Wagagagigikoko ni watu wa wapi?

steven1988

Member
Jan 31, 2017
30
27
Mwenye kujua kabila hili chimbuko lake ni wapi anijuze mana nimesikia walikuwa na mfalme aliyeitwa Huihui au mfalme Juha! Wanatoka maeneo gani hapa Tanzania. Nahitaji kujua historia yao kidogo.
 
Mkuu hizo ni hadithi za Bulicheka ndio hayo makabila yanatwaja, nadhani ni mambo ya kufikirika tu.
 
Hao ni KABILA na Mfalme aliyekuwa kwenye FIKRA za Msanii. Mwana Fasihi aliifasili na kuisawili Jamii. Ni Kama OKONKWO na Umuofia yake. Ki Uhalisia, Wahusika, maeneo na hata matukia ambayo ni kazi ya sanaa ni UBUNIFU. Ila kazi ya Sanaa IKIKUBALIKA, huchukuliwa na hadhira kama ni UKWELI... Rejea pia kazi za Fasihi kama za Musiba (na Willy Gamba wake), Xuma, JORAM KIANGO, Chonya wa Chilonwa, Lorienka Lenkaken, Obierika, Njoroge, Dkt. Stokimani, Honorable Chief Alhaj Dr. Nanga, MP.... na wengine wengi....
 
Hao ni KABILA na Mfalme aliyekuwa kwenye FIKRA za Msanii. Mwana Fasihi aliifasili na kuisawili Jamii. Ni Kama OKONKWO na Umuofia yake. Ki Uhalisia, Wahusika, maeneo na hata matukia ambayo ni kazi ya sanaa ni UBUNIFU. Ila kazi ya Sanaa IKIKUBALIKA, huchukuliwa na hadhira kama ni UKWELI... Rejea pia kazi za Fasihi kama za Musiba (na Willy Gamba wake), Xuma, JORAM KIANGO, Chinya wa Chilonwa, Lorienka Lenkaken, Obierika, Njoroge, DKT. Stokimani, Honorable Chief Alhaj Dr. Nanga, MP.... na wengine wengi....
oooh wataka kuniambia haya ni yakubuni na hakuna anayejua
 
bulicheka ni nani???!
Kuna kitabu cha hadithi nilikisoma kitambo sana miaka ya tisini hivi.
Ngoja nikupe dondoo kidogo kulingana na ninavyokumbuka.
Huyo Bulicheka ni mhusika mkuu ktk hicho kitabu nadhani kinaenda kwa jina la Safari ya Bulicheka (naweza kusahihishwa).
Bulicheka alikuwa na mke wake anaitwa Elizabeth. Nyumba yao ilijengwa juu ya mnaz.
BULICHEKA alisafiri(sikumbuki vizuri dhumuni la safari) na alisafiri kwa njia ya bahari kwa kutumia jahazi.
Bahati mbaya jahazi Lao lilipigwa na dhoruba baharini na hivyo likapasuka na Bulicheka aliokoka kwa kushikilia kitu ambapo kilimpeleka mpaka nchi kavu.
Huko katika nchi kavu alipofikia ndipo akakutana na hilo kabila la Wagagagigikoko na mfalme wao akiitwa Huihui.
(Utaniwia radhi kumbukumbu haipo vizuri sana kwa kuwa nilikisoma muda sana)
 
Uko SAWA kabisa Ndugu yangu. Dhumuni la safari ni KUTEMBEA/Mapuziko wakati wa Likizo. Ni kweli walitumia Jahazi. Walipo pata dhoruba, Bulicheka na Mkewe Elizabeth waliokoka kwa kuelea juu ya Meza. Wengine wote waliangamia. Walitua katika Kisiwa. Hapakuwa na makazi ya Watu. Waliogopa wanyama wakali. Walitengeneza nyumba yao kwa kujenga kati ya Minazi 4 ilokuwa karibu karibu. Walitumia meza yao kama "msingi" wa nyumba yao, na makauti kama paa. Nyumba ilikuwa juu kama kiota cha ndege mkubwa. Siku za mwanzo walikula chakula kidogo walicho okoka nacho, pamoja na madafu na nazi. Kuwa wakati Bulicheka alienda kuwinda, akamwua Mbuni kwa staili ya ajabu.
Ilitokea siku moja Mfalme (wa Bara) aitwae Huihui alitembelea kisiwa kile. Ilkuwa sehemu ya miliki yake. Alishangazwa na kiota kile cha ajabu. Akaawamuru wasaidizi wake kakaonewakaangalie kuna nini. Alishangaa zaidi kumwona Binadamu anaishi mle. Alimwamuru ashuke, Bulicheka akakataa. Akasema kama kweli Huihui anataka amani, WAPIGANE.....(inaendelea zaidi)...
 
endelea nimependa hadithi yako
 
endelea nimependa hadithi yako
Sawa kabisa. Ila SIYO HADITHI yangu. Nasimulia tu kile nilichokisoma (Kwenye Kitabu cha safari za Bulicheka nikiwa Darasa la 3).
Inaendela hivi....Baada ya Huihui kukubali kupigana, Bulicheka akamshinda Mfalme Huihui. Wananchi walifurahi maana Hui hui alikuwa hapendwi (inawezekana kabisa alikuwa Kiongozi dikiteta). Wakamfurahia Bulicheka. Kulikuwa na sherehe kubwa sana siku ya kumtawaza Ufalme. Elizabeth akawa Malkia. Basi Bulicheka akatawala vizuri na watu walimpenda. Aliwa fundisha mabo mengi, kama namna bora ya kutengeneza Mashua, kulima na kuhifadhi chakula nk. Ikatokea siku moja Meli toka Bara ilipita pale. Ikawa inaelekea Dar es Salaam. Akaomba KUKABIDHI NCHI. Akawaga wananchi wake. AKARUDI KWAO...na hapo ndipo hadithi iliposihia.
 
Kuna kitabu cha hadithi nilikisoma kitambo sana miaka ya tisini hivi.
Ngoja nikupe dondoo kidogo kulingana na ninavyokumbuka.
Huyo Bulicheka ni mhusika mkuu ktk hicho kitabu nadhani kinaenda kwa jina la Safari ya Bulicheka (naweza kusahihishwa).
Bulicheka alikuwa na mke wake anaitwa Elizabeth. Nyumba yao ilijengwa juu ya mnaz.
BULICHEKA alisafiri(sikumbuki vizuri dhumuni la safari) na alisafiri kwa njia ya bahari kwa kutumia jahazi.
Bahati mbaya jahazi Lao lilipigwa na dhoruba baharini na hivyo likapasuka na Bulicheka aliokoka kwa kushikilia kitu ambapo kilimpeleka mpaka nchi kavu.
Huko katika nchi kavu alipofikia ndipo akakutana na hilo kabila la Wagagagigikoko na mfalme wao akiitwa Huihui.
(Utaniwia radhi kumbukumbu haipo vizuri sana kwa kuwa nilikisoma muda sana)
Kitabu kiliitwa tu Bulicheka

Mke wa Bulicheka aliitwa Elizabetha

Safari yao haikuwa na dhumuni lolote isipokuwa kutalii tu

Baada ya merikebu kupigwa dhoruba waliokoka kwa kudandia meza iliyokuwa ikielea

Walipofika nchi kavu ni meza hiyo waliitumia kujenga nyumba kwenye minazi minne iliyokaribiana

Alipokwenda kuwinda akiwa anaburuza windo lake (mbuni) Kurudi nyumbani akashtukia windo limeshamezwa na mamba mwili mzima mpaka shingo aliyoshika

Akatoka nduki kufika nyumbani mke hayupo katika kumsaka ndio akakutana na kabila la wagagagigikoko chini ya mfalme huihui.

Akaishi na watu hao, siku moja mvua kubwa ikanyesha mwamba wa ukuta wa nyumba ukapasuka pesa nyingi sana zikamwagika toka ukutani akafurahi akapakia magunia kwa magunia

Hapa ni mwisho wa story kwa dondoo lakini alirudi kwao

nYaNi wA KaLe
 
Sawa kabisa. Ila SIYO HADITHI yangu. Nasimulia tu kile nilichokisoma (Kwenye Kitabu cha safari za Bulicheka nikiwa Darasa la 3).
Inaendela hivi....Baada ya Huihui kukubali kupigana, Bulicheka akamshinda Mfalme Huihui. Wananchi walifurahi maana Hui hui alikuwa hapendwi (inawezekana kabisa alikuwa Kiongozi dikiteta). Wakamfurahia Bulicheka. Kulikuwa na sherehe kubwa sana siku ya kumtawaza Ufalme. Elizabeth akawa Malkia. Basi Bulicheka akatawala vizuri na watu walimpenda. Aliwa fundisha mabo mengi, kama namna bora ya kutengeneza Mashua, kulima na kuhifadhi chakula nk. Ikatokea siku moja Meli toka Bara ilipita pale. Ikawa inaelekea Dar es Salaam. Akaomba KUKABIDHI NCHI. Akawaga wananchi wake. AKARUDI KWAO...na hapo ndipo hadithi iliposihia.
Una kumbukumbu nzuri, hiki kipande cha kupigana nilisahau

Kiufupi ni hadithi nzuri

nYaNi wA KaLe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom