Wahariri wa jiini Mwanza wamlilia marehemu mwalimu Sokoro, aliyekuwa mhariri wa BARMEDAS Tv

Mar 12, 2016
73
33

Aliekuwa Mhariri wa miaka mingi wa katika kituo cha runinga cha Barmedas Tv cha Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro, enzi za uhai wake. Marehemu Sokoro alifariki dunia jumamosi julai 16,2016 majira ya saa mbili usiku katika hospitali ya Rufaa Bugando alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

Wanahabari Jijini Mwanza wakieleza namna walivyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake

Wanahabari Mwanza wakieleza namna wavyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake.
Ni juzi tu Tasnia ya Habari ilipata pigo kwa kumpoteza Mwandishi mbobezi kwenye dimba la michenzo Dada yetu mpendwa Elizabert, na leo tasnia hiyo hiyo imekubwa na msiba mwingine wa kaka yetu sokoro. HAKIKA msiba wa ndugu yetu Sokoro umetuacha midomo wazi tunahisi km ni ndoto ya usiku lakini ndio ukweli.

Nani asiye mjua sokoro kwa ukarimu wake kwa kila mtu ? Kiukweli alikuwa mcheshi asiye na makuu. Aliipenda taaluma yake kwa dhati na kila penye kusanyiko la wanahabari naye alimuwepo.

Hakuonyesha umahiri pekee kwenye tasnia ya habari bali hata kwenye mambo mengine. Nani asiyejua uwezo wake.kwenye kupiga kinanda?. Nani asiyejua umahiri wake kwenye kuenzi utamaduni wa kiafrika?

Kipindi chake cha ngoma asilia pale Barmedas kilileta uhalisia wa utamaduni wetu. Sokoro waandishi wenzako tunakulilia umetuacha kwenye wakati mgumu.

Tutakukumbuka daima tulikuoenda lakini Mungu kakupenda zaidi na alikuita na umeitika leo haupo nasi. Huu ni wakati mgumu sana kwa tasnia ya habari. Mungu tupe nguvu tumpumzishe mwenzetu kwa mikono yetu miwili.
AMINA!
NAEDWIN SOKO;
MRATIBU, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MWANZA (MPC).
 
Inaelekea hii blog inahamishiwa humu sasa. Mara binti mwenye ndoto, na sasa habari hii. Hamna wasomaji wa blog yako huko?
 
Back
Top Bottom