Wageni huweza kuungana kuwakabili wenyeji walioparanganyika na kuwashinda

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
WAGENI HUWEZA KUUNGANA KUWAKABILI WENYEJI WALIOPARANGANYIKA NA KUWASHINDA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Moja ya Kanuni za wakati wote kwa Watibeli ni kulinda Umoja wa watu wetu. Tunafahamu, umoja wetu utalindwa na kuhifadhiwa ikiwa HAKI itatendeka, UPENDO utatufunika, UKWELI utasemwa na kupendwa, na AKILI na MAARIFA itapewa Heshima.

Watibeli tunafahamu, huu ulimwengu hakuna mtu mwenye mali zozote isipokuwa zile zilizobuniwa na akili za wanadamu. Hii inamaanisha yote mwanadamu aliyoyakuta sio yake( mambo asiyoweza kuyakumba, tengeneza au yasiyowezekana kutengenezwa na mwanadamu).

Ufahamu huu ndio unatupa sababu ya kutumia zile kanuni za kujihami na kujilinda ili kujiepusha na mashambulizi ya maadui zetu.

Ardhi, bahari, anga, vito vya thamani, wanyama, uoto, miamba, hewa, gesi, miongoni mwa mali na rasilimali zingine tunajua hakuna mwanadamu na mtu anayemiliki daima.

Sio ajabu ukisikia nchi hii ilikaliwa na Watu wa jamii fulani na sio ajabu karne zijazo ikakaliwa na Watu wasio na vinasaba na sisi. Kwa kulijua jambo hilo ni lazima tufanye mambo kwa akili zenye macho.

Mali na Rasilimali hudhibitiwa kwa muda na Watu wenye Akili na nguvu, na umoja katika kulinda Maslahi yao ikiwa ni pamoja na kulinda na kuhifadhi akiba ya vizazi vyao kwa karne.

Udhibiti huo utafikia kikomo baada ya wenye akili na nguvu na umoja zaidi yao watakapojitokeza dhidi yao.

Taikon nafahamu, hatuwezi kuunganisha Watu wasiofanana hasa kiakili, kimaono, kimaslahi, kihisia, na kimtazamo. Uzalendo namba moja kwa Watu wenye akili na wenye kuona mbali lazima ulenge kuwafanya Watu wafanane walau kwa asilimia 70% hii itafanya moja kwa moja Watu hao kuwa na nguvu.

Kuzaa Watu wengi haimaanishi chochote wala lolote katika udhibiti wa mali na rasilimali. Kuzaa Watu wengi ni faida kwa watakaowatumia hao watoto wako kuwatumikisha ili kujiongezea nguvu iwe nguvu za kiuchumi, kiutawala, n.k.

Watu watatu huweza kudhibiti Watu elfu tatu wasio na akili, upendo, na haki. Waliokosa umoja na ushirikiano.

Wageni na hapa namaanisha wavamizi au walowezi kwa sababu kwenye hii dunia kila mtu ni mgeni. Lakini yule aliyetangulia kudhibiti eneo fulani atatambulika kama MWENYEJI, na yule ambaye atafuatia atatambulika kama MGENI.

Wageni ni lazima waishi katika hali ya ugeni ikiwa watakuta Wenyeji wenye Umoja, nguvu, haki ya wao kwa wao.
Jamii yenye uaminifu, kupendana ni jamii jasiri, ambayo adui mgeni hawezi kuiangusha.

Ugeni unapomtoka mgeni hii inamaanisha anapata nguvu katika udhibiti wa baadhi ya Mali na rasilimali. Na hiyo inamaanisha wenyeji wanapoteza nguvu yao.

Mgeni abaki kama mgeni hiyo hutumika na itatumika siku zote na Watu werevu. Ingawaje Wenyeji wenye akili kubwa huweza kuwatumia wageni wenye maarifa kujiongezea nguvu maradufu na kuongeza uenyeji huku wakimpumbaza mwenyeji kuwa naye anapatamo. Lakini haya yote katika kumtumia mgeni ni lazima kudhibiti umoja wa wageni.

Ni lazima kuwagawa wageni na kuwaweka vipande vipande ili kuwadhibiti.
Ni lazima kudhibiti utajiri na upatikanaji wa mali wa wageni ili kulinda nguvu ya wenyeji.

Taikon nataka kusema nini?

Wageni huanza kwa kudhibiti mali na rasilimali nyeti kabla ya kudhibiti Nchi na taifa zima na Watu wake. Huwezi idhibiti dunia au taifa kabla ya kuanza kudhibiti mambo nyeti yanayotegemewa na yenye kushika maisha na kuendesha maisha ya Watu na nchi au dunia.

Vita ya wenyeji na wageni ni vita vya kila siku. Vita vya maisha.

Acha Taikon nipumzike sasa. Leo sitaki maswali.

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mfano halisi ni hapa bongo, wageni Wana umoja na Sisi wenyeji tumepangaranyika hatimaye wageni wanatutawala kiuchumi kuelekea kututawala kisiasa.
 
Na hii inakuja Kwa kasi sana waunguja na wapemba wanapewa maeneo ipo siku Hawa kenge tutawafurusha vibaya sana
 
Mnangoja nini, au wamewazidi ujanja?

Wapemba wana akili sana, bila msaada wa USA wala Uingereza wala NATO wanajichukulia ardhi kiulaini kabisa.

Nasikia sasa hivi Wapemba ndiyo walimaji wakuu wa vitunguu Tanzania na pemba kwenyewe hawavilimi.

Na sasa nasikia wamejaa Ifakara na Mbarali wanalima mpunga.

Hapo sasa.
 
Umeongea kweli na point. Umenikumbusha mbali sana. Na ndivyo ilivyo kokote uendako falsafa inayotumika ni hiyo. Ni kama waafrika tunajihisi tuko huru il-hali bado tunatawaliwa na mzungu.
 
Mnangoja nini, au wamewazidi ujanja?

Wapemba wana akili sana, bila msaada wa USA wala Uingereza wala NATO wanajichukulia ardhi kiulaini kabisa.

Nasikia sasa hivi Wapemba ndiyo walimaji wakuu wa vitunguu Tanzania na pemba kwenyewe hawavilimi.

Na sasa nasikia wamejaa Ifakara na Mbarali wanalima mpunga.

Hapo sasa.

😀😀

Waja mnamambo
 
Ni hatari sana Faizafoxy
 
Back
Top Bottom