Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Kwenye rangi kuna variations mkuu
Afadhali umesema!! Kuna watu walishakaririshwa rangi!! wakiona rangi nyingine wanadai siyo pure ni cross!! Tazama hawa hapa:
1694713622546.png

Hawa ni wale wenye manyoya marefu. Ila kuna aina ya GS pia wana manyoya mafupi (short hair GS). Kuna mwingine akiona manyoya mafupi anadai siyo pure ni cross!! Hata hivyo GS kuwa cross kunaweza kuwa faida zaidi kuliko pure, inategemea amecross na breed ipi!! Cross ya GS na BS ni madini yanayopumua!! Na bei yake ni kubwa kuliko pure GS au BS!!
 
mkuu unao pure?
Pure GS hawako agressive kivile, wanashambulia kwa amri au wakihisi wanatishiwa usalama wao. Ila ni walinzi wazuri, hawawezi kuruhusu mtu afanye tresspassing maeneo yao. Belgian shepherd ndo wakali zaidi. Sasa cross ya GS na BS inatoa breed iliyochanganya akili kubwa ya GS na nguvu+ukali wa BS.
 
Mi nafunga mbwa wa kiswahili na wako vzr Sana,kiulinzi ata adabu pia.nawapa huduma zote stahiki ikiwa chakula,chanjo zote,na kuoga kira jpili.kiukweli ulinzi tosha..
Ni hivi: Mbwa wa kienyeji bila matunzo = mbwa koko!!, Lakini mbwa wa kienyeji pamoja na matunzo stahiki = Local breed!!
 
German Shepherd bora sio lazima awe tan and black kama unavyodai, in fact German shepherd wa kwanza hakuwa na rangi hiyo alikuwa sable.

Nchi za wenzetu wanapenda tan and black au red and black color kwa ajili ya show line competition, kwa ajili ya ulinzi unaweza pick rangi nyingine, colour haimfanyi mbwa akawa mbegu mbaya.

German Shepherd wanaweza kuja na rangi kadhaa isipokuwa ikitokea akawa white au blue izo rangi zinkuwa considered fault.
German shepherd wapo wa rangi mbali mbali hata wenye rangi nyeupe tupu!! Mcheki huyu hapa:
1694716267211.png

GS ni jamii ya mbwa. Kwenye jkamii hii kuna tofauti kati ya mbwa na mbwa na wanaunganishwa na 1,. Akili kubwa (inaaminika hadi sasa GS ni breed yyenye akili kuliko breed zingine zote, wana uwezo mkubwa wa kufundishika na wako royal). 2. Miguu ya mbele kuonekana mirefu kidogo kuliko ya nyuma (hii ni kwasababu ile ya nyuma imepinda kidogo). Sifa zingine kama kusimama na kuchezesha masikio, hata baadhi ya breed zingine zinavsifa kama hiyo!!
o
 
@steven nguma hao wako naona ni cross breed ya gs
Unawaonaje? Tatizo lako wewe umekariri rangi fulani tu!! Ukweli ni kwamba huwezi kumtambua pure GS kwa UHAKIKA kuwa CROSS breed, vinginevyo utuambie kuwa macho yako yanaweza kuviona vinasaba(genes).Kijijini kwetu waarabu walihamia miaka mingi iliyoita na wakfanya cross na waafrika. Baadhi ya hizi cross wengine kwa macho wanaonekana kuwa ni pure waarabu (lakini ni cross) na wengine wanaonekana kwa macho kama pure waafrika (lakini ni cross), na wengine wanaonekana kwa macho kuwa ni mchanganyiko wa mwarabu na mwafrika (tunawaita MASHOMBE)!!

Sasa huyu cross wa kiarabu anayeonekana kwa macho kama pure mwarabu, akioana na pure mwarabu, au cross mwarabu anayeonekana mwarabu kwa macho, watakapopata watoto ndo siri inaweza kufumuka kwa kuangalia watoto wao!! baadhi ya watoto watatokea kuwa ni mchanganyiko(cross!), tunawaita "MASHOMBE", wengine wataonekana waafrika kabisa na wengine wataonekana ni waarabu kabisa!.

Hali kadhalika kwa mbwa!! Ndiyo maana kama unatafuta mbwa wa ulinzi, unaweza kuchukua yeyote hata kama ni cross maana mwonekano wake na sifa zake zilizo nyingi zinafanana kabisa na za Pure GS. Tatizo linakuja kama unatafuta mbwa ili uzalishe kwa ajili ya biashara!! Kama mbwa alikuwa ni cross, baadhi ya watoto wake watadhihirisha kabisa kuwa siyo pure breed ya GS, na hapo utapata hasara! Kama unatafuta kwa ajili ya kuzalisha ni vizuri ukajiridhisha kuhusu wazazi wa mbwa huyo angalau vizazi viwili nyuma!! Wafugaji wazuri huwa wanatunza historia ya mbwa kwenye kadi!! NARUDIA: Cross anaweza kufanana na pure kimwonekano asilimia mia moja, (Phenotypically similar, but genotypically different!), na huwezi kumtambua kwa macho, itabidi usubiri hadi uje uone uzao wake!! Mtu akidai kuwa atamtambua huyo ni mwongo na hana uelewa hata kidogo tu wa GENETICS!!
Mfano mwingine: Kuna mtu anaweza kuwa ni cross wa albino lakini huwezi kumtambua kwa macho!! Hana hata dalili kidogo za kuonekana kwa macho kuwa ni cross wa albino!! Huyu mtu akioana na mtu mwingine ambaye pia ni cross wa albino (naye huwezi kumtambua kwa macho), watoto wao baadhi watakuwa ni pure albino na hapo ndipo utakapojua kuwa kumbe wazazi walikuwa ni cross ya albino!!

Genetics ya watu inafanana na ile ya mbwa!! Mtu akidai anaweza kumtambua kila cross wa GS kwa macho tu, maana yake anauwezo wa kuviona vinasaba(genes) kwa macho!! Huo ni utapeli!!
 
Bado sijaona mbwa wazuri kama

Germany Shepherd
Gray wolf
Belgian Tervuren
Hii inategemea na mahitaji yako kwa mbwa!! Kuna vwatu wanafuga mbwa si kwa ajili ya ulinzi bali nkwa ajili ya mapambo!! Kwa hiyo hao ni wazuri kwako kwa mujibu wa mahitaji yako!! Lakini kwa mwingine angependa mbwa mzuri atakayekuwa anaweza kumbeba beba! Sasa utabeba beba GS?
 
Hivi vile vimbwa vya urembo huwa vinapiga hata kelele kweli endapo mwizi ameingia au mgeni wasiemjua?
 
RW hata akiwa trained nae ni kama anaprinciple zake flani hivi, ila hili chiz Pitbull hata sio lakuliamini swala la obedience kwake ni pata potea. GS ni wewe tu utavyotaka awe.
Uongoo
Mwal wa mathe hii ni uongoo

Nakuletea ka mbwa koko kamoja ukatrain basi kawe ka kishua shua.
 
Caucasian shepherd, Anatolian shepherd, Central Asian shepherd(alabai), turkish malakli

mmoja kati ya hao...

naulizia tu, sio kwamba nataka kununua saivi
Mkuu bongo kuna mpaka tibetan mastiff.
Hao Kangal na Caucasian wapo toka 2017 kipindi icho namimi nafuga.

Yupo mtu mmoja anaitwa Nuhu, yuko Kigamboni. Ana page instagram nadhani ..! yupo yule Ras Arusha alabai anao.

Bongo kuna breed nyingi sana, watu wamedare kweli, wale St bernard na jamii nyingi za large breed zipo mkuu.


Sent from my SM-G970U1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom