Waheshimiwa Mawaziri manunuzi ya mavazi yao huwa yanayafanyia wapi?

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Habari wana JF popote mlipo bila shaka wazima wa afya nyote,

Katika kutembea kwangu kote sehemu mbalimbali za Maduka Makubwa (Mall), Mlimani City, Woolworths, Quality Center, Mkuki Mall, City Mall na mengineyo. Haki tena sijawahi kukutana na Waziri wa Serikali ananunua mahitaji ya nguo au viatu katika maduka hayo, ambapo ni vitu muhimu kwa binadamu

Jambo hili linazua maswali mengi kuliko majibu. Je fikra zangu ziko sawa kuwa huenda wanaagiza kutoka nje ya nchi.

Na kama wanaagiza kutoka nje ya nchi, inakuwaje usumbufu unaopatikana katika size ya nguo na rangi pamoja na fashion, style ya mtu apendavyo. Mfano utakuta labda unavaa Suruali size 32 lakini ukiijaribu yawezekana kabisa iwe ndogo kwako ilhali ni size 32 ndo unavaa, inabidi sasa utafute yenye kukuenea.

Sasa kama umeiagizia nje ya nchi inakuwaje kupata ile yeye kukuenea na uipendayo ? Na gharama zingekuwa kwa nani? au katika Ofisi zao kuna mafundi wa nguo?

Ikiwa hawa Waheshimiwa Shopping wanafanya hapa nchini, ni kwenye Maduka yapi? Bila shaka kuna wataalamu hapa JamiiForums watauondoa utata huu kwangu hivi punde.

Nawasilisha!
 
Hakuna ujinga wowote ule na umefanya jambo zuri sana kusema ukweli kwa kuleta uzi wako hapa.

Kila mtu ana mambo yake anayopendelea kufuatilia na kufanya kwa manufaa yake binafsi au wengine ili aweze kuifurahisha nafsi yake na kuituliza.

Kwa jinsi ninavyofahamu mimi ni kwamba: Kuna wataalamu wa nguo na Madesigners hapa Tanzania na hasa Dar ambao wao wamejikita zaidi kutengezeneza Nguo Nzuri na kuziuza kwa gharama kubwa sana kulingana na mahitaji ya Malighafi na ubora wa bidhaa zao.

Hawa ni baadhi yao: Sheria Ngowi, Mustafa Hassanli, Ally Remtullah na wengine wengi tuu ambapo Maraisi wa nchi mbalimbali Africa na Viongozi wa njanja mbalimbali hupenda kwenda au kuwaita na kufanya nao biashara hasa haya mambo ya nguo, utunzanji na vipimo vilivyo sahihi kabisaa.
Ukipata nafasi pitia kurasa zao za Instagram na utagundua mengi.

Taarifa tu: Rais wa Zambia Edgar Rungu hupendelea kuvaa suti za Sheria Ngowi wa Tanzania.

"Kipendacho Roho, Hula Nyama Mbichi."

Nawasilisha.
 
Mpaka sasa nimepata jibu mujarabu. Asante mkuu kwa darasa, ubarikiwe

Mkuu wapo watu kutotaka kujifunza kwa mwingine au kuuliza, kumewapelekea kufanya mambo ya ovyo kabisa

Na hao ni chimbuko la viongozi mbumbumbu. Hawatupi shida kamwe
 
Moja ya mifano:
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    137.9 KB · Views: 39
  • tatizo 2.jpg
    tatizo 2.jpg
    37.8 KB · Views: 87
Habari wana JF popote mlipo bila shaka wazima wa afya nyote,

Katika kutembea kwangu kote sehemu mbalimbali za Maduka Makubwa (Mall), Mlimani City, Woolworths, Quality Center, Mkuki Mall, City Mall na mengineyo. Haki tena sijawahi kukutana na Waziri wa Serikali ananunua mahitaji ya nguo au viatu katika maduka hayo, ambapo ni vitu muhimu kwa binadamu

Jambo hili linazua maswali mengi kuliko majibu. Je fikra zangu ziko sawa kuwa huenda wanaagiza kutoka nje ya nchi.

Na kama wanaagiza kutoka nje ya nchi, inakuwaje usumbufu unaopatikana katika size ya nguo na rangi pamoja na fashion, style ya mtu apendavyo. Mfano utakuta labda unavaa Suruali size 32 lakini ukiijaribu yawezekana kabisa iwe ndogo kwako ilhali ni size 32 ndo unavaa, inabidi sasa utafute yenye kukuenea.

Sasa kama umeiagizia nje ya nchi inakuwaje kupata ile yeye kukuenea na uipendayo ? Na gharama zingekuwa kwa nani? au katika Ofisi zao kuna mafundi wa nguo?

Ikiwa hawa Waheshimiwa Shopping wanafanya hapa nchini, ni kwenye Maduka yapi? Bila shaka kuna wataalamu hapa JamiiForums watauondoa utata huu kwangu hivi punde.

Nawasilisha!
Shopping dubai kila weekend!
 
Mimi mwenyewe suti zangu sinunui spesho. Nachagua kitambaa (kuna material nzuri tu zinatoka Uturuki na kwingineko) nashonea kwa fundi wangu anayenishonea suti zikanikaa vizuri. Tatizo la hizi nguo za spesho ni kwamba saizi inaweza kuwa ni sawa kwa suruali lakini kwenye koti mikono ikawa mifupi au mirefu. Suruali pia zinaweza kuwa na kiuno na urefu sahihi lakini ikabana kwenye sehemu ya mapaja. Kwa hiyo, mimi nimeamua kwa miaka kadhaa sasa kushonesha tu suti zangu zote. Ukwa na fundi mzuri, suti ya kushona inaweza 'kukukaa' mpaka kila mtu anakusifia
 
Heri ya hayo ya kutotaka usumbufu jambo jema hilo.
 
Back
Top Bottom