Wafanyabiashara watishia kufunga maduka zaidi

Wafanyabiashara watishia kufunga maduka zaidi

Hapo ongeeni mengi ya kejeli lakini Point za maana mnaleta masihala lakini msisahau kukumbushia mwaka huu kuna njaa kali sana jaribuni kuwakumbusha wakuu wasije kutukana kulima tumelima lakini jua ndo kiboko yetu yaani iandaliwe fungu la kutosha la kupambana na njaa, sijui itakuwa cku ya nyani kumkana Mwanae na hasa kanda yetu ilee ya upendeleo!
 
Kwanza na wafunge tu serikali pesa tunayo hatutegemei visenti vya wafanyabishara vya kodi na tunampango wa kuchapisha hela mpya na nchi itakuwa tajiri!
 
Ni sehemu gani na mkoa gani na mtaa gani maduka yamefungwa? Kama wameona ni vyema kufunga wafunge....
Mwanza mtaa wa rwagasore maduka hayana wateja wamachinga wamepanga vitu barabarani nje ya maduka yani wanauza kila kitu ambacho kipo dukani mbaya zaidi hawalipi kodi wala hawana leseni sasa unategemea wenye maduka wafanye nini!?
 
Wafunge wale nini! Jeuri hiyo wanayo?
Hamjamwelewa Minja. Yeye kasema maduka ni biashara rasmi na inayolipa kodi na kufuata taratibu zote za kibiashara. Lakini wanasumbuliwa sanawakati sasa hivi wapo wanaoitwa wamachinga lakini anabiashara inajaa kontena na hatoi risiti bali yeye anapanga biashara zake nje usiku anakusanya.
Nao watafunga maduka na kuweka biashara nje ili wawe na hadhi ya machinga. Kufunga duka sio kuacha biashara.
 
serekali ingilie kati kodi ya pango tunayotozwa na wenye nyumba .hili ni tatizo la haraka ambalo ni sehemu ya kufungwa kwa biashara .wenye nyumba kariakoo ni sawa na makupe ni wanyonyaji wa kuu .kwa sababu wanaringia wachina .wachina wamekua ni sehemu yabkupanda kwa kodi ya pango ya biashara .tunaomba tra ifanye utafiti wa siri kwa wafanyabiashara wazawa itagundua kitu
 
Mshaambiwa hii nchi ni ya viwanda sasa maduka ya nini?wafanyabiashara wa nini? Wacha tuisome namba weee lalalalala tumeipenda wenyewe
 
Wigo wa kodi ni mpana sana na biashara ni kama daladala wengine wanafunga wengine wanafungua. Wengi wa hao wanaofunga hawakuwa wanalipa kodi hivyo serikali mapato yako vile vile tena yanaongezeka sab wigo umezidi kupanuliwa kwa mfano maduka mengi yanatumia efd mahotel yote siku hizi ukienda na mchepuko unapata efd makampuni ya huduma za kuzoa takataka wanatoa risiti za efd baadhi ya daladala wanatoa risiti za efd hebu angalia wigo huo.
Embu tutajie makusanyo ya TRA ya mwezi Novemba 2016
 
Wewe utakuwa mshabiki maandazi wa chama chako cha kijani
Hakuna chama kingine cha kushabikia sab wapinzani hawajitambui. Wanapinga ufisadi huku wanakumbatia ufisadi. Wanatetea demokrasia wakati kwenye vyama vyao migogoro kila kukicha huku chaguzi zao zikikosa mwelekeo wa kidemokrasia. Wanapinga ukabila udini na ukanda huku wameupa kibali kwenye vyama vyao.
Ccm ni mbovu lkn upinzani mbovu zaidi.

Mtanzani yeyote aliyepevuka kiakili anayeweza kuchambua mambo na kutafakari kwa kina akiamua kuwa mshabiki wa chama unadhani atashabikia chama gani zaidi ya ccm? Chama kinachojua makosa na kasoro zake kinayataja hadharani kisha kuyafanyia kazi sio upande wa pili wao ni malaika hawakosei lkn migogoro inaibuka kila siku.
 
Wakifunga watakuwa wamemkomoa nani?
Kumbuka ukifunga biashara yako wewe ni hasara kwako na familia yako.
Serikalit itaendelea kupata mapato yake vile vile kwa sababu wateja waliokuwa wananunua bidhaa kwako watakwenda kununua kwa mtu mwingine.
Hivyo utakuwa umejikaanga wewe mwenyewe.
 
Wakifunga watakuwa wamemkomoa nani?
Kumbuka ukifunga biashara yako wewe ni hasara kwako na familia yako.
Serikalit itaendelea kupata mapato yake vile vile kwa sababu wateja waliokuwa wananunua bidhaa kwako watakwenda kununua kwa mtu mwingine.
Hivyo utakuwa umejikaanga wewe mwenyewe.
Aliposema wafanyabiashara 2000 wamefunga maduka alimaanisha hali ikiendelea hivi, wenye maduka wote watageuka machinga na serikali itayakosa mamilioni ya kodi kutoka kwao...
 
Kwa kawaida hawawezi kufunga maduka nchi nzima.
Wengi wao wana mikopo kwenye Mabank na wanatakiwa kurejesha kila baada ya muda fulani.
Mimi nawashauri wasifunge biashara zao kwani kwa kufanya hivyo wanawapaisha wafanyabiashara ambao hawajafunga biashara zao.
 
Wafunge tu maana hata wateja hakuna wafunge hata mwezi mmoja hivi
Ukweli ni kwamba hakuna biashara. Wachukue likizo. Waajiriwa wao wawape likizo bila malipo Kama sheria inaruhusu. Wasisahau kutoa taarifa TRA wasije wakadaiwa kwa muda wasiofanya biashara.
 
Back
Top Bottom