Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

belgian laekenois
Screenshot_20181005-234242.jpeg
 
Mie nafugaga hii mijibwa ya uswazi (koko)
Yenyewe hayana gharama ya misosi maana yanakula chochote yanachokiona hata mavi ya walevi.!
Halafu wakiwa wengi huwa tunaua kisha tunawachuna na kuwapelekea wauza supu wa bar wao huchanganya na nyama ya mbuzi ili kuleta kale kaharufu ka kimbuzimbuzi kisha hupikwa supu na kuuziwa wateja.
Aisee mkuu umetisha
 
Unaua ndugu zako?
 
Ngoja niwape kisa kilimtokea family friend mmoja mwaka 2015 msimu wa xmass na mwaka mpya.

Jamaa alikuwa na GS wako nane. Kawaida huwapa msosi kila siku usiku mida ya saa 4 baada ya watu wote kuingia ndani maana ni wakali mno. Na zoezi la chakula kuna shamba boy huwa ndie anawahudumia mbwa.

Sasa shamba boy xmass alienda kwao kula sikukuu. Na family friend yeye ni mtu wa tungi sana huwa anakesha baa na wajomba zangu.

Siku shamba boy alipoondoka jamaa akawa amelewa zake akarudi home akapitiwa akalala (mbwa hawakupewa chakula kama kawaida).

Akaamka asubuhi akaandaa msosi vizuri akafungulia banda la kwanza. (Amewagawa katika mabanda mawili wanne wanne).

Baada ya kufungua banda la kwanza mbwa mmoja akaanza kumkoromea kwa hasira sana kisha akamrudia, wale wengine watatu nao wakamrukia wakaanza kumrarua kwa hasira, wale wengine ndani nao wakapandwa na wazimu mpaka wakavunja banda wakaungana na wenzao.

Mke wa jamaa ni mayowe tu kwa dirishani anashuhudia mumuwe anavyotafunwa bila kuwa na lakufanya. Watoto vilio mpaka majirani wakasogea karibu.

Bahati nzuri kuna mtoto wa jirani ni rafiki wa shamba boy na mara nyingi wakiwa wanalisha mbwa wanakuwa wote hivyo wale mbwa wamemzoea sana.

Basi dogo ndio kuingia pale akawatuliza mbwa na jamaa kukimbizwa hospital ambapo alilazwa miezi mitatu akiwa hana fahamu.

Kusema ukweli yule jamaa kama angekuwa kapuku wala asingepona kwa shambulio lile. Pesa ilimuokoa.

Baada ya kurudi uraiani alikuwa amefungwa POP miguuni wala kutembea bila magongo hawezi. Aliwatandika risasi mbwa wote na mpaka sasa sijui kama anafuga tena.

Mbwa ni Loyal Friend kuliko hata binadamu lakini ni hatari sana pia.

Wafugaji tuzingatie Terms and Conditions

Ngoja niwape kisa kilimtokea family friend mmoja mwaka 2015 msimu wa xmass na mwaka mpya.

Jamaa alikuwa GS wako nane. Kawaida huwapa msosi kila siku usiku mida ya saa 4 baada ya watu wote kuingia ndani maana ni wakali mno. Na zoezi la chakula kuna shamba boy huwa ndie anawahudumia mbwa.

Sasa shamba boy xmass alienda kwao kula sikukuu. Na family friend yeye ni mtu wa tungi sana huwa anakesha baa na wajomba zangu.

Siku shamba boy alipoondoka jamaa akawa amelewa zake akarudi home akapitiwa akalala (mbwa hawakupewa chakula kama kawaida).

Akaamka asubuhi akaandaa msosi vizuri akafungulia banda la kwanza. (Amewagawa katika mabanda mawili wanne wanne).

Baada ya kufungua banda la kwanza mbwa mmoja akaanza kumkoromea kwa hasira sana kisha akamrudia, wale wengine watatu nao wakamrukia wakaanza kumrarua kwa hasira, wale wengine ndani nao wakapandwa na wazimu mpaka wakavunja banda wakaungana na wenzao.

Mke wa jamaa ni mayowe tu kwa dirishani anashuhudia mumuwe anavyotafunwa bila kuwa na lakufanya. Watoto vilio mpaka majirani wakasogea karibu.

Bahati nzuri kuna mtoto wa jirani ni rafiki wa shamba boy na mara nyingi wakiwa wanalisha mbwa wanakuwa wote hivyo wale mbwa wamemzoea sana.

Basi dogo ndio kuingia pale akawatuliza mbwa na jamaa kukimbizwa hospital ambapo alilazwa miezi mitatu akiwa hana fahamu.

Kusema ukweli yule jamaa kama angekuwa kapuku wala asingepona kwa shambulio lile. Pesa ilimuokoa.

Baada ya kurudi uraiani alikuwa amefungwa POP miguuni wala kutembea bila magongo hawezi. Aliwatandika risasi mbwa wote na mpaka sasa sijui kama anafuga tena.

Mbwa ni Loyal Friend kuliko hata binadamu lakini ni hatari sana pia.

Wafugaji tuzingatie Terms and Conditions

ya Kingunge haya
 
Wakuu fugeni ng'ombe mpate kula nyama na masiwa
ni kweli mkuu lkn hatuwezi kufuga ng'ombe wote au mbwa.
ufugaji wa ng'ombe ni mgumu sana hasa mjini utawalisha nini?
ili uwafuge unahitaji shamba la majani, mjini wote twaweza kumiliki shamba? sio kiwanja.
lkn mbwa ni mita chache za banda waweza kufuga 2 na wana faida kama ifuatavyo;
1. mbwa aweza kuzaa mara 2 kwa mwaka
na kila uzao watoto 5 na kuendelea so
kwa mwaka 10@700,000=7, 000,000
2. wanauzwa wakiwa na miezi 2

ng'ombe anabeba mimba miezi 9
1.ndama ukimuuza akiwa na miezi 3 ni 300k
2. maziwa ukikamua lita 5 kwa siku
5@1,000 x30=150kx12=1,800,000
jumlisha na ndama
300k+1,800,000=2.1ml

haya nipe majibu kipi bora kufuga kibiashara?
 
Back
Top Bottom