Wafanyakazi wa hospital ya Butimba Nyamagana wagoma

Zeddicus Zu'l Zorander

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
803
950
Baada ya baadhi madaktari na wauguzi wa hospital ya wilaya ya Nyamagana (Butimba) kusimamishwa kutokana na uzembe uliosababisha watoto wachanga kufariki, leo wafanyakazi wa hospitali hiyo wamegoma kupokea wagonjwa mpaka wenzao watakaporudishwa.

Ndugu yangu aliyepeleka mgonjwa wake hospitali hiyo mida ya saa 5:30 asubuhi amekosa huduma na kuamua kumpeleka hospitali nyingine.

Updates..
Mmoja wa wauguzi aliyekuwa anahojiwa ITV amesema kwamba wamegoma kwa sababu wagonjwa wanawakerembesha sana, wanawaamrisha watoe huduma harakaharaka bila kufuata utaratibu.
 
Serikali inapaswa kuwasikiliza wafanyakazi wake pia na sio kukurupuka kwa kila wanachoambiwa.

Kwa mfano; Tukio la Mtwara, waziri mkuu kuwasimamisha watumishi ilitokana na malalamiko ya watu wasioijua system yetu ya afya. Hospitali inapokosa dawa, sio jukumu la mtumishi kutoa pesa yake mfukoni.

Wanachokifanya serikali ni kujenga chuki dhidi ya wataalamu, na kupalilia chuki baina ya wananchi na wataalamu. Anayekuja kuumia ni mwananchi mwenyewe.

Kitendo cha waziri wa Afya, kusema kuwa anawapa MENO wakuu wa mikoa na wilaya kuwatumbua wataalamu, ni kwanza kinakoleza moto badala ya kutatua changamoto. Kwa sababu, tumeona namna hawa wakuu wakikosa weledi na ufahamu kuhusu masuala mbalimbali likiwemo la afya.

Mimi, niliamua kusomea fani za afya kwa sababu nilizaliwa hospitali na kukulia hospitali huku wazazi wangu wakiwa ni watumishi wa afya kwa miaka mingi sasa. Nilivutiwa siku moja nami nifanye kama wazazi wangu kuwahudumia wagonjwa.

Niliwahi kusema, mama yangu aliugua EPT wakati anamhudumia mgonjwa mwenye TB. Alitumia dawa na akapona, na kipindi hicho nilikuwa High school & kidogo nighairi kuja huko Afya kwa sababu ya tukio lile. Lakini wakanisihi kuendelea na ndoto zangu.

Sasa, napoona serikali haiwajali wataalamu wake na kuwaita MAJIPU, tena wanaofanya kazi katika mazingira magumu nafedheheka sana hasa nikikumbuka tukio la mama.

Ndio maana vijana wengi wanakimbilia kwenye NGO'S kuliko huko hospitali kwa sababu ya haya; Na wamesomeshwa kwa mkopo 100% ili waje wawatumikie wananchi.

Wote serikali, wataalamu & wananchi tusipoungana kupigania afya za watu wetu tutaleta balaa; Na dalili zimeanza kuonekana.

Kazi kwenu!
 
Wanatetea uzembe wa wenzao
Sidhani kama hiyo inaweza kuwa sababu ngoja tuwasikie nayo kwa upande wao wana nini cha kusema. Kwa hali ilivyo sasa hivi sio rahisi mtumishi kutetea uzembe wa wazi wa mwenzie.
Isije kuwa sababu za kuwasimamisha wenzao zikawa ni sifa za Mulugo za kisiasa kulinda cheo chake aonekane kuwa anachapa kazi kumbe sababu ya bifo vile ni ukosefu wa dawa na vifaa tiba na gari la wagonjwa kukosa mafuta.
Sasa hivi sina imani sana na hatua hizi zinazochukuliwa na wanasiasa wa kaliba ya Mulugo.
Mfano ile issue ya walimu 8 kumbe kuna hadithi tofauti kabisa na itakuwa open ndani ya muda mfupi na wazazi wanalijua hilo
 
Kweli mkuu sidhani kama mtumishi anaweza fanya uzembe kama jinsi ilivyoelezwa isije kuwa ni uzembe wa serikali
 
Baada ya bahadhi madaktari na wauguzi wa Hospital ya wilaya ya nyamagana (Butimba) kusimamishwa kutokana na uzembe uliosababisha watoto wachanga kufariki, leo wafanyakazi wa hospitali hiyo wamegoma kupokea wagonjwa mpaka wenzao watakaporudishwa.
Ndugu yangu aliyepeleka mgonjwa wake hospitali hiyo mida ya saa 5:30 asubuhi amekosa huduma na kuhamua kumpeleka hospitali nyingine.

Aaaaghhhrrrr.....
 
Hili suala ni gumu sana na serikali inatakiwa wafikirie sana jinsi ya kutafuta suluhisho la hili hili suala.
Huduma za afya ni mbaya sana na hilo kila mtu analifahamu bila kubisha, hakuna huruma hata kidogo kwa wananchi, kwa ndugu zetu. Wenye hela zao wanakimbilia private lakini wenye hali ya chini ndio hao wanao teseka hadi kupoteza maisha humo mahospitalini.

Wewe daktari, wewe nesi huruma iko wapi, ubinadamu uko wapi? uwito uliojifunza uko wapi? Leo hii mnagoma, je mligoma pia wakati wagonjwa, wakina mama na watoto wao kupoteza maisha??? Mna goma kwa sababu mnafurahia uzembe uliofanyika???
Tuna fahamu maisha ni magumu, mshahara ni mdogo lakini je umejiuliza kwa hao wagonjwa wanao kuja hapo wanauwezo gani? wana maisha ya Aina gani?
Mna goma kwa sababu mko wachache, na mnafaamu kabisa kua mkigoma watuwatanipigia magoti..
Mna goma lakini je mmejiuliza kuna leo na kesho? leo ni yeye kesho ni wewe...
je mmejiuliza upande wapili wa Tanzania kuna ndugu yako, tena akawa ni mzazi wako, ghafla akaugua na akafika hospitalini huku madaktari na manesi wamegoma kama nyinyi.. hatimae mzazi wako akafariki kwa ajili ya kutopata huduma exactly kama mnavyo wafanyie watanzania wengine leo hii... Je utajisikiaje? will you forgive your self?? je unaamini kua kuna mungu? usiniambie unaenda kenisani au una swali kila siku halafu leo hii una fanya jambo kama hili??
Hali ni ngumu lakini tunaomba madaktari, manesi wa watanzania wote tutumie busara, hekima na huruma.
 
Kweli mkuu sidhani kama mtumishi anaweza fanya uzembe kama jinsi ilivyoelezwa isije kuwa ni uzembe wa serikali
Kuna mmoja anasema standard precedure za kupokea na kumhudumia mgonjwa walizifuata, wanasema labda kama kuna mtumishi alitumia lugha za kuchukiza ndio achukuliwe hatua.
 
Kila siku wafanyakaz wa sector ya afya so busara kugoma coz effect take mnaumiza wagonjwa pana jipo apo sio iv iv
 
Serikali inapaswa kuwasikiliza wafanyakazi wake pia na sio kukurupuka kwa kila wanachoambiwa.

Kwa mfano; Tukio la Lindi, waziri mkuu kuwasimamisha watumishi ilitokana na malalamiko ya watu wasioijua system yetu ya afya. Hospitali inapokosa dawa, sio jukumu la mtumishi kutoa pesa yake mfukoni.

Wanachokifanya serikali ni kujenga chuki dhidi ya wataalamu, na kupalilia chuki baina ya wananchi na wataalamu. Anayekuja kuumia ni mwananchi mwenyewe.

Kitendo cha waziri wa Afya, kusema kuwa anawapa MENO wakuu wa mikoa na wilaya kuwatumbua wataalamu, ni kwanza kinakoleza moto badala ya kutatua changamoto. Kwa sababu, tumeona namna hawa wakuu wakikosa weledi na ufahamu kuhusu masuala mbalimbali likiwemo la afya.

Mimi, niliamua kusomea fani za afya kwa sababu nilizaliwa hospitali na kukulia hospitali huku wazazi wangu wakiwa ni watumishi wa afya kwa miaka mingi sasa. Nilivutiwa siku moja nami nifanye kama wazazi wangu kuwahudumia wagonjwa.

Niliwahi kusema, mama yangu aliugua EPT wakati anamhudumia mgonjwa mwenye TB. Alitumia dawa na akapona, na kipindi hicho nilikuwa High school & kidogo nighairi kuja huko Afya kwa sababu ya tukio lile. Lakini wakanisihi kuendelea na ndoto zangu.

Sasa, napoona serikali haiwajali wataalamu wake na kuwaita MAJIPU, tena wanaofanya kazi katika mazingira magumu nafedheheka sana hasa nikikumbuka tukio la mama.

Ndio maana vijana wengi wanakimbilia kwenye NGO'S kuliko huko hospitali kwa sababu ya haya; Na wamesomeshwa kwa mkopo 100% ili waje wawatumikie wananchi.

Wote serikali, wataalamu & wananchi tusipoungana kupigania afya za watu wetu tutaleta balaa; Na dalili zimeanza kuonekana.

Kazi kwenu!
Mkuu,
Hawa jamaa hata hawaoni Dr anahangaika na nini
Daktari wa tz waliowengi wanapata shida sana.
Hawa wanasiasa inabidi wawe makini na maamuzi yao hizi kiki wanazotaka zitaleta shida
 
Haya sasa Mulongo Magesa jipu limeamia mwilini kwake.
Imebainika wauguzi hao wamefukuzwa kazi kwa makosa yanayofanywa na serikali ktk hospital nyingi tz.
 
Back
Top Bottom