Wiyelelee
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 1,071
- 347
Ukweli unauma sana, lakini ndo hivyo. Wakati wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wafanyakazi walikuwa na hesimika sana. Sababu moja ilikuwa ni kwamba hapakuwa na tofauti kubwa ya kipato kati ya wafanyakazi wa serikali na wale wa mashirika ya umma. Pili, japo hali ya kifedha haikuwa nzuri, mfumuko wa bei haukuwa mkubwa kiasi hicho ndo maana hata mahitaji hayakuwa ghali kiasi hicho. Huduma nyingi kama shule na matibabu zilikuwa zikitolewa bure na wafanyakazi wa serilaki walikuwa wanapatiwa nyumba za kuishi karibu na sehemu walizokuwa wakifanyia kazi. Hali hiyo ilikwenda sambamba na shule, vyuo ambapo taasisi hizi za serikali zilipata heshima sana.
Ikaja wakati wa ruksa oooooooo! Wacha wafanyakazi wadhalilishwe! Wengi waliikimbia serikali na kupata ajita kwenye NGO's CBOs, etc. Maana hata haikuwa na maana kufanya kazi kwenye mashirika ya umma kwa kuwa ulikuwa muda wa kukwapua kilichokuwepo.
Alipoingia Mzee Mkapa, ile heshima ilirudi tena. NAkumbuka wafanyakazi wenzangu waliacha kazi kwenye taasisi zisizo za serikali na kuingia serikalini. Mfumuko wa bei ukadhibitiwa hadi kufikia asilimia 4.5. Nakumbuka huko Salidalama pale Tandale unga super sembe ulikuwa Tshs. 180, Pepsi 150, Coca 200, Mkate 150 hadi 200, Nyama 600, Mchele Super 450, maharage 250, Sukali 300, vyumba vya kupanga Tshs 3,000 hadi tshs. 5,000. Vile vya self contained Tshs 10,000. Watu wakafurahia maisha kwa Mshahara wa Tshs 100,000 hadi 280,000. Wenye mapato makubwa ilikuwa hadi Tshs 450,000 (Wakurugenzi).
Ikaja awamu hii...mmmh! Awamu ya nne mbaya. Wafanyakazi wa serikali hawalipwi kwa wakati. Wanashindia mihogo inayouzwa pale karibu na Wizara ya Afya na IFM, hapo Jengo la Mkaguzi Mkuu nk nk. Wengi pia wameishia kuwa ombaomba! Mtu akimuona mfanyakazi wa serikali anamkimbia kwamba atamuomba hela! Fikiria hadi leo wengine hawajalipwa mshahara wa mwezi uliopita!
Tazama mfumuko wa bei, gharama za maisha, nyumba za serikali ndo kama hivyo zimeuzwa na wajanja, gharama za matibabu na shule zinapanda Mlima Kilimanjaro! Kila mmoja analalamika! Kwa kweli tunataka serikali iyaone haya na iyafanyie ufumbuzi wa haraka ili kurudisha imani na heshima kwa wananchi na wafanyakazi wa serikali.