Wagagagigikoko ni watu wa wapi?

Wagagagigikoko ni watu wa wapi?

Hao ni KABILA na Mfalme aliyekuwa kwenye FIKRA za Msanii. Mwana Fasihi aliifasili na kuisawili Jamii. Ni Kama OKONKWO na Umuofia yake. Ki Uhalisia, Wahusika, maeneo na hata matukia ambayo ni kazi ya sanaa ni UBUNIFU. Ila kazi ya Sanaa IKIKUBALIKA, huchukuliwa na hadhira kama ni UKWELI... Rejea pia kazi za Fasihi kama za Musiba (na Willy Gamba wake), Xuma, JORAM KIANGO, Chonya wa Chilonwa, Lorienka Lenkaken, Obierika, Njoroge, Dkt. Stokimani, Honorable Chief Alhaj Dr. Nanga, MP.... na wengine wengi....
Omofia kwenuu
 
Hao ni KABILA na Mfalme aliyekuwa kwenye FIKRA za Msanii. Mwana Fasihi aliifasili na kuisawili Jamii. Ni Kama OKONKWO na Umuofia yake. Ki Uhalisia, Wahusika, maeneo na hata matukia ambayo ni kazi ya sanaa ni UBUNIFU. Ila kazi ya Sanaa IKIKUBALIKA, huchukuliwa na hadhira kama ni UKWELI... Rejea pia kazi za Fasihi kama za Musiba (na Willy Gamba wake), Xuma, JORAM KIANGO, Chonya wa Chilonwa, Lorienka Lenkaken, Obierika, Njoroge, Dkt. Stokimani, Honorable Chief Alhaj Dr. Nanga, MP.... na wengine wengi....
Chief Nanga
 
Je, umesha wahi kusoma kitabu (hadithi) ya Safari za Bulicheka? Kma bado NAPENDEKEZA ukitafute na kukisoma. Ni kizuri...
hivi vitabu vikiitwa 'Someni kwa furaha'. Kulikuwa na book 1 na book 2. Hadithi ya Bulicheka ilikuwa book 1, ambamo pia mulikwa na hadithi ya 'Kalumekenge alipokataa kwenda shule'.

Tumesoma hivi vitabu enzi zetu.
 
Mwenye kujua kabila hili chimbuko lake ni wapi anijuze mana nimesikia walikuwa na mfalme aliyeitwa Huihui au mfalme Juha! Wanatoka maeneo gani hapa Tanzania. Nahitaji kujua historia yao kidogo.
Zanzibar na sasa hivi wana kiongozi wao tanzania anaitwa Samia bushiri (mgagagigikoko wa makunduuchi)
 
Kuna uwezekano mkubwa Wagagagigikoko ni Wacomoro. Maana walikuwa wanaongea kiswahili na visiwa vyao vilikuwa ni volcanic. Unaweza kuisoma hadithi yao nzima ndani ya app ya Maktaba Sauti. Ipo playstore. Kusoma ni free.

Bulicheka alivyokutana na Wagagagigikoko.


SAFARI YA BULICHEKA NA MKEWE

SEHEMU YA PILI

Siku moja walipochungulia dirishani saa za asubuhi, wakakiona kitu cha ajabu. Wakaiona mashua moja inakuja. Kwanza wakaliona tanga peke yake, lakini halafu ilipokaribia wakaona ya kwamba walikuwamo watu ndani, watu wa namna namna. Watu wasiokuwa na desturi nzuri.

Lizabeta akasema, “Lo! Watu hawa ni watu wa ajabu. Wamevaa singa za wanyama kichwani na wameshika mikuki mkononi. Lo! Naogopa huenda wakawa wala watu.”

Bulicheka akajibu, “Haifai kuogopa kabla. Ngoja wafike kwanza. Labda hawatuoni hapa tulipo!”

Wakaipweleza mashua yao wakashuka pwani. Mmoja wao alikuwa mnene kabisa na mwenye uso mkali sana, akiwa amevaa upanga. Bulicheka na Lizabeta wakamtambua kwamba ndiye mfalme wao.

Basi, watu wale walisimama kwa muda kidogo, halafu wakaanza kukizungukia kile kisiwa kila upande, hatimaye wakafika pale mahali ilipokuwapo ile minazi minne ya Bulicheka, na nyumba yake ikiwa mwenye makuti.

Mfalme yule akawaonyesha wenzi wake na kuwauliza, “Je, ni ndege wa aina gani awezaye kujenga kiota kule mnazini? Mmepata kumwona ndege wa namna hiyo?”

Wakajibu, “Hatujapata kumwona bado ndege mwenye kiota kama hicho.

Akasema, “Hebu , tupige makelele mengi ili atoke.”

Wakapiga makelele mengi kwa sauti kubwa hata Bulicheka akalifungua dirisha lake, akachungulia nje. Akawauliza, “Je, nyinyi mnataka nini hapa?”

Mfalme mwenyewe akamjibu, “Wewe unafanya nini hapa petu msituni, tena unakaa mtini kama vile ndege? Shuka chini.”

Bulicheka akasema, “Mimi ninakaa mnazini kwa hiari yangu! Hili si shauri lako. Ondoka hapa, kuna faru mkali sana. Atakuchoma kwa pembe lake.”

Mfalme akajibu, “Wewe unanidanganya tu. Ni mtu wa aina gani wewe? Umekujaje hapa?”

Bulicheka akasema, “Mimi nimekuja kwa mashua kama mlivyokuja nyinyi. Nikajenga nyumba yangu hapa juu! Je, wataka nini?”

Bulicheka akaona ya kwamba hawataki kuondoka. Walikuwa watu wenye kutisha na kutia hofu kweli kweli. Hawakuvaa nguo yoyote ile isipokuwa singa za mbega vichwani mwao, na ukindu viunoni, wakishika mikuki mikononi. Yule mfalme mwenyewe alikuwa amevaa upanga mkubwa sana, na shingoni kwake alikuwa amevaa ushanga.

Wale watu walipoona ya kwamba Bulicheka amekataa kuteremka chini wakapiga makelele mengi zaidi. Mfalme akamwamuru ashuke lakini hata hivyo hakutaka, kwa maana aliogopa kwamba hao huenda wakawa wala watu wenye hatari. Mwishowe alianza kuwatupia nazi kwa sababu alikuwa hana silaha ya aina nyingine, upinde wake ulikuwa umebaki mwituni.

Mmoja wao akasema, “Hakika hatuondoki hapa mpaka umepigana na sisi.”

Bulicheka akajibu, “Mimi sina ugomvi na nyinyi. Aliyeanza kunichokoza ni huyu mfalme wenu. Mkitaka, nitapigana naye, lakini nawaambieni kweli kwamba nitamshinda tu.”

Wote wakayakubali maneno yake, wakaona ya kwamba inafaa iwe hivyo. Kwa sababu walikuwa hawampendi mfalme wao kwa dhati.

Basi, Bulicheka akashuka. Kila mmoja wao akapewa rungu ili wapigane kila mtu akiwa upande wake, walikuwa hawana ruhusa kuwa na silaha nyingine yoyote.

Yule mfalme, ambaye jina lake ni Huhihuihui akadhani atamshinda Bulicheka kwa dhoruba moja tu, kumbe sivyo!

Bulicheka alikuwa mwerevu kabisa, alikuwa akiangalia sana Huhihuihui anazungukia upande gani na hivyo akawa analiepa kila pigo, papo hapo yeye mwenyewe akilitumia rungu lake vizuri. Alikuwa mwerevu kiasi cha kumshinda mfalme Huhihuihui bila kuzichafua nguo zake.

Labda mnafikiri watu wale walikasirika kwa sababu Huhihuihui alikuwa ameshindwa, lakini sivyo hata kidogo. Kama nilivyosema, mfalme huyo alikuwa mbaya sana, watu wake walikuwa hawampendi kwa sababu aliwasumbua wenyeji.

Basi, walifurahi sana kwa sababu mfalme wao alikuwa ameshindwa, wakamfukuzia mwituni aende kujitafutia chakula chake peke yake.

Wakamweka Bulicheka awe mfalme wao. Akapewa upanga ule mkubwa wa Huhihuihui ambao ala yake ni ngozi ya chatu, na mpini wake wa pembe. Akapewa vilevile ule ushanga wa kifalme auvae.

Bulicheka akamwita mwenzi wake, “Lizabeta shuka sasa. Usiogope tena. Sasa umekuwa malkia. Angalia bahati yetu kubwa! Tulifikiri tumepotea kumbe tumekuwa wafalme. Sasa tufunge safari yetu kwenda nyumbani hasa.

Lizabeta akashuka, watu wote wakamwinamia kwa heshima kubwa. Sasa siku zao za kukaa kisiwani zimekwisha, watakwenda kutawala.

Lizabeta akamwambia Bulicheka, “Waulize ni watu wa kabila gani hao? Utawezaje kuwa mfalme wa watu usiowajua kabila lao?” Bulicheka akasema, “Kweli. Ngoja niwaulize.”

Akawauliza, “Ati, nyinyi ni watu wa kabila gani? Sisi hatujapata kuwaona watu kama nyinyi.”

Wakasema, “Sisi tu Wagagagigikoko. Nchi yetu ni nzuri sana. Ukiisha kuiona utashangaa.”

Basi walitaka kurudi sasa katika nchi ya Wagagagigikoko. Wakafanya maandamano wakienda mmoja mmoja, kila mtu akishika mkuki wake, na Bulicheka pamoja na Lizabeta wakifuata nyuma mpaka kufika pwani.

Mashua yenyewe ilikuwa imepwelezwa juu ya mchanga. Mkubwa mmoja akawaamuru wengine kuishusha majini. Ilikuwa ni kazi kubwa kwa sababu mashua ile ilikuwa nzito.

Ilikuwa ajabu jinsi mashua ile ilivyoundwa. Karibu yote ilikuwa imetengenezwa kwa magamba ya mti fulani yaliyoshonwa pamoja na uzi, kama vile wenyeji wa Lamu wanavyoishona mitepe yao.

Bulicheka na Lizabeta wakasimama pwani kuwangoja watu wote wawe tayari, Bulicheka akiwa ameushika upanga wake na kuuinua juu kama ishara ya enzi yake.

Hatimaye, watu wote wakawa tayari, wakaingia wote ndani ya mashua, kila mtu akakaa mahali pake. Wagagagigikoko wakatweka tanga, wakaanza safari ya kwenda katika nchi yao.

Lizabeta alikuwa akiogopa kidogo kusafiri tena kati ya mawimbi, lakini kwa bahati nzuri hawakupata upepo mkali, wakaendelea vizuri kabisa.

Baada ya saa chache wakafika katika nchi ya Wagagagigikoko. Hakika, ilikuwa ni nchi nzuri sana. Toka baharini wakaziona nyumba nyingi zilizotengenezwa na kujengwa kwa mtindo wa pekee na namna yao wenyewe, siyo kama zilivyojengwa nyumba za Dar es Salaam au zile za Mombasa, Morogoro au Nairobi. Nyumba za mji huo zilikuwa nzuri sana, lakini zote zilikuwa zimejengwa juu ya nguzo nyingi, na mtu akitaka kuingia humo alikuwa hana budi kutumia ngazi.

Mambo hayo yote waliyaona toka mashuani. Mabaharia wakashusha tanga, wakaipeleka mashua karibu ya nchi palipokuwa na ulalo wa kuwapokelea wageni.

Wenyeji wengi walikuwa wamekusanyika pale ili kumlaki mfalme wao.

Lakini mtu mmoja alijitokeza kwanza, akawapasha wenyeji wote habari ya kwamba yule mfalme wa zamani, Huhihuihui alikuwa amefukuzwa, na badala yake walikuwa wamemleta mfalme mpya, jina lake Bulicheka.

Hapo Bulicheka akasimama wima, na Lizabeta vile vile. Wenyeji wote wakarukaruka kwa furaha, wakapiga vigelegele walipomwona mfalme wao mpya akitoka mashuani na kuikanyaga nchi yao.

Mara Bulicheka na Lizabeta wakapelekwa kwenye nyumba yao ya kifalme. Nyumba iliyokuwa kubwa na nzuri kuliko nyingine zote.

Askari wawili wakasimama mlangoni, na mbele ya mlango zilikuwako nguzo mbili kubwa sana zilizochongwa kwa ubao na fundi hodari.

Wakaongozwa ndani hadi kwenye chumba kimoja kizuri kilichopambwa. Wakaambiwa waketi juu ya viti viwili ambavyo navyo vimetengenezwa kwa ufundi mkubwa. Lakini Bulicheka akakumbuka ya kwamba walikuwa hawajapata kula chakula cha maana kwa muda wa siku nyingi, akawaambia wale Wagagagigikoko waliokuwapo kwamba yeye anaona njaa, na Lizabeta vile vile.

Mara wapishi wa mfalme wakatoka kwa haraka wakaenda kupika vyakula vingi vya kila namna; na baada ya nusu saa wakarudi, msafara mzima wa watu, kila mmoja amechukua mkononi sahani, au bakuli au kikapu kilichojaa chakula.

Mtu wa kwanza akaleta sahani kubwa ya wali, yaani ndicho chakula cha kwanza. Watu husema, “Wali ni sultani ya chakula, watawazwa katika kiti.”

Wa pili akaleta kikapu kilichojaa vitumbua vya sukari. Wa tatu, akaubeba mkungu mzima wa ndizi zilizo kubwa sana. Wa nne akaja na kuku, kila mkono umemshika kuku mmoja. Wa tano, akaleta sahani ya mayai. Basi, wakala, wakashiba.

Saa za jioni kukawa na ngoma. Ngoma yao ya ajabu. Watu wote wakapiga, wakapiga hata kukawa na muungurumo wa kuziba masikio. Mtu mmoja alikuwa na mbiu moja ndefu sana kiasi cha kushindwa kuuinua kwa mikono yake, ikalazwa chini, naye akapuliza ndani yake, akiyavimbisha mashavu yake mithili ya balungi. Tena mtu mwingine alikuwa na namna ya zeze ambalo lina umbo kama pembe la nyati, mwenyewe akilipiga linatoa sauti kama mlio wa ndege.

Ngoma hizo ziliendelea kwa muda wa saa nyingi sana. Giza lilitanda juu ya nyumba za watu, lakini mwezi ukaonekana katika minazi.

Hatimaye wakaenda kulala, kwa maana Bulicheka na Lizabeta walikuwa wamechoka sana kwa sababu ya safari na kukaa siku nyingi katika nyumba yao mnazini. Na watu wote walipokuwa wamelala usingizi, mtu mmoja alikuwa akisimama juu ya mnara kama mlinzi, ili apate kuulinda mji pasitokee hatari yoyote ya kushambuliwa kwa ghafula.
 
Back
Top Bottom