Wahaya na Wachaga bana

Bonesmen

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
929
991
uploadfromtaptalk1465720827947.jpg
 
Mimi mwenyew ni mhaya ila nachukizwa sana na watu wanaotaka sifa kutoka kwa watu afu mkoa wetu uko choka mbaya jaman
Mkoa wenu uko choka mbaya huko wilayani kwenu mkuu kwetu kama nje! Umasikini unaozungumziwa hapa sio umaskini wa maendeleo ni umaskini wa kipato kwa individuals! Na hii inatokana na mkoa wa Kagera kutokuwa na zao maalum au shughuli maalumu ya kuwaigizia kipato wakazi wa Kagera hasa baada ya Kahawa ambalo lilikuwa zao kuu la biashara kuporomoka vibaya sana. Wakazi wa Kagera sasa wanaishi % kubwa wakitegemea ndugu zao wasomi wanaofanyankazi nje ya mkoa na nchi hii haiwezi kupandisha kipato cha individuals! Kuna watu hawaelewi hizi takwimu zinahusu nini wamekariri chorus ya neno 'maskini'. Kama kigezo kwa mikoa iliyotajwa basi na mkoa wa Mwanza ni maskini kuliko Simiyu au Geita!?? Ishu ni ile ile ya kushuka kwa zao la pamba na vitega uchumi vingine vinavyomuingizia kipato mwananchi wa mkoa wa Mwanza na sio physical development! Ukiichukua Kagera ukailinganisha na mkoa wowote katika nyanja za maendeleo kama elimu (wingi na ubora wa shule + matokeo), miundo mbinu, nyumba (makazi) za watu za kuishi, n.k huwez kuilinganisha na hata mkoa kama Dodoma wanapojenga vile vi bus na wakaziita nyumba za kuishi au mikoa mingine kama Tabora, Simiyu, Shinyanga, Karatu, na mingine mingi. Nashauri kwa asiyepajua Bukoba afike Bukoba (sio kulinganisha mji ulivyojengwa tu na ukajidai umefanya comparison) nenda vijijini uangalie maendeleo yanayoonekana na kushikika (physical dvt) ulinganishe na mikoa uliyowahi kutembelea hadi vijijini. Nadhan ukirudi utatafuta post yangu unipe like.
Siitetei Kagera ila kiukweli wakazi wamekuwa maskini sana wa kipato kiasi cha kushindwa hata kumudu mahitaji yao ya msingi kwa siku! Nadhani wananchi wa Kagera ni wakati sasa wa kubuni shughuli/kilimo kingine cha kuwapatia kipato. Vinginevyo ndugu zenu mtatuona huku mjini tunakula maisha na kupewa sifa nyie mnakufa kwa njaa huko vijijini mnasubiri kuletewa na akina #Bepari. Cha kupewa hakiwezi kuwa sana na cha kujitafutia. Mtegemea cha nduguye hufa maskini. Mnakera sana!
 
Wahaya utajiri wao unatokana na SENENE Almaarufu PANZI, na NDIZI, si ajabu huyo kaka kauza senene zake kanunua AUDI
 
Back
Top Bottom