Wafuasi wa Uamsho waiamsha Zanzibar.........endelea kuona picha hizo

320343_10151056245136176_383623134_n.jpg


Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, Yussuf Ilembo na Amir wa Uamsho Sheikh Msellem Bin Ally wakiwa katika kikao cha pamoja wakitoa taarifa kwa vyomvo vya habari kuzungumzia hali ya utata wa kupotea kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed alivyotoweka na vurugu zilizochukua siku ya pili mfululizo na athari zake.
 
149672_10151055694736176_441273276_n.jpg


Eneo la Darajani likionekana limeharibika. Taarifa kamili kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Farid zitatolewa mchana wa leo na taasisi za kiislamu baada ya kumaliza kikao chao cha pamoja. Tunaombwa tuwe na subra na kuendelea kudumisha amani
 
404356_10151055675211176_1131161802_n.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed akitoa taarifa kwa umma kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti hali ya ulinzi na imeimarishwa katika maeneo yote ya Zanzibar
 
644096_10151054792581176_2075433788_n.jpg



Maskani ya Kisonge inavyoonekana muda mfupi baada ya kuzimwa moto na kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) uliowachwa na vijana waliopita na kutembea katika maeneo ya Mjini. Awali Sheikh Farid inasemekana hajulikani alipo na ndipo watu wakaanza kujikusanya. Si busara hata kidogo kuchokozwa mkachokozeka wakati huu ambao wazanzibari wanatakiwa kuwa kitu kimoja na kushirikiana na serikali yao ili kufikia lengo lililokusudiwa. Ni kweli wakati mwenye vitendo vinafanywa kwa makusudi lakini jee kuchoma moto, kupiga watu, kuharibu vitu vya watu na kupita na silaha mitaani ndio mtaweza kumuona mnayemtafuta? Tafakari
 
561552_10151050819506176_1237573833_n.jpg

Asalamu Alaykum leo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanatarajiwa kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Katiba. Tunawatakia kila la kheri wajumbe wetu kwani hatima ya wazanzibari ipo mikononi mwao tuwaombee tawifk na ujasiri wale wote ambao ni watetezi wa Zanzibar ili watufikishe pale wazanzibari wanapotaka kwenda inshallah. Fuatana nami nikiwa barazani
 
253137_10151049711841176_1055702300_n.jpg

Zanzibar Fighting Against Youth Challenges Organization (ZAFAYCO) wanapewa mafunzo ya siku mbili juu ya haki na wajibu kwa Vijana katika ukumbi wa Bwawani. Karibuni
 
292832_10151049101466176_1707344336_n.jpg



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi na Wavuvi wa Kijiji cha Chwaka. Sasa hivi anaoneshwa ZBC akifanyiwa mahojiano kuhusu masuala mbali mbali anasema yeye ni mzanzibari halisi fuatana nami:
- withbalozi wa tanganyika nchini zanzibar and msaidizi wa balozi mkaazi zanzibar.
 
523891_10151048808236176_1605648592_n.jpg

Wakati juzi kitendo cha kukojolea Quraan Tukufu kikifanyika huko Pemba na kijana Farid Abdallah Farid ambapo alifikishwa mahakamani, leo kitendo kama hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam baada ya kijana mmoja wa miaka 14 kukojolea Msahafu na kusababisha hamasa kwa waumini wa dini ya kiilamu kuandamana na kulaani kitendo hicho.
 
66379_10151047799086176_778314298_n.jpg


'Hongera sana bwana nasikia vitu vyako' ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum, Mansoor Yussuf Himid huko Fumba, wakati wa uzinduzi wa waya wa umeme wa megawati 100
 
208081_10151047783131176_200516728_n.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea Ripoti ya Tume ya kuzama kwa meli ya Mv SKAGIT,kutoka Mwenyekiti wa Tume kuchunguza ajali ya meli hiyo Jaji Abdulhakim Ameir Issa, Ikulu Mjini Zanzibar leo.
 
554403_10151047396191176_2131101431_n.jpg


wajumbe wa wa baraza la wawakilishi wa CCM walipokuwa wakisherehekea ushindi wa chama chao wakiwa wa kiapo cha mwakilishi wa jimo la Bububu Hussein Ibrahim Makungu jana katika kikao cha baraza hilo, nyimbo ya kuisifu CCM ilikwenda sambamba na happy birthday kwa kuwa Hussein ilikuwa ndio siku yake ya kuzaliwa
 
550660_10151047391021176_1323563829_n.jpg
,,
Mwakilishi mpya wa jimbo la Bububu aliyeapishwa sana akiwa na familia yake muda mfupi baada ya kuapishwa hapo jana barazani ambapo wawakilishi wa CUF wote walioka nje wakipinga kiapo hicho wakiamini kwamba ushindi wake haukuwa halali kutokana na uchaguzi haukuwa wa haki kutokana na fujo na rafu siku ya upigaji kura
 
73945_10151046865121176_90699857_n.jpg


Nami naungana na waumini wenzangu kumuombea dua hii mwalimu wangu Sheikh Nassor Bachu. Yarabbi Mola wangu mpe tahfif katika mtihani wake wa maradhi na apate nafuu kwa uwezo wako ya Jalali. Sheikh Nassor amerejeshwa tena hospitali na tunaambiwa yupo ICU kwa hivyo tunakuombeni dua zenu
 
644624_10151046835701176_49055434_n.jpg

Jumla ya wanafunzi 800 wa Zanzibar, watafaidika na ufadhili wa masomo ya Elimu ya Juu Kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Zanzíbar kwa mwaka wa masomo 2012-2013

Katika Mkopo huo wanafunzi 758 watakuwa wanasomea masomo ya Shahada ya kwanza, wanafunzi 40 Shahada ya Pili na Wanafunzi wawili wa masomo ya Shahada ya Tatu kutoka katika vyuo vilivyopo nchini Tanziania.
 
Back
Top Bottom