Wafanyakazi wote KIA wagoma asubuhi hii!

USD 1000 then Serikali imekaa kimya!!! I think bila CDM wangetuchukulia na wake zetu. Hivi hawaoni uchungu hawa watu au? Wabunge wa CCM wako pale kwa ajili ya nani? Mi nadhani wako kwa ajili ya Chama ila sio wananchi waliowatuma na kuwapeleka kule.....Yana Mwisho Haya.

Hili la USD 1000 nakataa CDM siyo wa kwanza kulizungumzia. Wanaokumbuka wakati wa kampeni 1995 Proffessor Lipumba alilizungumzia kwa uchungu sana wakati huo akifananisha kiwango hicho na mabeberu kumi ambayo mfugaji mdogo kabisa angeweza kulipa. Hata swala la Rada, Professor alishalizingumzia sana kwenye kampeni za 1995 na kuendea tatizo hakuwa na "mass support"
 
Mkurugenzi nakupa hongera kwanza kuvujisha hizo siri..umekuwa mzalendo sio kama kina Idd Simba, Wanajua wanachokivanya halafu wanakaa kimya..Hivi rais anaposikia mambo kama haya yanaendelea anajisikiaje?? Au anapata kale ka 10%..
 
Kwa hiyo wamepewa KIA kwa "vijisenti". Nawasikitika sana wanangu maana wataishi kwenye wataishi nchi iliyouzwa.
 
Hili la USD 1000 nakataa CDM siyo wa kwanza kulizungumzia. Wanaokumbuka wakati wa kampeni 1995 Proffessor Lipumba alilizungumzia kwa uchungu sana wakati huo akifananisha kiwango hicho na mabeberu kumi ambayo mfugaji mdogo kabisa angeweza kulipa. Hata swala la Rada, Professor alishalizingumzia sana kwenye kampeni za 1995 na kuendea tatizo hakuwa na "mass support"

Hakupata "mass support" kwa vile alilisema kwenye kampeni, na ukumbuke wakati huo hata CDM walikuwa wanataka uongozi.
 
1,600,000/=??ndo maana kasungura hakatoshi maana bado tunabadilishana precious assets kwa groli za mviringo,wanaacha kuwafukuza akina Jairo wanamfukuza meneja alafu shuleni tunakaririshwa ..mara good governance,mara rule of law..mara accountability,misamiati migumu kama nini na bado haitekelezeki
 
Mgomo umesitishwa kwanza, kwani kuna kikao cha dharura kimeitishwa ili kusolve hii issue ya wafanyakazi..
 
Halafu jamaa anaulizwa na kujibu kwa madaha kabisa <i><b>&quot;Hata mimi sijui ni kwanini Tanzania tu masikini&quot;</b></i>
<br />
<br />
yaani kama kuna mtanzania mtu mzima afu anasema hajui kwa nini tanzania ni maskin bas HANA AKILI.
 
Wamegoma wapi na zile ndege zimetua jro zimepokeelewa na nani??mkuu
 
$1000 x 1,600 = 1,600,000Tshs....???????
Hii habari ya kodi ni ya kweli kabisa, aliesimamishwa (sio kufukuzwa) anaitwa Bw. Amani,
Infact sie meneja wa Uwanja mzima, but upande wa Civil aviation (usalama wa anga),
Chanzo ni ni jamaa kupigania maslahi duni.
Kwa sasa hali ni shwari na ndege zinatua kama kawa
 
...acha-kumungunya maneno...ni-kusaidie kusema hivi,aliyesewa hajui kwa nini tz ni masikin ni huyo mkuu wa kaya...kwahiyo malizia kumtamka moja kwa moja "mkuu wa kaya ni chizi nukta"
 
Mkuu ukiangalia vizuti kama yeye chizi na unaweza kuta na wazazi wetu wako kwwenye list kwa kumuita katoka kwa mungu kama si kumpigia kura nimekupata lakini ina hu!!! Tunalo huu mwaka wa 1 bado miaka minne
 
hivi hawa viongozi wa magamba wana matatizo gani, mhando TBC walimnyima mkataba mpya kisa kafanya kazi yake vizuri kuripoti matukio ya uchaguzi 2010 bila upendeleo. leo tena huyu nae katoa siri kusaidia ufanisi wa uwanja kawa mbaya , hiv mnataka wafanyakazi wazalendo au wezi.? basi toeni sifa za wafanyakazi kuwa lazima uwe tayari kuiba mali ya Taifa ili tujue kabla ya kuajiliwa.
 
siku hiyo ya mkataba dola 1000 zilikuwa nyingi sana. ila ukisema hata mwaka 2020 utalipa dola 1000 wakati nyakati hubadilika hiyo siyo sahihi. ni kama wakati ule wa Bima Ya Maisha mtu ulikuwa unasaini kulipwa sh laki 5 hata ukifa una miaka 100. wakati unasaini bila kufikiria mbele unaona umeula. haya ndio yaliyotokea kwa KADCO.
 
Siri gani huyo meneja kavujisha kwa wabunge? nchi hii watu wanaonewa sana kazini wakiamua kusema madudu ya wakubwa wanatimuliwa kazi eti wamevujisha siri. wakubwa wao wale, wapendelee, wastarehe huku wafanyakazi wakisononeka kila siku. inabidi tuambiwe hiyo siri ni ipi. Maana ya Multiparty ni Transparency in Governance. Yaani kama vile kuweka kitu kwenye Glasi ambapo kila mtu huona kilichomo. Asante Vyama vingi.
 
Back
Top Bottom