Katika hali ya kusikitisha nchi yetu imevamiwa na wahamiaji haramu ambao wamefanikiwa kuwateka wenye dhamana ya kulinda nchi na kuhakikisha Sheria za nchi zinafuatwa.
Mikoa yote inayopakana na nchi jirani wahamiaji haramu wamefanikiwa Kwa kiwango kikubwa kununua ardhi kinyume na sheria za nchi yetu, ukitoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika hawajui la kufanya lakini mbaya zaidi wanaweza kukugeuza mtuhumiwa!
Nchi hii imepoteza wazalendo wengine inatubidi kuangalia tu kwa uchungu tukisubiri siku moja kutokee Watumishi wa Umma watakaokuwa na uzalendo vinginevyo wajukuu wetu tutawaachia vita na migogoro.
Asilimia kubwa wana vitambulisho vya mpiga kura na wanapiga kura katika nchi yetu na tunaangalia kama vile haituhusu ni kwasababu tumeleweshwa na mlungula.
Wenzetu waliopewa dhamana ya kutoa Vitambulisho vya Taifa nao hawako nyuma, wanatoa vitambulisho kwa wageni hao kwakutumia taarifa za uongo hata kama ni kinyume cha sheria, lakini bado ni tatizo kufanya hivyo na kuifanya nchi hii ionekane kama shamba la bibi. Hivi kweli hakuna wenye uchungu na nchi hii?
Siyo kwamba Raia wa kigeni hawafai la hasha, maana yangu ni kwamba kwakuwa kunasheria zilizopo kuhusu wahamiaji basi zifuatwe.
Kuna wahamiaji haramu na kunawahamiaji ambao wanafanya biashara haramu na kuna wahamiaji wanaoharibu maadili ya nchi yetu. Mfano Wachina na mashine zao za kamali huu ni mtandao ambao unaharibu maadili ya nchi yetu na unawagusa wanachi wenye kipato cha chini.
Kwa ufupi sioni kama waliopewa dhamana na mambo haya kama wanajali zaidi ya kufanya biashara batili. Ni Rai yangu kwamba tuige nchi za wenzetu jinsi wanavyokuwa makini na wahamiaji haramu hali inayowalazimu kufuata sheria za nchi.