Wafanyakazi serikalini wapoteza heshima

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,071
347
Ukweli unauma sana, lakini ndo hivyo. Wakati wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wafanyakazi walikuwa na hesimika sana. Sababu moja ilikuwa ni kwamba hapakuwa na tofauti kubwa ya kipato kati ya wafanyakazi wa serikali na wale wa mashirika ya umma. Pili, japo hali ya kifedha haikuwa nzuri, mfumuko wa bei haukuwa mkubwa kiasi hicho ndo maana hata mahitaji hayakuwa ghali kiasi hicho. Huduma nyingi kama shule na matibabu zilikuwa zikitolewa bure na wafanyakazi wa serilaki walikuwa wanapatiwa nyumba za kuishi karibu na sehemu walizokuwa wakifanyia kazi. Hali hiyo ilikwenda sambamba na shule, vyuo ambapo taasisi hizi za serikali zilipata heshima sana.

Ikaja wakati wa ruksa oooooooo! Wacha wafanyakazi wadhalilishwe! Wengi waliikimbia serikali na kupata ajita kwenye NGO's CBOs, etc. Maana hata haikuwa na maana kufanya kazi kwenye mashirika ya umma kwa kuwa ulikuwa muda wa kukwapua kilichokuwepo.

Alipoingia Mzee Mkapa, ile heshima ilirudi tena. NAkumbuka wafanyakazi wenzangu waliacha kazi kwenye taasisi zisizo za serikali na kuingia serikalini. Mfumuko wa bei ukadhibitiwa hadi kufikia asilimia 4.5. Nakumbuka huko Salidalama pale Tandale unga super sembe ulikuwa Tshs. 180, Pepsi 150, Coca 200, Mkate 150 hadi 200, Nyama 600, Mchele Super 450, maharage 250, Sukali 300, vyumba vya kupanga Tshs 3,000 hadi tshs. 5,000. Vile vya self contained Tshs 10,000. Watu wakafurahia maisha kwa Mshahara wa Tshs 100,000 hadi 280,000. Wenye mapato makubwa ilikuwa hadi Tshs 450,000 (Wakurugenzi).

Ikaja awamu hii...mmmh! Awamu ya nne mbaya. Wafanyakazi wa serikali hawalipwi kwa wakati. Wanashindia mihogo inayouzwa pale karibu na Wizara ya Afya na IFM, hapo Jengo la Mkaguzi Mkuu nk nk. Wengi pia wameishia kuwa ombaomba! Mtu akimuona mfanyakazi wa serikali anamkimbia kwamba atamuomba hela! Fikiria hadi leo wengine hawajalipwa mshahara wa mwezi uliopita!

Tazama mfumuko wa bei, gharama za maisha, nyumba za serikali ndo kama hivyo zimeuzwa na wajanja, gharama za matibabu na shule zinapanda Mlima Kilimanjaro! Kila mmoja analalamika! Kwa kweli tunataka serikali iyaone haya na iyafanyie ufumbuzi wa haraka ili kurudisha imani na heshima kwa wananchi na wafanyakazi wa serikali.
 
Ukweli unauma sana, lakini ndo hivyo. Wakati wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wafanyakazi walikuwa na hesimika sana. Sababu moja ilikuwa ni kwamba hapakuwa na tofauti kubwa ya kipato kati ya wafanyakazi wa serikali na wale wa mashirika ya umma

hapo kwenye blue pana mkinzano; nafikiri hujaelewa maana ya watumishi wa umma au watumishi wa serikali!!! hao uliowataja hapo wote ni kitu kimoja!!!! kwani watumishi waliojiriwa na serikali kuu, local government na kwenye mashirika ya umma wote ni watumishi wa serikali (wote ni watumishi wa uma) na ndio maana sheria yao ya ajira ni moja, yaani public servants Act!!!!!
 
hapo kwenye blue pana mkinzano; nafikiri hujaelewa maana ya watumishi wa umma au watumishi wa serikali!!! hao uliowataja hapo wote ni kitu kimoja!!!! kwani watumishi waliojiriwa na serikali kuu, local government na kwenye mashirika ya umma wote ni watumishi wa serikali (wote ni watumishi wa uma) na ndio maana hata sheria yao ya ajira ni moja, yaani public servants Act!!!!! hata sheria zinazowabana vingozi wa umma ni moja; hiyo hiyo iliyombana Mhando wa TANESCO(shirika la umma) ndio hiyo hiyo iliyowabana mawaziri!!!!
 
Ukweli unauma sana, lakini ndo hivyo. Wakati wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wafanyakazi walikuwa na hesimika sana. Sababu moja ilikuwa ni kwamba hapakuwa na tofauti kubwa ya kipato kati ya wafanyakazi wa serikali na wale wa mashirika ya umma

hapo kwenye blue pana mkinzano; nafikiri hujaelewa maana ya watumishi wa umma au watumishi wa serikali!!! hao uliowataja hapo wote ni kitu kimoja!!!! kwani watumishi waliojiriwa na serikali kuu, local government na kwenye mashirika ya umma wote ni watumishi wa serikali (wote ni watumishi wa uma) na ndio maana sheria yao ya ajira ni moja, yaani public servants Act!!!!!

Yaa, umepatia, nilimaanisha wafanyakazi wa mashisika ya Umma kama TRC, NMC, RTC kwa wakati huo.
 
Wakwanza kwenye kundi la wafanyakazi kudharauliwa ni walimu,hadi leo ndo wanalipwa kiduchu na mazingira duni ya kazi.
fikiria mwalimu wa Math anagombania daladala na wanafunzi wake wa form II alafu mwanafunzi anawahi seat ambapo mwalimu wake anasimama kwenye foleni hizi.
Chora hii pich kichwani mwako then uone ujio wa heshima!
 
unajua matokeo yake ni kutowajubika kwa wafanyakazi wa kipato cha chini si unaona mawazili mara huku mara kule makatibu vilevile wakurugenzi kwakuwa wanapata pesa na hali ya kufanya kazi wanayo hawa wanaolipwa kidogo wanafanya kazi watakavyo si unajua ukimsajili mchezaji kwa mia atacheza mpira wa mia. hivyo hivyo wafanyakazi wanafanya kazi kulingana na mshahara wake anaoupata ukichelewa naye kazi hafanyi kama mshahara unatosha siku tano anafanya kazi kwa nguvu siku tano zilizobakio inakula kwa serikari
 
Zamani ilikuwa hashima kubwa kufanya kazi serikalini angalia manesi na madaktari maskini jamani
 
Ukweli unauma sana, lakini ndo hivyo. Wakati wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wafanyakazi walikuwa na hesimika sana. Sababu moja ilikuwa ni kwamba hapakuwa na tofauti kubwa ya kipato kati ya wafanyakazi wa serikali na wale wa mashirika ya umma

hapo kwenye blue pana mkinzano; nafikiri hujaelewa maana ya watumishi wa umma au watumishi wa serikali!!! hao uliowataja hapo wote ni kitu kimoja!!!! kwani watumishi waliojiriwa na serikali kuu, local government na kwenye mashirika ya umma wote ni watumishi wa serikali (wote ni watumishi wa uma) na ndio maana sheria yao ya ajira ni moja, yaani public servants Act!!!!!

kateleza kidogo nadhani alimaanisha wafanyakazi wa sekta binafsi!
 
Pamoja mkuu,maisha magumu hata lunch tumeshindwa kwenda,tunaangaliana tu hapa ofisini,mpaka sasa hv no mshahara
Kweli ccm has to go lol

Mimi ndo kinaniuma sana maana mke wangu yuko serikalini na wakati mwingine nafikiria kwamba labda ananidanganya. Ila nikipiga simu kwa rafiki yangu kule hazina, unakuta anasema eti Epicor ina tatizo. Kwanini kama tatizo ni Epicor watu wasiende kusomeshwa? Katika sheria kuna kitu tunaita "Reasonable mind of Expectation" ambapo akili ikijiseti kwamba itapata kitu fulani, ikikosa kila kitu kinaweza kuvurugika. Fikiria kama unadaiwa kodi na mwenye nymba na wewe na mkeo mko serikalini. mkamuahidi mwenye nyumba kwamba tunakupa kodi Novemba. Halafu inakuja Nov wote hamna hela, Decembe unayasikia yale yale eti Epicor! Hivi wanataka watu waingie kazi ya ujambazi? Ndo maana Polisi wameanza kuwatapeli watu kwa kuwatoza Tshs. 800,000 kwa kazi ya polisi na kuwadanganya kuwapeleka Moshi CCP, kuwanyoa na kuwarudisha makwao. Yote haya ni kwavile hali imekuwa mbaya sana!
 
Weeh kaka! Yaani mkeo anakuambia hawajalipwa mshahara, unapiga simu kwa mtu hazina kuulizia?!?!?!?!?!

Hivi wewe mkeo akipiga simu ofisini kwako kuulizia kama ni kweli hamjalipwa mshahara utajisikiaje? Sijali sana arrangement zenu za maisha hata kama mkeo ndo analipa bills, lakini umezidisha aisee!

Mimi ndo kinaniuma sana maana mke wangu yuko serikalini na wakati mwingine nafikiria kwamba labda ananidanganya. Ila nikipiga simu kwa rafiki yangu kule hazina, unakuta anasema eti Epicor ina tatizo. Kwanini kama tatizo ni Epicor watu wasiende kusomeshwa? Katika sheria kuna kitu tunaita "Reasonable mind of Expectation" ambapo akili ikijiseti kwamba itapata kitu fulani, ikikosa kila kitu kinaweza kuvurugika. Fikiria kama unadaiwa kodi na mwenye nymba na wewe na mkeo mko serikalini. mkamuahidi mwenye nyumba kwamba tunakupa kodi Novemba. Halafu inakuja Nov wote hamna hela, Decembe unayasikia yale yale eti Epicor!
 
Weeh kaka! Yaani mkeo anakuambia hawajalipwa mshahara, unapiga simu kwa mtu hazina kuulizia?!?!?!?!?!

Hivi wewe mkeo akipiga simu ofisini kwako kuulizia kama ni kweli hamjalipwa mshahara utajisikiaje? Sijali sana arrangement zenu za maisha hata kama mkeo ndo analipa bills, lakini umezidisha aisee!

Yaani yote haya wewe umeliona hilo tu? Kwanza mke wangu hayuko hazina...na mimi sitegemei mshahara wa mke wangu. I am an academician and there are things that are important to follow up whether they concern you or not for the purpose of the interest of the society. Ni kwasababu hiyo basi utafiti huo umechangia kuona jinsi wafanyakazi wengine wa serikali wanavyoteswa wakati mshahara wao ni mdogo sana. Tena wanadhalilishwa kwa maana hata mlo wa mchana hawauoni. Hivyo kupiga simu hazina na kuulizia katika reasoning kuna kitu tunaita "Inductive reasoning, which is reasoning from particular to general (logical reasoning). There are other schools of thought but i chose this one and used my wife as a sample before generalising my results. Sijui kama limeeleweka hapo.
 
unajua matokeo yake ni kutowajubika kwa wafanyakazi wa kipato cha chini si unaona mawazili mara huku mara kule makatibu vilevile wakurugenzi kwakuwa wanapata pesa na hali ya kufanya kazi wanayo hawa wanaolipwa kidogo wanafanya kazi watakavyo si unajua ukimsajili mchezaji kwa mia atacheza mpira wa mia. hivyo hivyo wafanyakazi wanafanya kazi kulingana na mshahara wake anaoupata ukichelewa naye kazi hafanyi kama mshahara unatosha siku tano anafanya kazi kwa nguvu siku tano zilizobakio inakula kwa serikari

No wonder 1+1=3
 
Back
Top Bottom