Wafanyakazi wa Serikali Zanzibar wamelipwa tayari Mshahara wa Aprili 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameagiza malipo ya mishahara ya mwezi wa Aprili kufanyika mapema kuanzia tarehe 14 Aprili 2023 kwa wafanyakazi wa Serikali kwa ajili ya matayarisho ya Sikukuu ya Eid El Fitr.

Kwa mujibu wa tamko la Rais Dk. Mwinyi, hatua hiyo imelenga kuwapa wafanyakazi Serikalini muda wa kutosha wa kufanya maandalizi ya sherehe za Eid El Fitr.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuangukia kati ya siku ya Ijumaa au Jumamosi ya tarehe: 21 au 22 Aprili 2023 kutokana na kuandama kwa mwezi na kuashiria mwisho wa Ramadhan.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyakazi wa Serikali kwa ushirikiano wao wakati wote wa ibada tangu kuandama kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

1681628953567.jpeg
 
Zanzibar kwenye kuwajali watumishi wako vizuri sana

Hata issue ya nyongeza za mishahara karibu kila mwaka kwenye Mei Mosi huongeza

Na kwenye kupandisha watu madaraja huanza mapema (Aprili na Mei)

Kichefuchefu ni Tanganyika, kama watumishi waliopo chini ya TAMISEMI hawathaminiwi kabisa
Tuache maskhara hakuna watumishi wanashida kama polisi
 
Back
Top Bottom