Wafaransa wawili wauawa Zanzibar

Wafaransa wawili wauawa Zanzibar

Status
Not open for further replies.

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,737
Reaction score
42,829
1391241633700.jpg

Zanzibar.Raia wawili wa Ufaransa wameuawa na kutumbukizwa katika kisima cha maji kilichomo ndani ya uwanja wa nyumba yao na watu wasiojulikana katika eneo la Shehia ya Matemwe Kaskazini, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar (DCI), Yussuf Ilembo zinaeleza kuwa watu hao mtu na mkewe waliuawa hivi karibuni.

DCI Ilembo aliliambia gazeti hili jana kuwa tayari vikosi vya Zimamoto na Uokozi (KZU) na Polisi vimeanza kufukua kisima hicho na kwamba katika hatua ya awali wamefanikiwa kukuta mfupa wa mguu wa kushoto wa mmoja wa watu hao.

Aliwataja wazungu hao kutoka Ufaransa kuwa ni Francois Cherer Robert Daniel na Brigette Mary ambao walikuwa wakiishi kama mtu na mkewe wakiwa na mbwa wao anayeitwa Allan ambaye pia amekutwa amekufa ndani ya nyumba hiyo.

Alisema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa Wafaransa hao waliingia nchini kihalali mwaka 2013, na kununua nyumba kwenye ufukwe wa mwambao wa Bahari ya Hindi eneo la Matemwe na kuanza kuishi eneo hilo.

DCI Ilembo alisema polisi tayari wanawashikilia watu watatu wakazi wa Shangani katika Mjimkongwe wa Zanzibar na mmoja anayeishi katika eneo la Kilimani katika wilaya ya Mjini Unguja.

"Kuna askari wanaendelea na kazi ya kuzamia ndani ya kisima kilichomo ndani ya uzio wa nyumba hiyo, kazi bado ni kubwa na siyo ya siku moja," alisema DCI Ilembo.

Gazeti hili limefanikiwa kufika katika eneo la nyumba hiyo na kukuta askari Polisi wanne wakilinda nyumba hiyo huku harufu kali ikitoka katika shimo la kisima.

Hata hivyo, mlinzi wa nyumba hiyo ametoweka katika mazingira ya kutatanisha na simu yake kila ikipigwa imezimwa.

Mlinzi mpya aitwaye Omar Juma ambaye amekutwa akilinda nyumba hiyo baada ya kuajiriwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa amesema alikabidhiwa kazi ya ulinzi kuanzia Januari mwaka huu na hakumkuta mtu yeyote akiishi hapo.

"Kazi yangu ni kazi za ulinzi, nimeletwa hapa na mwajiri, sijui lolote, mwajiri wangu ndiye anayejua kama kulikuwa na watu kabla au la, sina la kusema na sijui nianzie wapi," alisema Omar.

Sheha wa Shehia ya Matemwe Kusini, Denge Khamis Silima aliyelizungumzia suala hilo kwa niaba ya Sheha wa Matemwe Kaskazini, aliliambia gazeti hili kuwa taarifa za kutoweka kwa wazungu hao zilianza kuenea kuanzia Desemba 27 mwaka jana.

Denge alisema alianza kupata taarifa za awali kutoka kwa mjumbe mmoja wa Shehia aitwaye Mkadam Tabu Vuia kwamba mlango wa nyumba ya wazungu hao ulikuwa wazi kwa muda mrefu na harufu kali ikitoka na inzi wakubwa wametanda katika eneo hilo.

"Nimeshiriki katika kazi ya kuchimbua kisima, askari wametoa mfupa wa mguu na unyayo unaoaminika kuwa ni wa mtu, ingawa tuliikuta nyumba ikiwa haikuvunjwa milango," alisema.

Alisema waliingia ndani ya nyumba hiyo kupitia dirishani wakakuta mbwa wa wazungu hao, Allan naye amekufa na kwamba kwa sasa wanasubiri ripoti ya uchunguzi wa polisi.

Sheha huyo wa Shehia ya Matemwe Kusini alisema mazingira waliyoyakuta ndani ya nyumba hiyo yameonyesha kuwa haikuhamwa kwa muda mrefu na kama kwamba wanatarajia kurejea wakati wowote.

Alisema baada ya kutoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya, askari polisi walifika katika eneo hilo na kazi ya kuchimba kisima ilianza baada ya kubaini harufu kali ilikuwa inatoka kisimani.

Hata hivyo, kazi ya kuchimba kisima ilikuwa ngumu baada ya kukutana na zege lililojazwa na walipoendelea kuliondoa zege hilo walipata mguu mmoja wa binadamu.

Denge alisema zoezi la uchimbaji wa kisima hicho lilikwama juzi kutokana na ugumu wa zege na hivyo kazi hiyo kuahirishwa na kuendelea jana baada ya kupatikana mashine ya kuchimbua vitu vigumu na vifaa ya kuongeza hewa ya oksijeni.

"Bado hatujafanikiwa kubomoa zege na kuingia kina kirefu kujua kama ipo mifupa zaidi au la, tunawasubiri polisi na askari wa zimamoto waje na vifaa," alisema Denge.

Agosti 7, mwaka jana raia wawili wa Uingereza, Kate Gee (18) na Kirstie Trup (18) walimwagiwa tindikali mjini Zanzibar.

Tukio hilo lilitokea saa 1:15 usiku Mtaa wa Shangani eneo la Mji Mkongwe wa Zanzibar, karibu na ofisi za Serikali ikiwamo Wizara ya Sheria na Wizara ya Katiba na Maendeleo ya Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto.

Wasichana hao walifika Zanzibar kwa mwaliko wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Arts in Tanzani
.

Source
: gazeti la Mwananchi
 
Hivi ni kweli haya matukio huko yanashindikana kukomeshwa!!!!!?????
 
My take..
inakoelekea z'bar si sehemu salama kwa wageni
 
Hivi ni kweli haya matukio huko yanashindikana kukomeshwa!!!!!?????

matukio haya yanaweza kukomeshwa,lakini kwa sababu hawajui madhara yake kwa ka-nchi kao wanayalea,soon watajua madhara yake na kuchukua hatua.
 
zanziber ina tegemea utalii....hapo wanaanza kuchemsha
 
Nchi ya wajinga kuamini wao ndio wenye hakj pekee ya kuishi kwanini zanzibad isiwe mkoa tumalize haya mambo ya kishenzi hali mnajua viongozi huko wako legelege
 
wazungu hao kutoka
Ufaransa kuwa ni Francois Cherer
Robert Daniel na Brigette Mary
ambao walikuwa wakiishi kama mtu
na mkewe
. Je hao si watu watatu? Au ilikuwa three-some?
Haya matukio yataiyumbisha sana Zanzibar katika soko la utalii. Kwa kuwa serikali imeyafumbia macho kwa makusudi, na wanataka kujitawala, sioni mustakabali imara za Zanzibar.
 
Hayu jamaa aliyewauzia nyumba inabidi akamatwe
 
yani mnafikiria utalii,amfikiri roho za walouwawa,hivi niambie bei ya roho ya mtu ni shingapi?
mi naona zanzibar ingetangazwa kimataifa si sehemu salama kwa mtu asiye mzaliwa wa huko.Labda serekali yao ingechukua hatua madhubuti za kupambana na matendo kibao yanaotokea huko,huku tukiwa hatujaona majibu yoyote,watu washauwawa,washamwagikiwa tindikari nani amekamatwa hadi leo,eneo lenye wakazi wachache namna hiyo unashindwa kubaini wahalifu-Watu wa huko wanaleana wanawaficha watendaj wa vitendo hivyo.kama huku watu wanavyowafuga wezi kisa wanawajua ni watoto fulani.HIVI HUYO MKUU WA POLISI WA HUKO ANASUBIL NINI KUJIUZULU MAANA YAMETOKEA MENGI HAKUNA JIBU HATA MOJA LILONYOKA LILOTOA MATUMAINI KWA NDUGU WALIOPOTEZA NDUGU ZAKO WAKIWA KWENYE ARDHI YA WAZANZIBAR,ngoja niishie hapa msije nin'goa kucha
 
Dhambi hiyo ya ubaguzi hata kuua itawatafuna wazanzibar na haitawabakiza! Ukizoea kula nyama ya mtu utaendelea hivyo hivyo.
 
lile tukio la tindikali limeathiri sana utalii znz watu kadhaa wameniambia hivyo, naona wanakoelekea ni kubaya zaidi. siku zote nashauri znz iwe mkoa tu na watu wa huko wengi waletwe bara ndiyo haya yote yataisha.
 
Wacheni ujinga na machuki ya kipuzi nyinyi, mnataka kusema Tanganyika hakuna mgeni aliyewahi kuuwawa.Tukiangalia haraka haraka tukio ni la kiuhalifu wa kawaida wamewauwa wamiliki wa nyumba ili wahodhi hiyo nyumba na mali nyengine za marehemu hao. Uislama utalii vina uhusianö gn na tukio hilo.? Badala kuwalaan wa husika mnawashambulia Wazanzibar wote plus na Iman yao!! Kwa chuki hz kunasiku mtawavamia kwa vifaru na ndege za kijeshi muwamalize wote.Au simuwambie kosa walio wafanyia km kuna uwezekano wawaombe RADHI.
Lakini km mauwaji ya wageni hakuna Watanzania waliouwa Uengereza Marekani Canada au hata Kenya ? Mbona hamkuzishambulia Nchi husika?
Utalii utakapokufa Zanzbar nyinyi mtafahaidika vipi. WACHENI UJINGA Kampen hizo angalau zingefanywa na KENYA tungewaelewa na si nyinyi kumbuken kwamba TRA na hapa wapo pia.
 
Mimi nadhani hapa hapahusiani na kumtetea allah-n mapigo.
Wala unaweza ikawa sio katika kutekeleza mafundisho ya dini ya haki yenye kuahidi wanawake sabini kama marupu rupu ukifa kazini.
Kwasababu wameua hadi kamboga ka ndugu zetu wahhehhe,hapa ni inaweza kuwa ni suala la mali tuu.
Zanziberi itakuwa salama kwa wageni wasilamu tuu kama mdau mmoja alivyosena hapo juu.
 
Napendekeza itangazwe kimataifa kuwa zanzibar sio mahali salama kwa wageni
 
zanziber ina tegemea utalii....hapo wanaanza kuchemsha

Hawawezi kuchemsha!!!umeme tunawalipia,elimu ya juu tunawalipia,ulinzi na usalama tunawalipia sasa unadhani wanaona maumivu ya kukosa watalii?hao ni watoto wa mama chochote wafanyacho wanadekezwa tu!!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom