Wafanyakazi precision Air wanakera

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,741
2,000
Nimekuwa nikisafiri mara kwa mara na shirika la ndege la precision Air mara kwa mara, katika kusafiri kwangu nimekuwa nakerwa sana na wafanyakazi ndani ya ndege wa kampuni hii wanavyojifanya kwamba kiswahili hawakijui vizuri! ajabu sana!. Kwa yeyote aliyesafiri na shirika hili atakubaliana na mimi kwamba lafudhi wanayoitumia katika kutoa matangazo au maelekezo unaweza ukadhani ni mgeni ameajiliwa kufanya kazi hiyo. Kwa ufupi wanaongea kiswahili katika intonation ya kiingereza! huu nauchukulia kama ushamba na ujinga na utumwa wa fikra.

Juzi juzi nilisafiri na kenya airways unafurahia jinsi mkenya anavyotamka maneno ya kiswahili na anapotakiwa kuongea kiingereza unakubali pia. Hawa wa precision ni kinyume kwa kweli wanahitaji kurekebishwa maana wanatia kinyaa.

Nawakilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom