UPUNGUZAJI WAFANYAKAZI KATIKA MAKAMPUNI YA SIMU – JIPU?
Kwa kitambo sasa kumekuwa na wimbi kubwa la upunguzaji wa wafanyakazi katika makampuni ya simu hapa nchini Tanzania. Wimbi hili limeonekana zaidi katika makampuni makubwa zaidi ya simu ya Vodacom, Tigo na Airtel. Haya ni makampuni makubwa ambayo yana wateja wengi zaidi wa simu za mikononi ukilinganisha na makampuni mengine kama Zantel, Smile, Smart, Halotel na TTCL. Ni dhahiri kuwa makampuni haya makubwa yana idadi nzuri tu ya wafanyakazi ambao zoezi hili linawaathiri wao pamoja na wategemezi wao.
Nia ya makala hii sio kulalamika tu juu ya jambo hili kwa kuwa linatokea pia kwenye sekta nyingine za kibiashara duniani. Tunajaribu kuangalia ulazima na uhalali wa zoezi lenyewe. Kwa kampuni kama TTCL ambayo ina wafanyakazi wazalendo wengi kulinganisha na haya matatu na ambayo haifanyi vizuri sana kibiashara, inaweza ingia akilini ukizungumzia upunguzaji wafanyakazi. Makampuni mengine kiuhaliasia hayana wafanyakazi wengi sana licha ya kuwa na “market share”(idadi ya wateja) kubwa kuliko TTCL kwa mfano.
Kinachooneka ni tamaa tu waliyonayo wawekezaji wa makampuni haya makubwa ambayo yapo tayari kufanya kila linalowezekana ku “maximize profit” (kujilimbikizia faida)!! Inafahamika kuwa kumekuwa na ushindani mkubwa wa kibiashara uliopelekea kuwa na ushindani mkubwa unaoonekana zaidi kwenye gharama za kutumia simu (voice and data). Hili linapelekea kila uchao kuwa na “offer” na mapunguzo ya bei yanayolenga kupata wateja zaidi. Na hii hufanyika kwa mtindo wa offer za vifurushi na “promoption” mbalimbali ambazo humpa faida mtumiaji wa huduma. Hii maana yake kupungua kwa faida kwa makampuni haya.
Lakini inasisitizwa hapa kuwa hii maana yake ni kupungua tu kwa faida na kamwe sio kwamba makampuni hayajiendeshi kwa faida. Bado kuna faida ya kutosha hasa katika nyanja za “data” pamoja na ”mobile money transaction” - biashara ya kutuma na kupokea hela kwa njia ya simu. Hizi ni biasahara ambazo watanzania wameonyesha mwamko mkubwa wa kuzitumia.
Wakati kampuni inayomilikiwa na serikali kwa asilimia 100 ikipambana kulinda ajira za wazawa waliopo pale, ingekuwa vema ikatupia jicho lake kwenye kampuni za kiuwekezaji za nje zikiwamo hizi za mawasiliano. Serikali ambayo ina nia thabiti ya kuongeza ajira kupitia viwanda kama inavyonuia, inapaswa pia kulinda ajira zilizopo na kupambana na hila hizi za wawekezaji kuwekeza na kuhamisha faida kila uchao. Serikali pia inapaswa pia kuangalia wimbi la “foreigners” (wafanyakazi toka nje) waliojazana katika makampuni haya ya simu kwa kisingizio cha “wataalamu”.
Najua majibu mepesi ya hawa wataalamu na wawekezaji kama kawaida itakuwa ni Watanzania wengi ni wavivu na hawako “serious”. Lakini ikumbukwe ni watazanzania hao hao walioijenga nchi hii kuwa na mazingira mazuri ya wao kuwekeza na kufanya kazi.Ni watanzania hao hao walioanzaisha baadhi ya makampuni na taasisi ambazo wawekezajia waliona yafaa kuingia ubia!!
Tunafahamu kuna sharia zilizo wazi juu ya wafanyakazi toka nje lakini tunachelea kusema kuwa hazifwati sawasawa na hii inachangia kuongeza matumizi ya makampuni haya kwa sababu mishahara na marupurupu wanayopata wataalamu hawa ni kufuru ukilinganisha na wazawa.Badala ya gharama hizi kuangaliwa pamoja na kupunguza idadi yao, kupunguza wafanyakazi wazawa huoneka njia mwafaka. Hii si sawa wala sio haki!! Mathalani Wakurugenzi Wakuu (MD) wote wa Vodacom, Tigo na Airtel ni kutoka nje pamoja na wakurugenzi wengine kadhaa! Sina hakika kama nafasi zote hizi hamna watanzania wanaoweza tenda kwa weledi na ufanisi. Wala hatupingi wafanyakazi toka nje kwa kuwa tunajua kuna wenzetu wengi wanafanya kazi nje. Ila yote haya yafanywe kwa kufata taratibu na kamwe yasiwe na matokeo hasi kwa Watanzania.
Ni vema watanzania ambao ndio walio wengi hutumia mitandao kufaidika na faida ipatatikanayo angalau kwa kiwango cha ajira kwa wapendwa wao (watoto/waume/wake zao). Uwekezaji wowote unapaswa uwe na manufaa pia kwa wazawa. Kama mheshimiwa Rais ameonyesha ujasiri wa kupambana na kiinimacho cha mchanga wa madini ambacho kimekuwa kizungumkuti cha muda mrefu, basi tuna imani anaweza pia tupia jicho lake huku ili kulinda ajira za watanzania alioapa kuwapigania daima.