Wahindi walazimisha kuuziwa nyumba za Upanga

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Hivi hawa wahindi wanatutafuta nini?
Ubaya ni kwamba wanawatumia watanzania wenye uroho wa fedha kutuhujumu.
Yani daktari wa muhimbili anaishi kiluvya wakati muhindi ananing'iniza miguu na kula pariki pale upanga,halafu tunajiuliza vifo vya kina mama na watoto vitapungua vipi.
Nchi hii?!!
 
namkumbuka Idd Amin Dada, huu ujinga aliukataa siku nyingi
 
NHC mkiwauzia hizo nyumba mjiandae kuuza nyumba zote za shirika hili.
 
ni kweli haya magabachori hayana faida kwetu, ila taito yako haiendani na ulichoandika. labda uweke details mkuu
 
Historia inaeleza kwamba hizo nyumba zilikuwa zao zikataifishwa. Kutoka Msajili wa Majumba hadi shirika la Nyumba. Naona wanataka kurudisha historia ya umiliki wao.Kinachotakiwa ni NHC kuweza kujenga majengo yatakayoendana na uwingi wa watu na kuondokana na mijengo ya zamani. Kiufupi wajenge Maghrofa ya nguvu kwenda juu kuwezesha wapangaji wengi.
 
hiyo historia imeanzia mwaka gani?
 
Nashauri wapelekwe msanga au tandahimba wapewe viwanja vipya waviendeleze!
 
hata kama zilikuwa zao sasa hv ni zetu na ni mali yetu na iuzwe kwa wazawa ...........
 
wahindi hawana makosa, tutalaumu wahindi, na baadae wakenya, baadae waarabu, baadae wazungu. tatizo lipo katika nchi yetu, kwanza tukubali sisi ndio problem
 
Hivi hawa wahindi wanatutafuta nini?
Ubaya ni kwamba wanawatumia watanzania wenye uroho wa fedha kutuhujumu.
Yani daktari wa muhimbili anaishi kiluvya wakati muhindi ananing'iniza miguu na kula pariki pale upanga,halafu tunajiuliza vifo vya kina mama na watoto vitapungua vipi.
Nchi hii?!!

Habari zako za kinafik nafik. Hao wahindi hizo pesa walizitowa wapi? Au wao wanauwezo wa kuzitafuta zaidi yako? Majumba ya Upanga yalijengwa na wahindi na yakadhulumiwa na nyerere na wapangaji ambao si wahindi huziuza kwa shida zao za pesa.

Au hujui kuwa wengi wetu hata tukifiwa Dar basi hata kama kuuza flat tutauza ili tusafirishe maiti Kilimanjaro au Kagera au Mbeya? Au hujuwi kuwa wengi wetu tukiwa na kipaimara basi hata flat tutauza ili tukifanye cha nguvu? Au hujuwi kuwa wengi wetu tukimcheza mwari tutauza hata flat?

Ujinga wetu ndio maradhi yetu.

Wahindi ni wachapa kazi, wametoka walikotoka wakaanza kuuza bajia, chachamawa, kachori lakini tazama baada ya muda wako wapi? Na hausikii wanamcheza mtoto, wanakipaimara, wana harusi za kifahari, wana maziko ya kuleweshana. Wao kazi, kazi, kazi. Ndio maana unawaona wao ndio wana mafanikio. Wahindi huanza kula maraha wakishajijenga kimaisha na si kabla.

Tusitake kuwalaumu wahindi kwa uzembe wetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom