ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,051
- 49,736
Hongera sana Watumishi wa TanRoads Kwa kupata kazi za Kudumu na bila shaka mtakumbuka fadhila za Mama mwaka 2025 maana Kuajiri watu wengi hivyo Kwa mara Moja Huwa ni Kwa Walimu na Manesi tuu.Kwenye swala la Ajira Samia hana mpinzani.
Pia hongera sana bwana Besta ,always watu wa dini Ile Huwa na huruma maana ungeweza kuacha na kusema mbona wengine wameacha lakini ukachukua initiative ya kiungwana.
Maana sio Haki Taasisi Kuajiri na kutumia 70% ya Watumish Kwa mikataba then ikija Ajira wanapata watu wengine kabisa tofauti na hao ambao wanafanya kazi taasisi mda mrefu.
My Take
CEOs wengine wanifunze Kwa Bwana Besta hususani TARURA,RUWASA, TANESCO, Halmashauri nk ambako wamekuwa wanatumia sehemu kubwa ya Wafanyakazi wa mikataba ila linapokuja Suala la Ajira wanapata watu wengine badala ya ku recruit staff wa mikataba waliopo kazini mda mrefu.
============
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) tangu mwezi June mwaka jana 2023; imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kutoa ajira za kudumu kwa Wafanyazi waliokuwa na ajira za mikataba ili kuboresha utendaji kazi kwenye Taasisi hiyo.
Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mha. Mohamed Besta wakati akifungua Mkutano 19 wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 13 hadi 14 Februari 2024 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Amesema wakati anaingia mwezi June 2023; Taasisi hiyo ilikuwa na Wafanyakazi 755 ambao walikuwa wameajiriwa kwa kudumu na wengine 2100 wakiwa wameajiriwa kwa masharti ya muda yaani mikataba, sasa kwa kushirikiana na Menejimenti wamechukua hatua Madhubuti ambapo wameweza kuomba na kupata kibali cha kuajiri wale ambao waliokuwa na mikataba na sasa wemekuwa Waajiriwa wa kudumu kwenye Taasisi hiyo.
Amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kwamba kadri hali inavyoendelea kuwa nzuri, itaendelea kuboresha maslahi ya Wafanyakazi kwa mujibu wa Uchumi wa Nchi yetu.
Amewashukuru Wafanyakazi hao kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha katika nyakati zote za utendaji kazi hasa kwa kuwekeza nguvu, ujuzi na utaalamu wao katika kipindi ambacho Serikali kupitia TANROADS ilikuwa ikitatua changamoto zilizotokana na Mvua kubwa za El- nino ambazo katika baadhi ya Mikoa iliyoharibika miundombinu ya barabara.
Mtendaji huyo Mkuu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS amesisitiza “Nawashukuru sana kwa ushirikiano ambao mnaoendelea kunipa hata katika mazingira magumu tuliyonayo sasa ya Mvua za El-nino mmeendelea kufanya kazi usiku na mchana ninawaomba tuendelee kuushi kwa pamoja tuishi kama Ndugu sisi ni familia, katika uongozi wa siku hizi kazini pawe mahala mazuri pa kuishi wafanyakazi wenzako wakuone ni sehemu ya Maisha yao kwamba mnaweza kutatua changamoto mbalimbali za kazi na hata za Kijamii’’.