Wafanyakazi Wazawa HALOTEL tunanyanyaswa.

gerry ZaNtes

Member
Jan 1, 2014
25
13
Tafadhali muheshimiwa waziri naomba uanze na kampuni ya halotel wafanyakazi wazawa tunanyanyasika sanaaaa. Hatuna mikataba inayoeleweka, mishahara kiduchu wakat kazi kubwa, hatupewi overtime wakat tunafanya kazi hadi usiku wa manane, hatupewi hata bima ya afya, tunatumia fedha zetu wenyewe kufanya kazi za kampuni na haturudishiwi, tunacheleweshewa mishahara yetu wkt mwingine hadi tarehe 15 mwez unaofuata, mtu akiuliza kitu kuhusu mshahara, marupurupu au overtime anafukuzwa kazi kama mbwa. Hayo ni machache tu tafadhali fika ujionee mwenyewe mheshiwa. Wafanyakazi wazawa halotel tunanyanyaswa wakat wagen wanaishi kama wafalme. Uhuru uko wapi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom