Wafuatao, wanaweza kuvivaa viatu vya Magufuli na vikawaenea

Maoni Yako yanaheshimiwa.

Ingawa Mimi nijuavyo, kunguni au kupe Huwa habagui, hachagui, kwake Damu ndo kitu muhimu.

Akipenya yeyote kati ya hao, lazima utaendeleza mapambio.
This is 2023 ,wewe mada inasema 2000.

Wapenye wapi Sasa?
 
Philip Mpango hafai, hii nchi haitaki kuongozwa na watu wa namna yake, ni mpole mno.

LISSU ni mwanaharakati, hafai kuwa raisi.

GWAJIMA hafai hata kidogo, kwanza umetumia vigezo gani kumuweka hapo?

KASSIM✅️
Huyo uliyemuwekea tick, naye hafai isipokuwa anao unafuu ukilinganisha na waliotajwa au waliopo ndani ya chama chake.

Kuna wengi walionesha uwezo wa kitendaji chini ya usimamizi wa MWAMBA, Kassim akiwa mmoja wao!

Ili nchi ya kiafrika itoke kwenye dimbi la umasikini, ni lazima UKATILI WA KIMAENDELEO uanzie kwenye serikali kwenda kwa wananchi.

Watake watafanya, wasitake watafanya...kila anayepumua ndani ya nchi atainamishwa!
  • Sio kuna wenye kulipa kodi na wenye kusamehewa kodi
  • Sio kuna wenye kupita barabara za kurudi na wenye kutembelea LC 300
  • Sio kuna wenye kuazibiwa kwa wizi wa kuku, miaka 100 jela na wenye kurudisha mzigo au kuhamisha idara/kituo cha kazi kama adhabu ya ubadhirifu

Magu hakuwa mwana-ccm aliyeivishwa na chama, alikuwa mwananchi aliyelelewa kitaa, akasimamia imani yake ya KIUME bila kujali usasa wa wanaharakati.

Wanaume wavaa vimodo, vinjunga, dont touch, cheni, hereni; wanaojadiliana na -ke jinsi ya kuleta usawa wa kijinsia.

MAGU ni ishara wazi tuliyopewa ili tujue ni muelekeo gani utatutoa tulipo, kwenda mbele!
 
Salaam, Shalom!!

Nimefanya Utafiti mdogo na kufanikiwa kupata kujua size ya viatu vya mzalendo na mchapakazi Magufuli.

Viatu hivyo vimenakshiwa na sifa ZIFUATAZO,

1. UTHUBUTU& MSIMAMO THABITI.

2. UZALENDO.

3. UCHAPAKAZI.

4. MAONO.

Wafuatao, Wana sifa hizo hapo juu ingawa Si zote, lakini angalau wanaweza kuvivaa viatu hivyo na kuongoza njia.

1. KASSIM MAJALIWA

2. PHILIP MPANGO.

3. TUNDU ANTIPAS LISSU.

4. JOSEPHAT GWAJIMA.

Na Kwa uchache, mmoja kati ya hao, atapenya ya na kutuongoza kufika Nchi ya AHADI kuanzia mwaka 2020V,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni🙏

Mkuu ni kwamba huyo JPM ndio SU Unit ya urais hapa nchini ama?
 
1. Bashiru Ally Kakurwa
2. Humphrey Polepole
3. Abel Makubi
4. Luhaga Mpina
5. Kassim Majaliwa
6. Philip Mpango
Kassim Majaliwa na Philip Mpango wamo tayari kwenye list muhimu, top 4.

Tusubiri.
 
We kwl bwege, viatu vya JPM nani anataka kuvivaa? Yule shetani alituharibia nchi yetu. Mama ndio anaiponya kwa kutumia 4Rs. Usitukumbushe ushetani wa yule mfu wenu. Mungu fundi ameamua ugomvi tumshukuru Mungu.
Ushetani haujadiliwi hapa. Sifa ni nne zimeainishwa hapo juu. 1.Uzalendo, 2. Maono, 3. Uchapakazi, 3.Uthubutu.

Anyway, mawazo na maoni Yako yaheshimiwe.
 
Back
Top Bottom