Wafuasi wa Uamsho waiamsha Zanzibar.........endelea kuona picha hizo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafuasi wa Uamsho waiamsha Zanzibar.........endelea kuona picha hizo

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Oct 18, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Kutofahamika wapi yuko Sheikh Farid na yupo katika hali gani ni jambo la hatari; lakini kufanya vitendo vitakavyopelekea kupotea kwa UMOJA na AMANI ya nchi yetu ni jambo lililo hatari zaidi. Farid ni kiongozi wa watu, ni raia halali wa Zanzibar, na ni binaadamu anaestahili kupata haki zote za ubinaadamu. Kutoweka katika mazingira yasiyofahamika hadi dakika hii ni jambo linalokwenda kinyume na misingi ya haki za binaadamu, na ni jambo linalokwenda kinyume na Katiba yetu ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010 maana Katiba yetu katika SURA YA TATU, Kinga ya Haki za Lazima, Wajibu na Uhuru wa Mtu Binafsi inaeleza: "

  11. (1) Binaadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.
  (2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

  12. (1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wo wote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
  (5) Katika kifungu hiki neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja kwa watu mbali mbali kwa kutegemea utaifa wao, kabila, jinsia, ulemavu, pahala walipotokea, muelekeo wao wa kisiasa, rangi au dini ambapo watu wa aina fulani wanaonekana kuwa ni dhaifu na duni au wawekewe vikwazo na pingamizi ambayo wale watu wa aina nyengine hawawekeani au wanapewa fursa au faida ambayo hawapewi watu wa aina nyengine.

  13. (1) Kila mtu anayo haki ya kuwa na hifadhi ya maisha yake
  (2) Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria.
  (3) Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.

  14. (1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru.
  (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa
  uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yo yote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vyenginevyo isipokuwa tu:

  (a)katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria; au
  (b)katika kutekeleza hukumu, amri, au adhabu iliyotolewa na Mahkama kutokana na shauri au kosa la jinai ambalo mtu amekutwa na hatia ya kulitenda.

  Kwa msingi huo, Serikali, vyombo vyake vyote na wananchi kwa ujumla – tuna wajibu wa kulinda haki ya uhai, usawa na uhuru wa Farid na kufuatilia kujua haki ya usalama wa kiongozi huyu ambae anawakilisha Jumuiya halali na iliyosajiliwa kisheria.
  Pamoja na ukweli huo, bado AMANI ni jambo muhimu sana kwetu sisi WOTE na kwamba sote kwa ujumla wetu tuna wajibu wa kumtafuta kiongozi huyu kwa kupitia utaratibu wa AMANI na DEMOKRASIA (peaceful and democratic means) maana furaha yetu ya kibinaadamu, maendeleo yetu ya uchumi na ya maisha kwa jumla, yote yanategemea kuwepo kwa AMANI. Lakini pia ifahamike kuwa, AMANI na HAKI ya binaadamu ni vitu viwili vinavyoambatana. Kwa hiyo, katika jitihada zetu kwa umoja wetu za kutafuta na kudumisha AMANI; lazima vile vile tuwekeze katika jitihada za kutafuta na kudumisha HAKI na HAKI ionekane ikitendeka.

  Hata hivyo, kwa kuwa Serikali imetoa tamko kupitia Waziri wake Mh. Mohamed Aboud kwamba imewasiliana na vyombo vya Dola ikiwemo Polisi, Jeshi la Wananchi, Idara ya Usalama wa Taifa, Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuanzia KMKM, JKU, Chuo cha Mafunzo, Zimamoto na Valantia ambapo vyombo vyote kwa pamoja vimeeleza na kudai kutoelewa wala kuhusika na cho chote kuhusu tukio hili la kutisha na lililojaa utata, na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta na kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ili kupata ukweli wake na kuchukua hatua zinazofaa – ni busara kwa wanafamilia, wapenzi, wafuasi wa kiongozi huyu na Wazanzibari kwa ujumla tukawa wastahmilivu na kushirikiana kujua nini hasa kilichojiri na/au kumsibu kiongozi huyu.

  Halikadhalika, utakuwa ni uamuzi wa maana sana endapo hatutalihusisha tukio hili na masuala ya Kidini wala Chama wala Serikali mpaka pale tu itakapoeleweka na/au kuthibitika vyenginevyo. Pamoja na kwamba Sheikh Farid ni kiongozi wa juu wa Taasisi/Jumuiya ya Kiislamu – lakini Uislamu unasimama juu ya misingi ya ushahidi na dalili. Aidha, kulihusisha tukio hili na masuala ya tofauti za imani za Kidini au misimamo ya Serikali au Vyama vya Siasa kwa ‘sasa' ambapo bado hakujawa na ushahidi - ni kwenda kinyume na misingi ya Uislamu kwa vile Qur' an inaeleza kwenye SURA YA 5 (AL MA'IDAH) kwamba:

  "Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda". (Aya nambari 8).

  Mwito wetu kwa Wazanzibari, ni muhimu sana kuimarisha Umoja wetu wa Pamoja, kudumisha Amani na utulivu ndani ya nchi yetu na kwamba harakati zote za kumtafuta Sheikh Farid ziendelee na kuendelezwa na Wazanzibari wote kwa ajili ya kuthamini haki ya maisha ya mwenzetu na udugu miongoni mwetu.

  Pia, tusikubali kutumiliwa na maadui wa Zanzibar na wa Wazanzibari kwa kutumika kwa njia yo yote inayoweza kuhujumu harakati zetu za kudai mamlaka na madaraka kamili ya Zanzibar kitaifa na kimataifa na kwamba kwa Umoja wetu wa Pamoja – tunayalinda Maridhiano ya Wazanzibari na Serikali yetu ya Umoja wa Kitaifa na kwamba kupitia Umoja wa Pamoja uliopo Zanzibar – shabaha yetu ya kuwa na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar iliyo huru ndani na nje na kufuatiwa na mfumo mpya wa mahusiano ya Mkataba na Tanganyika na kwengineko inabakia pale pale na kuendelezwa kwa njia za amani na za kidemokrasia.

  Mungu mlinde na mhifadhi Sheikh Farid na kila balaa na belwa, hasada na mahasidi na lifumbue fumbo hili tujue kilichojiri.

  Mungu ibariki Zanzibar.
  Mungu wabariki Wazanzibari.

  Jamhuri ya Watu wa Zanzibar – KWANZA !


  NA KHALID GWIJI  [​IMG]
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Haaaaaaaa uamsho wasubiri kibano tu kesho
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mtoto apigwa na bomu la Machozi lilimpasua mguu maeneo ya Darajani.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 12. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  hawa ******* wanataka kutuona tulio tulia machizi kwa maana mpaka sasa bado sijajua madai yao hasa ni nin?? Mara wachome moto makanisa mara sijui wawajeruhi polisi mara watanganyika hawatakiwi zanzibar. Sasa sijui tuwaelewe vipi lakini hakuna la kupoteza na wala hatuja chelewa sana dawa yao ni wanajeshi tuu ni mwendo wa risasi za moto kwa kwenda mbele. Ni kuwadungua tu kama popo
   
 13. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwani wafikiri katika majeshi hamna uamsho! wamo kibao ndio maana ukaona zoezi la kuwatumia JWTZ ni gumu kidogo
  angalia afghanistan, majeshi wa afgan wakiwa kazini wanauwa raia wao, wakibaki na wamarekani wanawageuzia kibao
  nao pia wanawauwa hapwendu mtu hapo....
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hii picha bwana umedanganya umma. This picture has been on internet for about three if not four days. Leo inaletwa hapa upya unasema eti ya uamsho acha mbwembwe wewe!! unataka kumtisha nani?
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  News Updates.

  Hali ya visiwani sio shuari kabisa kama alivyosema kamishna wa jeshi la Police mussa...tusifanye mchezo wa kitoto hili suala lazima serikali

  itambue kua kutoonekana kwa amir farid hali itazidi kuwa mbaya usalama unaonekana kuwa mdogo sana imani ina nguvu zaid mjue kuliko siasa

  kama mnaona ni masihara angalieni nchi mnapoipeleka!! Kiongozi mkubwa anapotoweka ktk mazingira ya kutatanisha kiaina hivyo mnategemea

  nini na matamko mbali mbali yalikua yakisikika kutoka kwa viongozi wa serikali na wa chama cha ccm juu ya viongozi hawa wa jumuiya hizi sasa

  leo limetokea hili baada ya kauli zenu na vitendo vyenu ambavyo mnatumilia jeshi la polisi kuanzisa fujo zisizo na msingi kwa wananchi leo

  mtawaambia nini wakueleweni??? Tufikiri huu sio usalama kama tunavyoambiwa hakuna anaekaa kwenye hekalu au kambini tunaishi nao humu

  humu mitaani hivyo amani,utulivu unahitajika kwa haraka: Chanzo:
  https://www.facebook.com/
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 17. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  Dhaifu nchi imemshinda...ingekuwa mkapa au NYERERE hapa ungeona N NEW MOVIE,,,,,,,,,,,,
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Michenzani Zanzibar..................
   
 19. A

  Amri kuu ni Upendo JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 310
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ...inatisha!!
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  Kweli kuna taarifa kuwa Farid Hadi ambae ni Amir wa Jumuiya ya Maimamu, Zanzibar hajaonekana tokea usiku wa jana, na hadi sasa hajulikani alipo. Pamoja na taarifa hizo, ni vyema zaidi.
   
Loading...