GE2025 Wafuasi wa Chadema hawajui wanapoelekea

GE2025 Wafuasi wa Chadema hawajui wanapoelekea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
54,015
Reaction score
43,157
Wanaukumbi.

Tumebakiwa na miezi miwili tuingie kwenye Uchaguzi Mkuu. Bahati mbaya au nzuri Wafuasi wa Chadema hawajui wanapoelekea sasa hivi wamepanda basi la CCM ambalo hawajui linapoelekea mfano tunaona walivyojaa kwenye mfumo wa CCM.

Nyuzi nyingi za uchaguzi wa CCM hapa JF zinafunguliwa na Pro- Chadema
Inafurahisha sana wafuasi wa Chadema wanapeana faraja kuliwazana kuwa CCM inatasambaratika huko Dodoma kwenye uchaguzi wao kuwa hawamtaki Rais Samia, ukiwauliza mbadala wa CCM nani wanasema Polepole.

Wameishamsahu Kamanda Tundu Lissu. Sasa hivi wamejikita kufuatilia mkutana wa CCM na wanataka Rais Samia asichaguliwe yaani wanawapangia CCM namna ya kuendesha uchaguzi wao ni kituko.

Hamna tena No reforms no election sababu wameishapanda basi la CCM hawajui linaenda wapi.

Ushauri wangu kwa Makamanda huu muda uliobaki ni mchache msiutumie kuandamana humu JF na IDs feki, kila mmoja anatakiwa kuaiga familia yake kuwa naenda kwenye mapambano kuikoa Chadema kuzuia Uchaguzi Mkuu naingia barabarani No reforms no election.

Kuna mawili naweza kurudi au nisirudi hii ndiyo njia muhimu kwenu ya kumuenzi Tundu Lissu. Sasa hivi Polepole anaonekana shujaa kwa wafuasi wa Chadema kuzidi Lissu na Heche daaah.
 
Uchaguzi upi tena.....

IMG-20250726-WA0108.jpg
 
Sio kusariti neno sahihi ni kusaliti.

Hatimae urais nao umekuwa wa viti maalum, mama anapiga mwingi.
Kwa hiyo mmesaliti Tundu Lissu.

Hamna tena No reforms no election tupo Dodoma😀

Cha kufuraisha wanaolalamikia uchaguzi wa CCM ni wafuasi wa Chadema.

Huwenda una umri mdogo CCM huo utaratibu viti Maalum alianzia kwa Nyerere, Mwinyi. Mkapa😀
 
Hakuna chenye mwanzo kikakosa mwisho na amini mwisho wenu utakuja kuwa mbaya sana mda utaongea tuombe uzima
 
CDM Ni dude kubwa..Hadi Mwenyekiti yupo ndani (Ili sa100 apite bila kupingwa_ hii Ni aibu y Karne, Na historia utanikumbuka kuwa ndiye Rais pekee baada YA mfumo Wa vyama vingi ambaye aliteuliwa Na tume na kupita bila kupingwa

Kama CCM Ni wanaume twendeni Kati kwenye mfumo Ulio bora
 
Hakuna chenye mwanzo kikakosa mwisho na amini mwisho wenu utakuja kuwa mbaya sana mda utaongea tuombe uzima
Kamanda gani unalia lia unatia huruma ingia barabarani No reforms no election zuia uchaguzi.
 
CDM Ni dude kubwa..Hadi Mwenyekiti yupo ndani (Ili sa100 apite bila kupingwa_ hii Ni aibu y Karne, Na historia utanikumbuka kuwa ndiye Rais pekee baada YA mfumo Wa vyama vingi ambaye aliteuliwa Na tume na kupita bila kupingwa

Kama CCM Ni wanaume twendeni Kati kwenye mfumo Ulio bora
No reforms no election lini? Taja tarehe kisha kaige familia yako kuwa naenda kuzuia uchaguzi.
 
Labda wamejitoa mhanga kama Hamas
 
Kura wanapiga CCM wenyewe walalamikaji ni Chadema😀
 
Kuna mawili naweza kurudi au nisirudi hii ndiyo njia muhimu kwenu ya kumuenzi Tundu Lissu. Sasa hivi Polepole anaonekana shujaa kwa wafuasi wa Chadema kuzidi Lissu na Heche daaah.
Mtu mwenye akili timamu hawezi kuja humu kwenye jukwaa hili na kuandika upuuzi wa aina hii.

Lakini inafaa p ia uelewe kuwa pamoja na njama zote dhidi ya CHADEMA, Samia na GENGE lake hawapati ahueni yoyote. Hali ndiyo inazidi kuwawia mbovu zaidi.

CCM ambayo GENGE liliiteka na kukitumia chama kama ngao ya kuvuruga nchi, wanachama wa chama hicho nao sasa wametambua ulaghai mkubwa anaoutumia Samia Suluhu Hassan na GENGE lake kuchafua taswira nzima ya chama chao.

Kwa hiyo, mtu kama wewe unapokuja hapa na kuzungumzia CCM; usisahau kwamba siyo chama kitakacho endelea kushikiliwa na GENGE tena.

Andiko lako hapa ni la kuonyesha maumivu makubwa kwa kupoteza nyenzo mliyokuwa mmeipanga kuwatimizia hujuma zenu kwa waTanzania.
Siyo furaha ya kuwananga CHADEMA, ambao nao watapata nafuu baada ya kutoka kwenye makucha yenu.

Hovyo Kabisa.
 
Sisi tunasubiria tuone mtakavyo kanyagana si mmepitisha wenyewe jana
 
Somo fupi kwa wasio ielewa CCM, hilo ni dubwasha kubwa sana.

CCM ina wanasiasa ambao wamekulia ndani ya chama na kutengenezwa kuwa viongozi mfano Mwigulu, Bashungwa, Biteko, Nape na ghasia wengine wa hovyo leo kama mawaziri.

CCM pia ina walinzi wake (wing ya usalama wa taifa) ambao sio lazima wote uwa wanasiasa ila wanalelewa kuhakikisha CCM inabaki madarakani na Ina wahudumia wananchi; mfano Rajabu Lhuwavi.

Asilimia kubwa ya mawaziri ni vijana waliopikwa na CCM kushika madaraka (ni wanasiasa tu) na kuna watu kama Polepole wanatokea angle zingine za chama za ulinzi hadi kuwa wanasiasa (wapo wengi ila rarely kuwa wanasiasa).

Ndio maana Polepole anaita CCM chama chetu (elewa nyuma yake kuna nguvu kubwa).

CCM sio ya mzaha-mzaha usidhani wahuni wanaweza kukichukua hiko chama kirahisi tu, halafu walinzi wake wawaangalie tu.

Watch this space.

Tanzania ni nchi imara
 
Kura wanapiga CCM wenyewe walalamikaji ni Chadema😀
Umejuaje wanaolalamika ni CHADEMA. Umekagua kadi zao za uanachama wa chama hicho?
Na hata wangekuwa ni wa CHADEMA, wao siyo waTanzania?
 
CDM Ni dude kubwa..Hadi Mwenyekiti yupo ndani (Ili sa100 apite bila kupingwa_ hii Ni aibu y Karne, Na historia utanikumbuka kuwa ndiye Rais pekee baada YA mfumo Wa vyama vingi ambaye aliteuliwa Na tume na kupita bila kupingwa

Kama CCM Ni wanaume twendeni Kati kwenye mfumo Ulio bora
We mwenyewe sijui km unaelewa ulichoandika.
 
Back
Top Bottom