Wafanyabiashara watishia kufunga maduka zaidi

Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiasha kasema hali ilivyo,wewe unayetete ni nani vile,yawezekana ukawa akina pangu pakavu tia mchuzi! tujitambue
 
kama Rais angepata fursa ya kujibu hili tishio la wafanyabiashara unahisi angewajibuje ukirejelea majibu kwa mbunge wa wale waathirika wa tetemeko aliyeomba kupunguziwa bei za vifaa vya ujenzi?

Hapa kasi tu!

========

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, amesema wataendelea kufunga biashara, kama maeneo ya wafanyabiashara hayataboreshwa ili kuwavutia.

Minja alisema hayo jana kwenye mahojiano maalumu na kituo kimoja cha redio, kuhusu kufungwa kwa biashara Dar es Salaam. Alisema awali wakati Serikali inaingia madarakani, ilijipambanua kuwa itahakikisha watu wanalipa kodi, ili kukuza uchumi wa nchi.

Minja alisema walikubali mpango huo wa Serikali kutokana na malengo yake mazuri kwa wafanyabiashara ya kuleta ushindani kwenye biashara.
"Baada ya hapo, kuliibuka mfumuko wa kodi bandarini kutokana na mahesabu ya upitishaji mizigo,” alisema.

Alifafanua kuwa hakukuwa na kodi mpya, bali kilichofanyika ni kwa wenye mzigo bandarini kuongezwa thamani ambapo mwenye mzigo wa Sh milioni 30, alijikuta ukibambikiwa Sh milioni 200.

"Na hii si kodi mpya, bali ni yale mahesabu ya ushuru wa forodha," alisema na kuongeza kuwa baada ya kubaini hilo, walitembelea nchi mbalimbali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutafuta mbinu za kudhibiti ubambikiwaji wa thamani za mizigo.

Alitaja nchi walizotembelea kuwa ni Kenya na Uganda, ambako walikuta kodi zikikatwa kulingana na thamani halisi ya mzigo na hakukuwa na ubambikizaji.
Minja alisema kama uchumi wa nchi unakua, anaiomba Serikali ihakikishe ukuaji huo unamgusa mwananchi wa kawaida, ili kuondokana na malalamiko.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi kwa mwishoni mwa mwaka jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema pamoja na uchumi kukua kwa asilimia 7.2, baadhi ya wafanyabiashara walifunga karibu maduka 2,000.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, utafiti uliofanyika Dar es Salaam na Arusha kati ya Agosti na Oktoba mwaka jana, ilibainika katika wilaya ya Ilala wafanyabiashara wakifunga maduka 1,076.

Dk Mpango alisema kwa Kinondoni biashara 443 zilifungwa na kufuatiwa na Temeke, ambako biashara 222 zilifungwa huku Arusha, wafanyabiashara 131 wakifunga biashara zao.

Alitaja aina ya biashara zilizofungwa kwa wingi kuwa ni za sekta ya ujenzi na biashara ya jumla na rejareja na chache zikiwa kwenye huduma za usafiri.

Chanzo: Jambo leo
Mtanyooka tu mwaka huu..na Biashara zenu za madili madili the.rais endelea kushikilia hapo hapo tutafanana tu njia za mkato hakuna tena
 
Nyie wafanyabiashara makanjanja wakina minja tulieni sindano iwaingie
 
Kwanza baadhi ya sisi wafanyabiashara hatumtaki Minja ni kigeugeu sana huyu Jamaa mana alitugeuka kwenye risiti za mashine kama siyo yeye...inabidi aachie madaraka tu mana muda wake ushaisha hataki kuitisha uchaguzi mpya
 
Mtanyooka tu mwaka huu..na Biashara zenu za madili madili the.rais endelea kushikilia hapo hapo tutafanana tu njia za mkato hakuna tena
Ulishawai kubambikiwa makadilio ya mzigo au wewe mwenzetu mtumisi wa huma unahuhakika wa kupata mshahara mwisho wa mwezi.Bora unyamaze kuliko kuchangia biashara karibu 2000 zinafungwa kinaonekana kama wapiga dili unajua kitu kinaitwa multiplayer effect unapokuwa na wafanyibiashara 2000 wakifanya biashara?.
 
kama Rais angepata fursa ya kujibu hili tishio la wafanyabiashara unahisi angewajibuje ukirejelea majibu kwa mbunge wa wale waathirika wa tetemeko aliyeomba kupunguziwa bei za vifaa vya ujenzi?

Hapa kasi tu!

========

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, amesema wataendelea kufunga biashara, kama maeneo ya wafanyabiashara hayataboreshwa ili kuwavutia.

Minja alisema hayo jana kwenye mahojiano maalumu na kituo kimoja cha redio, kuhusu kufungwa kwa biashara Dar es Salaam. Alisema awali wakati Serikali inaingia madarakani, ilijipambanua kuwa itahakikisha watu wanalipa kodi, ili kukuza uchumi wa nchi.

Minja alisema walikubali mpango huo wa Serikali kutokana na malengo yake mazuri kwa wafanyabiashara ya kuleta ushindani kwenye biashara.
"Baada ya hapo, kuliibuka mfumuko wa kodi bandarini kutokana na mahesabu ya upitishaji mizigo,” alisema.

Alifafanua kuwa hakukuwa na kodi mpya, bali kilichofanyika ni kwa wenye mzigo bandarini kuongezwa thamani ambapo mwenye mzigo wa Sh milioni 30, alijikuta ukibambikiwa Sh milioni 200.

"Na hii si kodi mpya, bali ni yale mahesabu ya ushuru wa forodha," alisema na kuongeza kuwa baada ya kubaini hilo, walitembelea nchi mbalimbali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutafuta mbinu za kudhibiti ubambikiwaji wa thamani za mizigo.

Alitaja nchi walizotembelea kuwa ni Kenya na Uganda, ambako walikuta kodi zikikatwa kulingana na thamani halisi ya mzigo na hakukuwa na ubambikizaji.
Minja alisema kama uchumi wa nchi unakua, anaiomba Serikali ihakikishe ukuaji huo unamgusa mwananchi wa kawaida, ili kuondokana na malalamiko.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi kwa mwishoni mwa mwaka jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema pamoja na uchumi kukua kwa asilimia 7.2, baadhi ya wafanyabiashara walifunga karibu maduka 2,000.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, utafiti uliofanyika Dar es Salaam na Arusha kati ya Agosti na Oktoba mwaka jana, ilibainika katika wilaya ya Ilala wafanyabiashara wakifunga maduka 1,076.

Dk Mpango alisema kwa Kinondoni biashara 443 zilifungwa na kufuatiwa na Temeke, ambako biashara 222 zilifungwa huku Arusha, wafanyabiashara 131 wakifunga biashara zao.

Alitaja aina ya biashara zilizofungwa kwa wingi kuwa ni za sekta ya ujenzi na biashara ya jumla na rejareja na chache zikiwa kwenye huduma za usafiri.

Chanzo: Jambo leo
Minja?!!!
 
Ni sehemu gani na mkoa gani na mtaa gani maduka yamefungwa? Kama wameona ni vyema kufunga wafunge....
Dar na arachuga refer report ya hali ya uchumi mwishoni mwa mwaka jana.Usijitoe ufahamu kama hamna akiba ya magazeti Google utapata hiyo tarifa.
 
Lakini wakifunga labda sababu iwe ni hali ngumu, hakomolewi mtu.
 
Wayafunge tuu, Mfanyabiashara yoyote lazima uwe na plan A na B, A ikishindikana unakwenda B. Mi nimefunga naenda kulima na kufuga.
 
Wanaotaka kufunga maduka wasipate shida, waniambie niwasaidie kuyafunga, watayafungua 2025 nikitoka, by rais Wa Ghana. Nahisi hili lingekuwa miongoni mwa majibu
Rais wa ghana anekosa pesa ya kuendesha bajeti yake alioisoma kwa mbwembwe, amekimbilia kukopa kwenye bank za ndani ambazo kabla alisema zinaifilisi sirikali.
Sasa biasharavzikifungwa, hata pato la ndani litakosekana maana hakuna tena kodi ya kukusanya. Pengine ndio maana wale wakusanya ushuru wameshindwa kusoma taarifa yao ya wiki
 
Back
Top Bottom