Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge wawili wa ACT-Wazalendo wawajia juu Maalim Seif na Zitto Kabwe kwa kumuunga mkono Tundu Lissu

Natabiri kuna wana jf humu leo siku imewaishia vibaya.🤣🤣🤣 kama unaweza kuwataja we wataje.



MAGUFULI4LIFE.
 
siasa ni sayansi... hao jamaa wako timamu kabisa... kuna kundi kubwa linatafutwa kufuata kauli ya kiongozi mkuu wa chama... sababu maneno ya hao wachache yatawafanya wengine waone kwamba wenzao hawataki mabadiliko na hawana nia ya kumuondoa ccm... hasira juu yao itawafanya wengine waunge kauli ya kiongozi wa chama kwa wingi...
siasa ni sayansi
Wala hawawezi kuwaondoa watanzania kwenye ajenda kuu ya kuwatoa Ccm madarakani mwaka huu.

Hawa wote ni wana Ccm waliotumwa kuokoa jahazi kwa kuleta taharuki ila uzuri ni kwamba watanzania mwaka huu hatubabaishwi na siasa za matumbo. Tupo serious na jambo letu la kuwatoa Ccm madarakani!!
 
Natabiri kuna wana jf humu leo siku imewaishia vibaya.🤣🤣🤣 kama unaweza kuwataja we wataje.



MAGUFULI4LIFE.
Yaaani siku iharibike kwa sababu ya mamluki wa Ccm waliotumwa kwa makusudi kuharibu ajenda kuu ya watanzania ya kuwatoa Ccm madarakani mwaka huu????

Mtasubiri sana. Kila mbinu yenu lazima ifeli mwaka huu. Ajenda kuu ya watanzania mwaka huu ni ile ile Tundu Antiphas Lissu Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025 na Maalim Seif Raisi wa Zanzibar 2020-2025
 
Ha ha ha Chama cha Mbowe cha hovyo sana. Hivi kule kwenye chama chenu mtu bright ni nani?. Maana kuanzia mwenyekiti mpaka shabiki ni utopolo mtupu.Chama kilicholaaniwa hicho.
Genius wetu ni huyu.
EkjOyBlX0AEyvSk.jpg
 
Yaaani siku iharibike kwa sababu ya mamluki wa Ccm waliotumwa kwa makusudi kuharibu ajenda kuu ya watanzania ya kuwatoa Ccm madarakani mwaka huu????

Mtasubiri sana. Kila mbinu yenu lazima ifeli mwaka huu. Ajenda kuu ya watanzania mwaka huu ni ile ile Tundu Antiphas Lissu Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025 na Maalim Seif Raisi wa Zanzibar 2020-2025
Kama Corona ilimkimbia leo maneno yako tu haya hebu tulia hii nchi iendele. Kama waafrika tunahitaji heshima yetu tuliyoporwa kwa miaka mingi.


MAGUFULI4LIFE.
 

WAGOMBEA wawili wa kiti cha Ubunge wa Chama cha ACT-Wazalendo kupitia majimbo ya Kibamba jijini Dar es Salaam na Kyerwa mkoani Kagera wamewajia juu viongozi wa chama hicho kutokana na kauli yao ya kumuunga mkono mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu.

Wakizungumza katika mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Wagombea hao Mwesigwa Siraji wa Kibamba na Ntareyeiguru Frederick wa Jimbo la Kyerwa, kwa pamoja walisema kauli ya viongozi wao hao hazikubaliki na kwamba zimekiuka misingi ya katiba ya chama hicho.

Alisema wakiwa kama wagombea na wanachama wa chama hicho, hawawezi kulazimishwa ghafla 'kumpigia' debe Lissu hali yakuwa chama hicho kinaye mgombea wake wa nafasi hiyo ya Urais Bernard Membe ambaye kwa mujibu wao anakubalika maeneo mengi nchini.

"Kwa utafiti tulioufanya Membe atapata ushindi mkubwa kutokana na kukubalika na wananchi wengi, cha kushangaza wao wanamuacha na kushinikiza watu tumuunge mkono Lissu" alisema Siraji

Alisema kwa mujibu wa kifungu kilichopo ukurasa wa 21 wa katiba ya ACT Wazalendo, ni kinyume na utaratibu kwa mwanachama yoyote kumuunga mkono au kumpigia debe mtu kutoka chama kingine ambapo kwa kufanya hivyo mtu huyo anakuwa amejifuta uanachama ndani ya chama hicho.

Alisema kwa misingi hiyo, Kiongozi Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe pamoja na Mwenyekiti wao Maalim Seif Sharif Hamad wanakosa sifa za kuwa wanachama wa ACT-Wazalendo kwa kitendo chao cha kumnadi mgombea wa Urais wa CHADEMA Tundu Lissu.

"Kutokana na hatua hiyo tumepanga jumatatu tutakwenda kufungua kesi mahakamani kule Zanzibar ili ichukue hatua ya kumvua Maalim Seif nafasi yake ya kugombea Urais kutokana na kukosa sifa" aliongeza Siraji

Kwa upande wake Frederick alisema wao kama wanachama wa chama hicho wanalaani kitendo cha viongozi hao kuamua kumkacha mgombea wao Membe hali ya kuwa walimpitisha wao kuwania urais kupiti chama hicho.

"Isitoshe Membe alishiriki kwa ziadi ya asilimia 75 kuandaa ilani ya chama ya mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu, leo wanajitokeza hadharani kusema hawamtambui, hiyo siyo kweli sisi bado tupo naye hadi mwisho wa uchaguzi" alisema Frederick

Alisema wao kama wabunge wanaendelea kumuombea kura Membe katika majukwaa yote wanayosimama na imani yao ni kwamba atashinda kiti hicho licha ya hujuma anazofanyiwa na viongozi hao wa juu wa chama hicho.

Aidha kwa pamoja walikionya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kisitarajie mteremko katika nafasi zote kwa kuwa chama hicho kimejipanga kikamilifu kuhakikisha kinaibuka na ushindi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

View attachment 1609710

Pichani kulia ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibamba kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo,Mwesigwa Siraji akionesha kitabu cha Katiba yao ya chama hicho mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), ambayo amedai kuwa viongozi wake wa juu wanaikiuka na wao hawatokubali.Mwesigwa amesema kuwa wakiwa kama wagombea na Wanachama wa chama hicho, hawawezi kulazimishwa ghafla kumpigia debe Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu hali ya kuwa chama chao kina Mgombea Urais Ndugu Bernad Membe anaetambulika kisheria.Kushoto ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyerwa,Ntareyeiguru Frederic.

Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyerwa, Ntareyeiguru Frederic akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),kuhusu kulaani kitendo cha viongozi wa chama hicho kuamua kumkacha mgombea wao Mhe,Membe hali ya kuwa walimpitisha wao kuwania urais kupiti chama hicho."Isitoshe Membe alishiriki kwa ziadi ya asilimia 75 kuandaa ilani ya chama ya mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu, leo wanajitokeza hadharani kusema hawamtambui, hiyo siyo kweli sisi bado tupo naye hadi mwisho wa uchaguzi" alisema Frederick
Hela ya CCM inaliwa kiboya sana. Wameshadakishwa na Chakubanga vimilioni kadhaa wakinukishe
 
Yale Yale ya Pro, LIPUMBA na Dokta Slaa, ya kununuliwa na MaCCM ili KUVURUGA na KUUA UPINZANI,
Yalianzaga hivi hivi kama mzaha vile.
Membe Mungu anakuona.
Ndipo mnapotakiwa na nyie mutambue kuwa tatizo siyo Lipumba wala Slaa. Tatizo ni ushenzi wa Maalim Seif mnayemuona kuwa ndo mpinzani wa kweli.

Lipumba na Slaa hawahusiki na ACT lakini tatizo lile lile linajirudia kwenye chama alichokimbilia Maalim Seif. Kwa lugha nyingine hii inaitwa "carry over" au "cross contamination" kwa maana uwepo wa beberu hutambulika kwa harufu yake.
 
Wala hawawezi kuwaondoa watanzania kwenye ajenda kuu ya kuwatoa Ccm madarakani mwaka huu.

Hawa wote ni wana Ccm waliotumwa kuokoa jahazi kwa kuleta taharuki ila uzuri ni kwamba watanzania mwaka huu hatubabaishwi na siasa za matumbo. Tupo serious na jambo letu la kuwatoa Ccm madarakani!!
Sasa hao CCM uwatoe kutoka wapi na kuwapeleka wapi?! Mbona mnateseka na kupata taabu Sana? Kama ni kuwatoa madarakani Hilo haliwezekani..Lissu amefanya kosa la kimkakati...kuwakumbatia mabeberu na kuendekeza ushoga..
 
Sasa hao CCM uwatoe kutoka wapi na kuwapeleka wapi?! Mbona mnateseka na kupata taabu Sana? Kama ni kuwatoa madarakani Hilo haliwezekani..Lissu amefanya kosa la kimkakati...kuwakumbatia mabeberu na kuendekeza ushoga..
Mtajua hamjui mwaka huu. Jiandaeni tu kuwa wapinzani 2020-2025
 
Mtajua hamjui mwaka huu. Jiandaeni tu kuwa wapinzani 2020-2025
Unateseka bure Ndugu yangu...jiandae kuteseka zaidi baada ya Oktoba 28...Lissu huyo atashndwa vibaya mno..halafu hata kuandamana Kama mnavyodai kufanya haitawezekana...uchaguzi wa mwaka huu hauna nguvu Wala shamrashamra isipokuwa labda mtandaoni ndio ninyi sijui akina Lord denning ndio mnafurukuta..Lord dah..Lord.

Title hii siyo ya kawaida..katika maeneo mengi kwa sasa hapa TZ huyo Lissu anafahamika kwa sifa mbili...moja anataka wakoloni na mabeberu warudi kututawala...na ya pili anataka wanaume waanze kuoana wenyewe kwa wenyewe Kama wanavyofanya wazungu..kwa hiyo Lissu Hana kitu...
 
We ndio kilaza kweli, Kampeni ni za Chama sio za Membe as an Individual person weee nazi koroma
Ndo dk 89 za Membe hizi sio?
ACT ilikosea sana kumkaribisha Membe
Sasa mtu haonekani week tatu tangu kampeni zianze ulitegemea viongozi wafanye nini zaidi ya kuumga mkono Tundu Lissu
 
Yani watu wameamua wenyewe kushirikiana na chama ambacho si cha upinzani sijui kwa kutegemea nini halafu sasa wanakuja kulalamika et wamenunuliwa na ccm wakati walishasema toka zamani kuwa hicho chama(ACT) kinatumika na serikali ya ccm.View attachment 1609758
Wanaoharibu siasa za nchi hii ni Maalim Seif na Prof. Mbowe..!! Wajinga sana!
 
Hata ccm walisema Lowasa ni mwiz na fisadi je Leo lowasa yuko chama gani?
Ccm, cdm na act wote wajinga. Jembe la ukweli ni Prof. Lipumba tu kwa maana hashobokei makapi ya ccm. Mapema kuelekea uchaguzi wa mwaka huu Cuf ilishatoa msimamo wake kukataa mashirikiano na lichama lolote linaloshobokea makapi ya ccm.
 
Lowassa alitumwa kazi ameshaifanya pale chadema na sasa amerudi head office,Membe nae sasa yupo kazini hapo ACT akimaliza kazi nae atarudi Head office.
Cuf peke yake ndo imebaki na purity yake hasa baada ya kujiondoa Maalim Seif. Maalim na genge lake wamewapelekea pira ACT na mshirika wao cdm.
 
Lowasa alikuwa mpinzani?
Kwa cdm na babu yao Maalim Seif, Lowassa ndo mpinzani wa kweli na Lipumba ndo msaliti. Bichwa kuuubwa ndani hamna kitu, bure kabisa! Maslim aliwahi kusema bora kukaa meza moja na ccm kuliko Lipumba na kweli kaenda kumuokota Membe kada la Ccm liwe mgombea wao!
 
Back
Top Bottom