Wahitimu kulipa madeni ya mikopo ya Chuo

Paroko da travellor

Senior Member
Oct 16, 2012
102
101
Habari wakuu,

Nimeona waziri Ndalichako kamsimamisha kazi kiongozi anayehusika na kukusanya madeni ya mikopo ya wanafunzi waliokopa bodi siku za nyuma.

Je, Ni halali wanafunzi kulipa madeni?
 
Sababu ni mfumo mbovu tu. Kulipa mkopo wangelipa hazina moja kwa moja na ripoti iwe inatoka kila mwisho wa mwezi kuwa zimekusanywa fedha kiasi gani!
 
Kulipa ni lazima. Sema hapa kulukuwa na kamchezo wa alipewa jukumu la ukusanyaji alijiwekea utaratibu wa kupiga za walimu anakula halafu ili isiwe noma haangaiki na wengine kwa sababu waalimu huwa hawana noma.
 
mimi nishalipa lakini kwenye database ya Bodi ya Mikopo inaonyesha sijalipa chochote, hela niliyokuwa nakatwa vigogo wa Bodi ya Mikopo wamejengea Mahekalu MBEZI BEACH , natakiwa nianze upya kulipa upya, wana Jamvi naomba mnisaidie kulipa hilo deni la marudio
 
haa haa

haaa haaaaaaaa mpigie kassim mkuu...
 
Mi nadhani isiwe tabu MZK. Kama ulikuwa unalipa deni la mkopo kupitia mwajiri kuna uthibitisho wa makato wapelekee. Kama ulikuwa unalipa Bodi ya Mikopo wewe mwenyewe una risiti zao waonyeshe. Wakikukatalia wapeleke kwa Pilato. Labda kama unanogesha gumzo jamvini!
 
Sababu ni mfumo mbovu tu. Kulipa mkopo wangelipa hazina moja kwa moja na ripoti iwe inatoka kila mwisho wa mwezi kuwa zimekusanywa fedha kiasi gani!
Watu hawa ni wajinga, na sioni kwa nini wasitumbuliwe. Asilimia kubwa ya wahitimu vyuoni wako serikalini na wachache wako sekta binafsi.

Wanachotaka mtu ajipeleke mwenyewe ili akatwe.

Kwa nini kwa mfano wasianzie kwenye tamisemi kukusanya taarifa za watumishi wenye degree na kuanza kukata? Kwa nini wasifike kila idara kuanzia wilayani kuchukua database ya watumishi kubaini wenye degree?

Uzembe tu na ili kulinda ufisadi eti wamewapa kampuni ndo ikusanye madeni wakati wao wenyewe kazi wangeiweza.

Watumbuliwe tu
 
Nilishtuka sana kusikia na anayesimamia marejesho naye katumbuliwa, nikajiuliza sababu za kutumbuliwa, nikawaza kama sababu nikutokukusanya madeni watakua wamemuonea sana. Watusamehe tu wengine tuna miaka mitatu kazini (private) lakini kodi (PAYE) tuliyolipa serikalini ni mara 10 ya huo mkopo sasa wakitudai na mkopo watakua wanatuonea kwa kweli mana tumeshachangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa,mtu nalipa kodi minimum laki 4 kwa mwezi bado unataka unikate na hiyo loan. Daaaaaah wawe na huruma kidogo.
 
Watu hawa ni wajinga, na sioni kwa nini wasitumbuliwe. Asilimia kubwa ya wahitimu vyuoni wako serikalini na wachache wako sekta binafsi.

Wanachotaka mtu ajipeleke mwenyewe ili akatwe.

Kwa nini kwa mfano wasianzie kwenye tamisemi kukusanya taarifa za watumishi wenye degree na kuanza kukata? Kwa nini wasifike kila idara kuanzia wilayani kuchukua database ya watumishi kubaini wenye degree?

Uzembe tu na ili kulinda ufisadi eti wamewapa kampuni ndo ikusanye madeni wakati wao wenyewe kazi wangeiweza.

Watumbuliwe tu
Kigezo sio wenye degree maana kuna watu wenye degree wamesomeshwa na wazazi/walezi wao kwa 100% hawakupata mkopo wowote kutoka HESLB.
 
Back
Top Bottom