Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,512
Dokta Tulizo Shemu ni mmoja wa madaktari bingwa wa Moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambaye amesisitiza ushirikiano huo utasaidia kuwajengea uwezo ikiwemo matumizi ya teknolojia za sasa na pia utaokoa zaidi ya shilingi bilioni 2.4 iwapo wagonjwa hao wamesafirishwa nje ya nchi ikiwemo India kwa ajili ya upasuaji wa moyo kama huo.
Bwana Bader al Anezi ni mtaalamu wa mishipa ya Moyo na mwalimu toka nchini Saudia Arabia amesema taasisi ya kimataifa ya misaada ya kiislamu inalenga kutoa huduma ya matibabu ya Moyo na kubadilisha uzoefu na wataalamu wa matibabu wa Moyo wa kitanzania na kusisitiza moja ya changamoto zinazowakabili ni taratibu ngumu za utoaji wa matibabu ya Moyo hususani katika operesheni.
Akizungumza na ITV mmoja wa wagonjwa wa Moyo waliokwisha mfanyiwa matibabu amepongeza jitihada zinazofanywa na madaktari hao katika kutibu magonjwa ya Moyo kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kwenye mishipa ya damu badala ya kupasua kifua ambapo amewataka watanzania kutumia taasisi hiyo na kuondokana na dhana ya kufuata matibabu ya moyo nje ya nchi.
ITV