Wafanyakazi 150 kufyekwa ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi 150 kufyekwa ATCL

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Farmer, Mar 17, 2009.

 1. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  WAFANYAKAZI wanaokadiriwa kufikia 150 kati ya 297 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), watapunguzwa kazi ili kuweka uwiano kati ya watumishi na idadi ya ndege zinazotoa huduma ndani ya shirika hilo, Mwananchi imebaini.

  Kwa muda mrefu, ATCL imekuwa ikishutumiwa kwa kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi isiyolingana na ndege inazomiliki. Habari za kuaminika zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa wafanyakazi hao wanatakiwa wawe wamepunguzwa kazi ifikapo Mei, mwaka huu.
  Kwa mujibu wa taarifa hizo, mikakati inayofanyika sasa ni mchakato wa kuandaa hesabu za mafao ya wafanyakazi hao, zoezi linalofanywa kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha na Uchumi.
  Shirika hilo la umma ambalo lipo kwenye harakati ya kuendeshwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni moja ya China, kwa sasa lina ndege mbili tu ambazo zinatoa huduma ya usafiri ndani ya nchi.

  Katika idadi hiyo ya wafanyakazi 150 watakaopunguzwa, wachache ambao ATCL itawahitaji baada ya kuongeza idadi ya ndege zake, watapewa likizo ya bila malipo kwa muda usiojulikana.
  Miongoni mwa waliomo kwenye orodha ya kupewa likizo bila malipo wamo marubani na watendaji wa ndege, ambao ni adimu katika sekta ya usafiri wa anga.

  ATCL kwa sasa ina marubani wazalendo 20 na wengi kati ya hao wakiwa katika orodha ya kupewa likizo hiyo bila malipo. Hata hivyo, suala la kupewa likizo bila malipo limekuwa na mvutano mkali kiasi cha kusababisha mpango wa kufanikisha zoezi hilo kusuasua.
  Inaelezwa kuwa hali hiyo inatokana na Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU), kuweka wazi kuwa hakuna sheria inayoruhusu mfanyakazi kupewa likizo ya bila malipo.

  Chanzo chetu kinapasha kuwa mazingira hayo yanaashiria kuwa huenda wafanyakazi hao adimu wakawekwa katika orodha ya watakaopunguzwa, lakini baadaye wataajiriwa upya kutokana na umuhimu wao.

  Mwananchi lilipowasiliana na mkurugenzi mkuu wa ATCL, David Mattaka, alijibu kuwa ni mapema kuzungumzia suala hilo kwa sababu bado lipo kwenye mchakato.
  "Siwezi kusema lolote kwa sasa kwa sababu hili ni suala ambalo lipo kwenye mchakato. Subiri likikamilika tutawaeleza, hakuna jambo la siri," alisema Mattaka, ambaye alikuwa mkurugenzi wa PPF.

  Serikali kwa sasa ipo kwenye mkakati wa kuliendesha shirika hilo kwa ubia na kampuni ya Kichina ijulikanayo kama China Sonangol International Ltd (CSIL).
  CSIL ilitiliana saini na serikali hati za makubaliano Februari mwaka huu. Katika makubaliano hayo, pande hizo mbili zilikubali kuhakikisha ndege saba zinanunuliwa ifikapo mwaka 2012. Tayari CSIL limeilipa moja ya kampuni za nje kufanya tathmini ya mfumo mpya wa kuiendesha ATCL pamoja na idadi ya wafanyakazi watakaoajiriwa.

  Serikali ilivunja mkataba mwingine wa namna hiyo na Shirika la Ndege la Afrika Kusini Agosti 2006 baada ya kubaini kuwa hali ya ATCL inazidi kuwa mbaya. Kuanzia hapo serikali ilikusudia kuifufua upya ATCL, lakini mambo yalikuwa mabaya zaidi baada ya shirika hilo kunyang'anywa leseni yake ya kurusha ndege angani mwishoni mwa mwaka jana kutokana na kasoro kadhaa za kiutendaji.

  Baada ya kusahihisha kasoro hizo, ATCL ilirejeshewa na sasa shirika hilo limeanza tena kutoa huduma kwa kuchechemea baada ya wateja wengi kupoteza imani kutokana na kunyang'anywa cheti cha usafiri wa anga.  Source; Mwananchi
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Kupunguza wafanyakazi (retrenchment), sio kitu kizuri. Yule mesenger mleta barua za kupunguzwa kazi kwa despatch anaitwa 'Israeli'. Hili ni jambo mbaya kabisa katika ajira ila inapofikia shirika (ATCL), lina watumishi 300 kuhudumia ndege 2!. Suala hili haliepukiki.
  Haya, kupunguza, wapunguzeni ila mafao yao lipeni pamoja na golden handshake yao ya maana. Najua ATCL haina kitu lakini serikali has to bail it out and bear the burden.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Na Mattaka MD aliyelifikisha hili shirika hapa kwa hasara je nae atapunguzwa kazi ili kuongeza ufanisi?
   
 4. Marlenevdc

  Marlenevdc Member

  #4
  Mar 17, 2009
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  At last some people are waking up and opening their eyes!
  I have never stopped wondering why Kenya Airways has been expanding its business, increasing its services and in fact challenging Ethiopian Airways as the flag bearer of Africa. Nairobi at the moment is the hub of East, Central and South African air travels. Kenya Airways has stable constant connections with European capitals e.g. London, Amsterdam, Copenhagen etc.
  Air Tanzania??!! Nothing........
  2 planes with internal flights services with 250 employees. That is what was used to be called COMMUNIST ECONOMIC PRINCIPLES!!
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kweli,

  Ila sii unajua Mustafaa Nyang'anyi na Mattaka ni maswahiba wa JK?
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  JK analipa fadhila kwa maswahiba....kazi zao zingetangazwa kpmg wafanye interview watu wamwage busines plan...waone vichwa vilivyopo na watoe fund atcl itarudi strong sana.....
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hatuitaji ndege zaidi ya tulizo nazo (2). Kwanza hata hizo mbili ni more than we need. Mfano zile flight za KIA/Mwanza kufikisha abiria 50 tu tabu. Bora ku invest kwingine.
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,626
  Trophy Points: 280
  Kupunguza wafanyakazi (retrenchment), sio kitu kizuri. Yule mesenger mleta barua za kupunguzwa kazi kwa despatch anaitwa 'Israeli'. Hili ni jambo mbaya kabisa katika ajira ila inapofikia shirika (ATCL), lina watumishi 300 kuhudumia ndege 2!. Suala hili haliepukiki.
  Haya, kupunguza, wapunguzeni ila mafao yao lipeni pamoja na golden handshake yao ya maana. Najua ATCL haina kitu lakini serikali has to bail it out and bear the burden.

  MKUU;HILI SHIRIKA LINA NDEGE 4,HUO UHUNI WA WAZIRI KUKIMBILIA NDEGE NI UJINGA;NILIPATA KUONANA DADA MMOJA AKANIELEZA MATESO WANAYOPATA KUTOKA KWA VIONGOZI WAO;NDEGE 2 NDIZO ZINAZORUKA;2 MOJA NASIKIA INAITWA AIRBUS LILIKUWA HAPO NASIKA WAMELIPELEKA SERVICE;LINGINE LIKO HAPO DAR;HALINA LILE WAL HILI;MI NAFIKIRI HAWA VIONGOZI WAJIULIZE KWANZA ;

  1) HILO AIRBUS WANALIPA DOLLER 360,000 KWA MWEZI /31 MEANS KWA SIKU MOJA WANATAKIWA KULIPA DOLLER 11,000 USD;SASA ILE NDEGE IMELALA SIKU NGAPI PALE CHINI;NA NASIKIA HIYO ILIOPO BOEING INALIPIWA DOLLER 260,000 USD YAANI KWA SIKU NI USD 8000, BADALA YA KUKAA NA KUTAFAKARI KUENDELEA J=KUPATA HASARA KAMA HIZO WANAKIMBILIA VITU MINOR,HAYA POLE ZAO NAWAKARIBISHA PPF
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,626
  Trophy Points: 280
  Marlenevdc
  Marlenevdc has no status.
  Junior Member Join Date: Wed Oct 2008
  Location: Dar-es-Salaam, Brussels, London
  Posts: 9
  Rep Power: 0

  Thanks: 0
  Thanked 4 Times in 4 Posts
  Credits: 1,043

  Re: Wafanyakazi 150 kufyekwa ATCL

  --------------------------------------------------------------------------------

  At last some people are waking up and opening their eyes!
  I have never stopped wondering why Kenya Airways has been expanding its business, increasing its services and in fact challenging Ethiopian Airways as the flag bearer of Africa. Nairobi at the moment is the hub of East, Central and South African air travels. Kenya Airways has stable constant connections with European capitals e.g. London, Amsterdam, Copenhagen etc.
  Air Tanzania??!! Nothing........
  2 planes with internal flights services with 250 employees. That is what was used to be called COMMUNIST ECONOMIC PRINCIPLES!!
  __________________

  R U SURE WITH BOLDED ONE; THEY HAVE 4 AIRCRAFT MA DEAR,.....DONT LISTEN POLITICS....WANATAKIWA WAKAE WAFIKIRIE NINI CHA KUFANYA
  Marlene vdc
   
Loading...