Wafungwa wa ngono ISIS wazuiwa kushika mimba

Status
Not open for further replies.

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la New York Times, umetambua kuwa kundi la wapiganaji la Islamic State, linalowashikilia wanawake kutoka jamii ya Yazidi sasa linawapa wafungwa hao wa ngono vifaa vya kuwazuia kushika mimba-- ili kuendelea kutumika na wanamgambo hao.

Gazeti hilo lililowahoji zaidi ya wanawake 35 kutoka kwa jamii hiyo ndogo ya Yazidi, waliokimbia maafa ya wanamgambo wenye itikadi kali nchini Iraq linasema kuwa dawa za kupanga uzazi za kumeza pamoja na za kudungwa zimekuwa zikitumika.

Aidha, ripoti za wanawake kuavya mimba pia ziliripotiwa.
Kundi la IS, limekiri kuwatumia wanawake hao kama watumwa kingono.

Kundi la IS, limekiri kuwatumia wanawake hao kama watumwa kingono.

Kumekuwa na madai ya ubakaji wa wanawake na wasichana wa Yazidi kwa muda mrefu, huku wakitumia dhana wanayosema kuwa, unaweza kumbaka mwanamke mradi hashiki mimba.
 
Duu kuwapa "Contraceptives" maana yake condom hawatumii hao ISIS, je HIV watazuiaje? Poleni sana wanawake mliotekwa
 
Duu kuwapa "Contraceptives" maana yake condom hawatumii hao ISIS, je HIV watazuiaje? Poleni sana wanawake mliotekwa
watu wanaojifanya eti wanapinga itikadi na life style za magharibi wanatumia contraceptives, kitu ambacho ni cha ki magharibi
 
Watakuwa wanatumia, lakini mafundisho ya Dini wanayoyaamini ni zaidi ya Mihadharati.
Hawa hawafuati mafunzo yoyote ya dini ,yote wanaofanya ni kinyume na dini.Na pia jambo la kujiuliza
Dawa za kuzuia mimba wanazioata wapi
Na kwa nini hao wanawake wasitumike kuelekeza hawa wanamgombo waliko ,ili kuwamaliza?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom