafrani kati yao na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Hamisi Dilenga wakati akiwaeleza utaratibu uliopangwa na Utumishi kuajiri.

  Bw. Dihenga aliwaeleza kwamba Wizara ya Utumishi ndio yenye mamlaka ya kutoa nafasi za ajira na hivi sasa imesitisha rasmi mpango uliokuwepo wa kuwapa ajira walimu waliofeli baadhi ya masomo yao na kuwapa muda wa miaka miwili kuyarudia.

  Alisema kuwa baada mpango huo kusitishwa ghafla wizara ya elimu ililazimika kufanya mazungumzo na baadhi ya vitengo vinavyohusika, ambapo walikubaliana kwamba walimu hao wanatakiwa kusajiliwa upya katika vyuo ili kurudia masomo hayo kabla ya Mei mwaka huu ili wapeww ajira, kitendo kilichozua zomeazomea na maswali mengi.

  Maneno makali ya kukaripiana kati ya walimu na Bw. Dihenga yalitawala wizarani hapo, hali iliyomfanya kiongozi huyo kuwahoji kama wanatambua wanayeongea naye na ana nafasi gani kwao, ndipo walizidi kumhakikishia kwamba wanachohitaji ni haki yao na sio kuangalia cheo chake.

  Ilifikia wakati Bw. Dihenga kutoa majibu ya mkato na kwa hasira kulingana na maswali yaliyokuwa akiulizwa kwamba kuna walimu waliofeli na wameajiriwa na wengine ambao hawakufeli wameachwa.

  Bw. Dihenga alisema kwamba wizara ya elimu haina mpango wowote wa kutoa ajira nyingine kulingana na maagizo kutoka wizara ya utumishi na kuongeza kwamba cha kuwasaidia ni kuwaombea Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) kupokea fedha zao za usajili ili kurudia mtihani wa masomo waliofeli.

  Walimu hao walisema kwamba hawako yatari kurudia mtihani huo kwa madai kwamba wizara imetoa ajira ya kujuana kwani kuna walimu walifeli zaidi ya masomo matatu, wanafahamu kwa majina lakini wameajiriwa huku.

  Bw. Dihenga alitoa tamko kwamba walimu wote walioajiriwa huku wakiwa hawakufaulu masomo yao watanyang'anywa ajira hiyo na kuwapa waliofaulu hata kama walisharipoti shuleni.

  Baada ya maswali kuzidi, Bw. Dihenga alivunja kikao kwa hasira na kusema tafuteni mwingine anayeweza, pia nendeni mnapoweza, lakini mtarudi kwangu, hali iliyosababisha walimu kwenda Ofisi za Waziri Mkuu na kukumbana na askari wa kutuliza ghasia getini na kuwaziua kuingia.

  Askari hao ambao tayari walikuwa wamejiandaa kwa lolote, waliwataka kuondoka hapo haraka kwa sababu sio sehemu ya kufanya mikusanyiko, pia waliwataka kuandika barua ya kumuona Bw. Pinda kwa siku maalumu.

  Awali, walimu hao walianza kumzuia Waziri wa elimu Dkt. Shukuru Kawamba asiondoke ofisi hapo hali iliyosababisha ulinzi kuimarishwa ambapo waliamua kubandika mabango kwenye majengo ya wizara hiyo.

  Baadhi ya mabango yalisomeka kwamba "Nini kazi ya Kawambwa, ni kukimbia majukumu yako au kufumbia macho kilio chetu, JK timiza ahadi zako za ajira kwa walimu au fedha ndizo mnazotaka kulipa Dowans, tumechoka na ubabaishaji wa serikali hii jamani adhabu yake ni mwaka 2015 tufanye kweli.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  mbeleko za JK za kumbeba mkwere mwenzie yaelekea karibu zitakatika........................
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hawa wanalimu wamechukua wrong move.

  Kwanza, wamekubali kuwa hawana sifa na wanasisiiza kuwa hawataki kutafuta hizo sifa. Tutanataka walimu wenye sifa, hawa wasio na sifa ndio wanaochangia kushusha kiwango cha elimu nchini.

  Pili, nadhani hawako makini na taratibu za ajira, waende kulalamika wizara inayoajiri.

  Tatu, two wrong does not make a right. Kama walimu wasio na sifa wamepata ajira, haimaanishi na hawa wenye madai (ambao pia hawana sifa) nao wapate ajira. Kinachotakiwa ni hao walioajiriwa bila sifa waenguliwe.

  Kwa upande wa Katibu Mkuu Dilenga naye hajui kudeal na crisis, ukiwa kiongozi hutakiwi kuonyesha hasira, kutumia jazba na vitisho vya cheo.
   
Loading...