Wafanyakazi nchi zima kuandamana kupinga bei ya umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi nchi zima kuandamana kupinga bei ya umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jay One, Dec 25, 2010.

 1. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,084
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi wote nchini watandamana kupinga bei ya umeme, hayo yamesemwa na
  Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicholas Mgaya, source Mwananchi 25 Dec 2010
  The only way now ni Maandamano to save TZ iliyo lemewa na ufisadi, outdated constitution favours only one party, & new NEC
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hongereni wafanyakazi. Sasa sisi wafanya biashara haturuhusiwi?
   
 3. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kama unaathiriwa na madudu ya Tanesco then una kila haki ya kuandamana kudai haki yako maana wanakuwa wanakiuka sehemu yao ya mkataba wa huduma na wateja. Wanafunzi, wafanyakazi, wafanyabiashara, wenye kazi za ufundi, watoa huduma mbalimbali, watumia barabara na wananchi wote kwa ujumla wana haki ya msingi ya kuandamana kwenda ofisi zote za Tanesco za kanda, makao makuu pale Ubungo na pia kwenye ofisi ya mheshimiwa Mganga Ngeleja na kushinikiza ang'atuke kwa kuudanganya umma na kushindwa kufanya kazi iliyompeleka pale.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TANESCO kama mlidhani Badra Maasoud ndiye aliyekua mbaya wenu mkamnyang'anya ajira yake, sasa wala dili wa kupotezesha umeme ili wakachote fedha zetu kiaina aina, kitumbua ndio hicho kianaingia sumu wala si mchanga tena.

  Ni garika ukisikia wafanyakazi wameamua kugoma. Moto huu wa kuibiwa watu 'KURA ZAO' ni moto mkubwa mpaka chao kirudishwe!! Ngeleja, ahadi yako ya kutokukata umeme ndio vipi tena au ndio mpaka miaka mitatu itakayogeuka tena kuwa umri wa mtoto kwenda shule?????????

  Katika hili,vyama vyote vyama vyote vya siasa, vyuo, asasi za kirai, na hata wakulima vijijini lazima tuandamane mpaka kieleweke maana gharama za bidhaa zizalishwazo kwa umeme wa jenereta bila sha itapanda, watu kupunguzwa ajira, masomo kutetereka, na gharama ya mkulima naye kufikisha mali ya shamba sokoni kuwa taabu maana mafuta yakuendeshea gari yatakua yakigawiwa kati ya magari na mijenereta.

  Habari ndio hiyo, wasemavyo Dr Slaa na Prof Lipumba kwamba kuichagua CCM au hata kuiruhusu kukuibia kura ni MAAFA, sasa ukwelio huo ndio huu hapa.
   
 5. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wakati ninyi manalalamika umeme Rais yenu yeye anaendelea kukata mawingu tu. Amenishtusha sana eti kipindi hiki anafanya safari ya Malawi tena kwa siku moja? Sasa si wangeongea tu kwa simu ikatosha?

  Kweli hili tunalo watanzania
   
 6. e

  ejogo JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naomba safari hii tufanye kweli hata wakitutishia nyau. Haina maana hata kidogo mshahara hawaongezi lakini wanazidi kutupandishia tu gharama za maisha kila kukicha. Wanataka tujiue kwa ukali wa maisha!!
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Kwenda kutafuta hifadhi kama akina raisi Mengistu Haile Mariam au Siad Bare waliokimbia nchi zao ni sharti uende mguu kwa mguu endapo mamba hayatokua mambo tena maana wapigakura wameamua kila kona ya nchi wanataka chao.

  Sasa, kwa hali hiyo kaka si lazima utangaziwe kinachotokota maana hata kule ma-Ulaya Ulaya nako hakukimbiliki tena maana ukishaiba tu kura na kuingia madarakani kimabavu watu wapende wasipende basi ujue kwa wenzetu ushakua adui.


  Mapinduzi ya Nguvu wa Umma ni mbaya zaidi maana huwezi kuongoza watu wasiokua na imani na wewe kimabavu. Lazima uchumi utatetereka sana, maisha kuendelea kuwa magumu mno na mwisho wake ...
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Bei ya umeme Tanzania ni kubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kati (Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda na Tanzania) na si ajabu katika Afrika nzima. Wtanzania si ajabu ina watumiaji wachache wa umeme katika bara la Afrika kulinganisha na nchi yoyote ile (watumiaji laki sita na ushee baada ya miaka 49 ya kujitawala). Mishahara yetu si ajabu ni katika ile midogo katika nchi nyingi za Afrika labda tunaweza kuwemo katika top 5 labda tumezipita Somalia na nchi nyingine chache. Pamoja na hayo tuna "amani" ya miaka chungu nzima na rasilimali mbali mbali zikiwemo dhahabu, uranium, almasi, Tanzanet, mbuga za wanyama zinazowavutia watalii chungu nzima toka duniani kote, vyanzo vingi vya maji vikiwemo mito, maziwa na bahari. Vyote hivi havisaidii katika kuinua hali ya maisha ya Watanzania walio wengi. Tuna nini sisi Watanzania!? Tumerogwa au tumeleaaniwa na Mungu!? Aaaaaaaarrrrrggggghhhhhhh!!!:angry:

  Nchi nyingine katika hali kama hizi nilizozitaja hapo juu ingekuwa mbali sana kimaendeleo na wananchi wake wangekuwa na maisha mazuri sana ukilinganisha na maisha ya Waafrika wengi katika bara letu. Miye nayaunga mkono haya maandamano. Hili ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 18.5 lipigwe vita kwa kila hali.

  Hivi TANESCO imekosa kabisa kutafuta njia nyingine za kuongeza mapato yao na pia kupunguza gharama zao za uendeshaji? Kwanini wafanya kampeni ya nguvu kudai madeni sugu ya mabilioni toka kwenye taasisi mbali mbali za Serikali, mashirika na watu binafsi? Kwanini wasipunguze mishahara yao na marupurupu kwa asilimia fulani (10% to 20%) au hata kupunguza idadi kuwa ya wafanyakazi walionao? (kitu ambacho huwa sikifagilii sana)

  Kwa mwendo huu wa TANESCO kutaka kuongeza bei kila kukicha kutokana na madudu chungu nzima yaliyofanywa na Vingunge wa awamu ya pili, tatu na nne (IPTL, Net Gropu Solutions, Richmond/Dowans n.k) basi si ajabu idadi ya wateja wa TANESCO itapungua sana na kuwa chini ya hao wateja laki sita na ushee maana Watanzania wengi watashindwa kuhimili bei kubwa za TANESCO kutokana na mapato yao kiduchu.


  MERRY XMAS
   
 9. A

  Alpha JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  i'll believe it when i see it.

  Watanzania walivyo waoga.
   
 10. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi wa Serikali Tuuu au pamoja na Sekta Binafsi aka Makampuni???

  Mbona Wafanyakazi wa Sekta binafsi inaonekana kama hawana mtetezi? Ile nyongeza yao ya mshahara ilifanyika au ilikuwa siasa? Je TUCTA wanasemaje kwa hili.

  kati ya wafanyakazi sekta binafsi/makampuni/viwanda na Wale wa Serikali/Mashirika ya Umma ni wepi wengi?
   
Loading...