Wagombea urais tunaomba kujua mmefanya nini kwanza kabla ya kutupa nyimbo mpya

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Tumekuwa tukishuudia wagombea urais mbali mbali wakijitokeza kuomba nafasi na hili nawapa hongera
baadhi ya wausika wamekuwa serikalini miaka mingi sana kwahiyo tungependa kujua kabla ya kutueleza mambo mapya utakayoyafanya endapo utachaguliwa tuambie kwanza ulichokifanya kwa nafasi yako hiyo ndogo uliokuwa nayo kabla ya kutaka nafasi kubwa.

Inatia aibu sana kumuona mtu amekaa serikalini miaka mingi leo anasimama mbele ya wananchi anatangaza nia ya kugombea urais lakini anachokitaja katika utimushi wake wa muda mrefu ni Titles pekee yake Zero accomplishment. kama uliwahi kuwa waziri wa wizara fulani hiyo siyo accomplishment bali ni title je ulifanya nini kwa nafasi hiyo ndogo uliyopewa kuondoa baadhi ya matatizo waliyonayo watanzania. napenda kurudia kuwa vyeo au titles siyo accomplishment/uliyoyafanya kuwanufaisha au kinachoendelea kunufaisha wananchi kwa ajili ya ya cheo ulichopewa.

Kwa mfano mtu amekaa bungeni miaka 20 hajawahi hata siku moja kukemea rushwa leo anakuja anadai anachukia rushwa inashangaza sana. kwa wale wagombea ambao hamjatangaza tunaomba mtuambie mmefanya nini kwanza kabla ya kutupa ahadi na mipango mingine mipya.
 
Brother your very wright. Hatuhitaji mtu aje atuambie nitafanya hivi au vile. Atuambie nimefanya hivi na niliishauri serekali kufanya kile. And then from there ndo tumuamini kwamba kumbe alishatenda na ni mtu wa action. Si wakati wa mashairi ni wakatiwa vitendo then tukuhukumu kwa vitendo vyako.
 
Back
Top Bottom