Wafanyakazi wa mgombea wa CCM wazingira ofisi

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Ni aliyekuwa mgombea wa udiwani kata ya Kirumba kupitia CCM bwana Jackson Robert maarufu kama Masamaki.Hajalipa mishahara ya wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi anayoimiliki iitwayo Victoria Support Services kwa takribani miezi minne sasa.Kwa sasa wafanyakazi wamezingira ofsini kwake pale mtaa wa Nera jijini Mwanza na jamaa kaingia mitini...Kwa sasa wanapanga kuandamana kwenda kwa RC.

Jamaa ameripotiwa kuyumba ki uchumi baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye kampeni kuupata udiwani na kuambulia patupu baada ya wana Mwanza,kata ya Kirumba kula CCM kama kawaida yao na hatimaye kupiga kura yao CDM na kumwezesha mgombea wa CDM kuibuka kidedea.

MY TAKE:Ni bora uongozi wa CCM ukaandaa utaratibu wakuwa unawawezesha wagombea wao hasa wafanyabiashara wanapofikia hatua ya kufulia kwa manufaa ya chama chao.

Source:Mimi mwenyewe nimepita viunga vile vya mitaa ya Nera,picha sikupiga kwani nilihisi uvunjifu wa amani kutokea maana jamaa walikuwa na hasira sana.
 
Idimulwa,
Tunashukuru kwa taarifa. Ukifika Nyamagana msalimie Laurance Masha na ukifika Ilemele mwambie Anthony Diallo nampa hi sana. Waambie wasikonde ndio siasa. Mungua akipenda wanaweza wakarudi mjengoni mwaka 2040.

TUMBIRI wa JF,
P.O BOX - PM JF.
 
Kumbe udiwani unalipa namna hiyo hadi kufikia mtu kufilisi kampuni yake ili achaguliwe!
 
Idimulwa,
Tunashukuru kwa taarifa. Ukifika Nyamagana msalimie Laurance Masha na ukifika Ilemele mwambie Anthony Diallo nampa hi sana. Waambie wasikonde ndio siasa. Mungua akipenda wanaweza wakarudi mjengoni mwaka 2040.

TUMBIRI wa JF,
P.O BOX - PM JF.

Sawa mkuu nitafikisha salaam
 
Tukiendelea kuwafanyia hivi hawa matajiri wa CCM basi watashika adabu na 2015 hakuna atakeyetokeza pua yake kutaka uongozi kwa pesa yake. 2015 wagombea wa chadema wanaweza kuwa wanapita bila kupingwa maana matajiri lazima watasusia CCM.
 
Hivi Lau masha hajachaguliwa katika viti maalumu vya juzi? kachukuliwa Mbatia kaachwa lau masha.Kula CCM kulala CDM.jamaa kafilisi kampunyi kisa udiwani? dah noma
 
Kansa ya kuhonga ili kupata kura imekomaa sana magamba,hakuna hata mmoja anaejiamini lazima kuhonga,stail ya chadema nzuri sana kula ccm... tufike mahali hata kama una buku 20000 tu unagombea ubunge!
 
Msaada ninaoutoa labda niutoa kwa hao vijana wanaodai chao! kwani wanalinda mawe au mali? Wamkomoe tu, si wanajua liability ipo kwake?

Eti eeh...Nimeupenda huu ushauri wako mkuu...wacha niupenyeze kwa wahusika.
 
Hiyo maneno ya kula ccm na kura cdm imenikumbusha Bw Nchemba alivyokuwa anagawa bia pale Arusha Night Park a.k.a Masaburi bar! Vijana walizifakamia huku wakimwona mjinga maana uchaguzi ulikuwa Arumeru yeye anagawa bia Arusha. Poor him!
 
Back
Top Bottom